Ili kuondoa uhaba wa hosteli kwa ajili ya wanafunzi unaovikabili vyuo vikuu barani Ulaya, baadhi ya vyuo vikuu nchini Denmaki, Ujerumani, Ufaransa (Le Havre) [fr] na Uhispania vimejaribu kubadili makontena na kuyafanya yawe hosteli za wanafunzi. Makontena yanaonekana kufaa kwa sababu hayana gharama kubwa na yanazoeleka kirahisi. Hata hivyo, taasisi kadhaa tayari zimeibua masuala kadhaa [fr] kuhusiana na mifumo ya kuyapasha “makazi” hayo joto pamoja na masuala ya usalama.
3 maoni