Sabika Sheikh, Mwanafunzi wa Pakistan Aliyetaka Kuunganisha Nchi Mbili Auawa kwa Kupigwa Risasi

Mwili wa Sabika Sheikh ukifika Pakistan. Picha iliyochukuliwa kutoka video ya YouTube na Newsleak

Mazishi ya Sabika Sheikh yalifanyika katika mji wa nyumbani kwake karachi tarehe 23 Mei, 2018, siku tano baada ya mwanafunzi aliyepelekwa Marekani kwenye mpango wa elimu nje ya nchi kutoka Pakistani mwenye miaka 17 kuuawa na vijana wenye silaha ambao walipiga risasi shuleni katika jimbo la Texas.

Kwa ujumla watu 10 waliuawa akiwemo Sheikh na 13 kuumia katika vurugu hizo. Sheikh alikuwa ni mwanafunzi aliyekuwa Marekani kwenye mpango wa elimu nje ya nchi katika sekondari ya juu ya Santa Fe iliyopo chini ya Idara ya udhamini wa Ikulu ya Marekani programu ya KL-YES na alikuwa amepanga kurudi nyumbani tarehe 10, Juni 2018.
Habari za kifo chake zilitawala vyombo vya habari katika Pakistan, na salamu za rambirambi zilimiminika sana. Kabla ya mwili wake kupelekwa Pakistan, mazishi yalikuwa pia yafanyike Texas tarehe 20, Mei 2018.
Michael Mathes, mwandishi wa siasa za Marekani ofisi ya habari ya AFP alitwiiti:

Ni mauaji tu. Wahudhuriaji wa huduma za mazishi katika Stafford, TX muombee jeneza la Sabika Sheikh, mwanafunzi kijana wa Pakistani wa programu ya elimu nchi za nje Marekani aliuawa katika mauaji ya umma kwa kupigwa risasi katika shule yake ya sekondari ya juu karibu na Santa Fe

Kwenye mazishi yake wazazi walezi wa Sheikh walisema ambavyo alikuwa ameyabadili maisha yao:

Baba yake mlezi anazungumzia jinsi Sheikh alivyokuwa amewagusa katika maisha yao. Alimtaja kama zawadi nzuri ambayo ilitolewa kwa ajili ya maisha yake. Anasema mzizi wa kila kitu ni upendo. Anataka kuchukua mila na desturi za upendo aliotoka nao Pakistan.

Mama yake mlezi Joleen Cogburn kwa majonzi alieleza kitu kilichokuwa kimemumotisha Sheikh kusoma Marekani:

Nilimuuliza jinsi alivyojihusisha na kutaka kuwa mwanafunzi katika programu ya elimu katika nchi ya Marekani na kwa nini. Na alijibu ni kwa sababu nataka kujifunza utamaduni wa Marekani na ninataka Marekani kujifunza utamaduni wa Pakistan na ninataka tuwe wamoja na kuungana. Alisema sijui kama wanajua wanavyopaswa kutujua.

Kwa hisia zake juu ya kuchaguliwa kusoma Marekani, Sheikh alisema kupitia ujumbe wa video:

Watu walioko karibu yangu wameumia kidogo kwa kuwa nitakuwa nawaacha, lakini hii ni jambo zuri sana kutokea. Nilifurahai sana na bado nina.

Mara nying vyombo vya habari vya marekani huandika habari za Pakistan labda iwe vinafanya hivyo , kwa jicho la ugomvi. Mzaliwa wa Pakistan ambaye ni mtumiaji wa tweeter Marekani ni mmojawapo ya waliosema kuwa Pakistan mara nyingi huoneshwa kuwa nchi isiyo na usalama:

Wazo tu … binti huyu aliyezaliwa na kukulia hakufia katika nchi yake, haina maana kupambana na ugaidi. Amekuja na kufa kwa kupigwa na risasi shuleni ni kejeli Sabika Sheikh kupiga risasi shuleni Texas

Umma kupigwa risasi pamoja na shuleni ni tatizo kubwa katika Marekani. Kutokana na taarifa kutoka hifadhi ya vifo vinavyosabishwa na kupigwa na risasi (kupitia Vox), tangu mwaka 2012 karibu watu 1941 wameuawa na 7104 kujeruhiwa katika matukio 1686 ya umma kupigwa risasi, hii ina maana kwamba kila tukio watu wanne au zaidi (bila kuhesabu wafyatuaji wa risasi) wanakufa kwa kupigwa risasi muda na mahali palepale. Pia marekani ina kiwango kubwa cha mauaji ya binadamu kwa kupigwa risasi.

Wachambuzi wanasema sehemu ya tatizo ni urahisi wa kuingiza bunduki katika Marekani: nchi ina kiwango kikubwa cha kumiliki bunduki duniani .

Akiongea na vyombo vya habari, baba na mjomba wake waliomba seriakli ya Marekani kufanya shule kuwa sehemu salama kwa wanafunzi wao. Kwa kifo chake, mgogoro wa mauaji ya umma kwa risasi katiak nchi ya Marekani umekuwa ni jambo linalogusa mataifa.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.