Don Osborne anajadili habari iliyowekwa kwenye tovuti ya Chuo Kikuu cha Olivet Nazarene ikionesha ramani ya “Lugha za pili kuzungumzwa zaidi duniani.” Anaeleza matatizo makuu kutokana na habari hiyo:
Suala la kwanza ni kudhani kwamba “lugha inayozungumzwa zaidi kwenye nchi yoyote huwa wazi; mara nyingi, ni lugha ya taifa husika.” Barani Afrika hali ni tofauti, kama kusema “lugha inayozungumzwa zaidi” maana yake ni kuhesabu idadi ya wazungumzaji. Kwa mfano nchini Mali, ambapo hali ya lugha iliangaziwa kwenye blogu hii katika kutazama uzungumzaji wa lugha – Kibambara kinaonekana kuwa lugha maarufu kuliko hata lugha rasmi ya Kifaransa.
Lugha rasmi si kigezo kinachoaminika katika kupima umaarufu wa lugha barani Afrika, zaidi ya mukhtadha (muhimu) wa matumizi rasmi na umaarufu wake. Kwa mifano ya nchi hizo mbili, kuna masuala mawili yanajitokeza:
•Afrika Kusini inazo lugha 11 rasmi (tovuti ya Olivet imetaja Kizulu pekee kuwa lugha rasmi). Kwa hiyo moja wapo ya lugha rasmi inakuwa lugha ya pili kuzungumzwa. Pengine lugha hiyo inaweza kuwa ki-Xhosa kama inavyooneshwa, lakini mtazamo wa kutumia lugha rasmi kama kigezo hauonekani kufanya kazi katika mazingira haya.
•Rwanda ina lugha tatu rasmi (Kinyarwanda, Kifaransa, na Kiingereza), na Jamhuri ya Afrika ya kati inazo mbili (Ki-Sango na Kifaransa). Kwa sababu tovuti haijazingatia lugha hizi rasmi katika kujadili lugha za pili zinazozunguzwa zaidi, imejikuta ikidai kwamba Kiswahili ni lugha ya pili kuzungumzwa zaidi nchini Rwanda, na kwamba lugha za asili ndizo zinazotumika zaidi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati – jambo ambalo halitoi taswira halisi.
Soma sehemu ya pili ya hoja zake hapa.