· Juni, 2013

Habari kuhusu Sanaa na Utamaduni kutoka Juni, 2013

Jamaica: Watoto kama Wasanii

  11 Juni 2013

Blogu ya Maonyesho ya Sanaa ya Taifa Nchini Jamaika inayo msisimko kuhusu maonyesho yajayo ya sanaa ya watoto, ambayo yataonyesha “mwitikio wa pekee wa watoto kwa maswali kuhusu udadisi wao na msukumo wa aina tofauti wa ubunifu unaokua.”

Vijiwe Vya Usomaji Gazeti Mjini Mumbai Vyazorota

  8 Juni 2013

Vachanalays (vituo vya kusoma magazeti) ni jambo la kawaida katika vitongoji vingi mjini Bombay ambapo wenyeji husoma magazeti na kujadili habari zilizotokea siku husika. Sans Serif anaripoti jinsi vituo hivyo vinavyozidi kupitwa na wakati pole pole. Blogu hiyo pia inaonyesha picha nzuri inayojieleza ya mwanablogu wa picha M.S. Gopal juu ya maudhui hayo...

Alfabeti Hufurahisha na Kuhuzunisha Nchini Bulgaria

[…] Mojawapo ya likizo safi na takatifu zaidi nchini Bulgaria! Ni sherehe itupayo fahari ya kuwa tumetoa kitu chochote duniani! Ni likizo isiyohusiana na waasi wowote, vita, wala vurugu, ingawa hutujaza uzalendo na furaha. […] Unapotembea katika mitaa, mabango ya ugenini na maelekezo, yanazidi haya tuliyonayo kwetu kwa mbali sana...