Habari kuhusu Sanaa na Utamaduni kutoka Februari, 2009
Dunia Nzima: Lugha 2,500 Zinapotea
Ramani shirikishi ya lugha zinazopotea, inayoonyesha lugha 2,500 kati ya 6,000 ambazo ziko hatarini, imezinduliwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO). Shirika hilo la kimataifa linawaomba watumiaji wachangie kwa kutuma maoni kwenye mradi huo ambao unawatia mashaka wanablogu wengi wenye nia ya kuhifadhi tamaduni.
India: Filamu ya Slumdog Millionaire Yanyakua Tuzo za Oscar
Filamu ya Danny Boyle, Slumdog Millionaire, iliyotokana na kitabu chenye maudhui ya India imefanya vyema katika sherehe za 81 za tuzo ya Academy. Wahusika wake kutoka Uingereza na India walitia...
Jamaika: Miziki Yenye Maneno Machafu Yazuiwa
Utata wa muda mrefu juu ya usahihi wa kurushwa hewani kwa miziki fulani umezuka tena nchini Jamaika. Wanablogu wa Jamaika wanapaza sauti zao.
Karibeani Ya Kifaransa: Tamasha la Kanivali 2009 Lazinduliwa
Kanavali ni utamaduni, sehemu ya uhai wa kila Muhindi wa Magharibi bila kuwaacha wale wa Karibeani ya Kifaransa. Ufuatao ni muhtasari wa blogu kutoka Martiniki, Guyana ya Kifaransa, Haiti na Guadalupe, ambao unaelezea mambo yanavyokuwa kwenye Kanivali.
Kampuchea: Vikwazo Vya Intaneti Vyalenga Wasanii
Wizara ya Masuala ya Wanawake nchini Kampuchea imetishia kuizuia tovuti yenye michoro ya wacheza ngoma ya Apsara walio vifua wazi pamoja na mwanajeshi wa Khmer Rouge. Uchujwaji wa habari wa namna hii unawalenga wasanii wanaotambulika zaidi kwa uwepo wao katika mtandao wa intaneti.