Habari kutoka 30 Januari 2014
UBUNIFU: Makontena Yatumika Kama Hosteli za Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Ulaya
Ili kuondoa uhaba wa hosteli kwa ajili ya wanafunzi unaovikabili vyuo vikuu barani Ulaya, baadhi ya vyuo vikuu nchini Denmaki, Ujerumani, Ufaransa (Le Havre) [fr] na Uhispania vimejaribu kubadili makontena na kuyafanya yawe hosteli za wanafunzi. Makontena yanaonekana kufaa kwa sababu hayana gharama kubwa na yanazoeleka kirahisi. Hata hivyo, taasisi kadhaa tayari zimeibua...
Shindano la Kuchochea Uanzishwaji wa Biashara Mpaya Nchini Madagaska
Harinjaka, mwanzilishi wa mradi wa Habaka na mwanablogu anayeishi Madagaska, ameanzisha Shindano la biashara mpya Antananarivo 2014 [fr] lenye lengo la kuchagua na kuunga mkono wazo la biashara nchini Madagaska. Anaamini kwmaba kuna mustakabali mzuri kwa ujasiriamali na ubunifu [fr] nchini Madagaskari. Hapa unaweza kuona tangazo la tukio hilo[fr] :
Mwaliko wa Mapendekezo ya Tuzo za Blogu Nchini Kenya 2014
Waandaaji wa Tuzo za Blogu nchini Kenya 2014, ambao ni Umoja wa Wanablogu nchini humo (BAKE) kwa sasa wanakaribisha mapendekezo ya wawaniaji wa tuzo hizo mpaka Februari 10, 2014. Watumiaji wanaweza kupiga kura kwa njia ya mtandao kuanzia Machi 1, mpaka April 30, 2014 kupendekeza blogu wanazoona kuwa ni bora...