· Julai, 2009

Habari kuhusu Sanaa na Utamaduni kutoka Julai, 2009

Afrika: Wanablogu wamwombolezea Michael Jackson

Barani Afrika, wanablogu wanatoa heshima zao za mwisho kwa Michael Jackson baada ya kifo chake hivi karibuni kwa kutuma picha, video za muziki, mashairi pamoja na tafakari. “Pumzika Kwa Amani” anaandika Mwanablogu wa Kenya WildeYearnings. “Sasa unalo anga zima kucheza kwa madaha kwa staili ya kutembea mwezini…”

Afrika Kusini: Kuvuvuzela au Kutovuvuzela?

Mjadala kuhusu kifaa maarufu kinachoitwa vuvuzela kinachopigwa na mashabiki wa mpira wa miguu Afrika Kusini umetawala katika blogu mbalimbali duniani tangu kuanza kwa Kombe la Mabara la mwaka huu nchini Afrika Kusini, lililohitimika wiki iliyopita. Waandishi wa habari, watazamaji wa televisheni, makocha na baadhi ya wachezaji wa kigeni walitoa wito wa kusitisha matumizi ya kifaa hiki katika Kombe la Dunia la 2010 nchini Afrika Kusini. Mabishano haya yana sauti kubwa kama chombo chenyewe.