Kudhibitiwa kwa Sanaa ya Michoro ya Uchi Kuna Maana Gani Kwetu na Mitandao ya Kijamii?

Ventana Vista Hacia La Sucre. Imagen por Erika Ordosgoitti.

Dirisha lenye madhari inayoelekea Sucre. Picha na Erika Ordosgoitti.

Michoro ya uchi, moja wapo ya mada za muda mrefu zaidi na zinazoendelea kuwa na umaarufu katika ulimwengu wa sanaa, imesababisha kusimamishwa kwa akaunti nyingi za mtandao wa facebook katika kipindi cha miaka kadhaa. Mfano wa hivi karibuni na uliotangazwa kwa kiasi kikubwa ni ule wa akaunti ya Jerry Saltz, msanii anayetumia sanaa kukosoa kupitia Jarida la New York. Mwezi uliopita, akaunti yake ilifungiwa kwa sababu aliweka michoro inayosemekana kuwa haina maadili, kwa mujibu wa vigezo na masharti ya mtandao huo.

Kwenye mitandao ya kidijitali, ‘kutokuwa na maadili’ mara nyingi humaanisha uchi au ngono. Kwa kilichomkuta Saltz, michoro ilisemekana kuwa na taswira ya ngono, kwa mujibu wa blogu ya New York Times inayoitwa ArtsBeat. Lakinikigezo hicho hicho kimetumika kuhakiki aina mbalimbali za michoro na picha, kuanzia ile ya akina mama wanaoonekana kunyonyesha mpaka kwa wasanii ambao kazi zao zinaonesha chuchu, sehemu za siri za kiume, na hata zile za kike. Via vya kike vinaonekana kuwa ndiyo michoro inayoongoza kupigwa marufuku kwenye mitandao ya kijamii, hata kwenye sanaa ya mchoro maarufu wa Gustave Courbet wa mwaka 1866 unaojulikana kama The Origin of the World. [Asili ya Ulimwengu].
Msanii wa sanaa za maonesho wa Venezuela Erika Ordosgoitti, ambaye kazi zake zinajikita zaidi kwenye maeneo ya mwili wa mwanamke, ni mfano mwingine wa mtu aliyekumbana na changamoto nyingi kwa sababu ya kuchapisha kazi zake za sanaa zenye kuonesha sehemu za siri kwenye mitandao ya kijamii. Miongoni mwa kazi nyingine, Facebook imefuatilia mchoro wa mwili wake mwenyewe ukiwa uchi kwa mara tano sasa.

Captura de pantalla del proceso de denuncia de contenido pornográfico en Facebook. Compartido por Erika

Picha ya taarifa kuhusu maudhui ya kingono kwenye mtandao wa Facebook ikisema kwamba picha ya Erika imelalamikiwa na hivyo, imefutwa. Imewekwa kwenye mtandao na Erika Ordosgoitti.

Maandishi hayo hapo juu, yanaeleza sababu za Fecebook kufuta picha hiyo na yanasomeka hivi: “Tumeikagua picha iliyolalamikiwa kwa kuonesha utupu au kuwa na maudhui ya kingono. Kwa sababu inakiuka Msharti na Vigezo vyetu, picha hiyo imeondolewa. Asante sana kwa kutujulisha. Tumemjulisha Erika Ordos kwamba tumefuta picha yake, lakini hatukumfahamisha nani aliwasilisha malalamiko. Facebook haina utaratibu wa kuweka wazi jina la mtu anayelalamikia maudhui.”

Global Voices ilimwuliza Ordosgoitti atusimulie uzoefu wake kuhusu kufuatiliwa kwa kazi zake kwenye majukwaa ya mitandao ya kijamii kwa lengo la kumdhibiti. Kuanzia hapo, tumeanza kufikiri namna watumiaji na wasimamizi wa mifumo ya mtandao wanavyoweza kuwezesha ufuatiliaji huu. Makala hii itakuwa ya kwanza katika mfululizo wa machapisho yatakayojadili namna mbalimbali za kushughulikia suala la kudhibitiwa kwa sanaa hii, kwa kutumia masimulizi ya Erika Ordosgoitti na wasanii wnegine waliobanwa na masharti na vigezo vya mitandao ya kijamii ikiwa ni pamoja na makubaliano ya kijamii.

Maonesho ya hivi karibuni ya Ordosgoitti, yaliyokuwa na jina la Comida de moscas (Chakula cha Nzi), yalikuwa ni mtazamo kuhusu ufuatiliwaji aliokumbana nao na namna alivyoweza kufanya kazi zake.

Tahadhari: Picha inayooneshwa hapa chini ina maudhui yenye lugha kali.

Los primeros años fue un fenómeno de redes. Continuamente me cerraban la cuenta, me bloqueaban, me advertían; yo deliberadamente insistía. Recibí muchos insultos y algunas pocas amenazas de muerte.

Katika mwaka wa kwanza, ukurasa wangu ulikuwa maarufu mno mtandaoni. Kila mara waliufunga ukurasa wangu, kunizuia kuitumia akaunti yangu na wakati mwingine kunionya, lakini bado niliendelea na kazi zangu kwa makusudi. Nilitukanwa sana na hata wakati mwingine kupata vitisho vya kuuawa.

Captura de pantalla 2015-03-18 a las 11.21.31

Video ikiwa na maneno yenye matusi aliyoyapata Ordosgoitti kutoka kwa watumiaji wa mtandao wa intaneti. Picha iliyotumiwa ni ya msanii na imechapishwa kwa ruhusa.

Msanii wa Venezuela Eliseo Solis Mora alijikuta kwenye hali kama hiyo si muda mrefu uliopita. Alifungiwa na Facebook kwa kuchapisha mchoro wenye sura yake—ukionesha sehemu za mbele za uchi wake ambao ni sehemu ya kazi zake za sanaa ya maonesho. Anaandika:

Las redes hoy son un medio complejo. Me han censurado en varias de ellas por los contenidos de mis fotos. En Facebook publiqué una imagen de Esther Ferrer y me bloquearon. Me volvió a ocurrir con un desnudo que luego dediqué a Ai Weiwei. En Instagram borraron automáticamente una imagen mía que fue denunciada…

Mitandao ya kijamii siku hizi imekuwa jukwaa gumu kulitumia. Nimefungiwa kwa sababu ya picha zangu. Kwenye mtandao wa Facebook, niliweka picha za Esther Ferrer na wakanifungia. Imetokea tena kwa mchoro niliokuwa nimeuchapisha kwa heshima ya Ai Weiwei. Kwenye mtandao wa Instagram, picha yoyote inayolalamikiwa hufutwa mara moja.

Walalamikaji habaki kuwa siri

Ordosgoitti anasema wasanii hufungiwa au kufuatiliwa shauri ya malalamiko yanayotoka kwa watumiaji wengine wa mtandao wanaoona mashapisho yao.

He tenido ya unas siete cuentas diferentes en Facebook. En la actualidad conservo dos, una oficial y otra alternativa, por lo general una de ellas está bloqueada, entonces uso la otra para superar el bloqueo

Nimewahi kuwa na akaunti kama saba tofauti za mtandao wa facebook. Kwa sasa nina akaunti mbili: moja rasmi na nyingine ni mbadala, na mara nyingi moja wapo hufungiwa, kwa hiyo ninatumia nyingine kukabiliana na hali hiyo.

Msanii huyo anasema vigezo vya kufuatiliwa havizingatiwi sana na havitumiki kwa usawa. Anabainisha kwamba watumiaji wanaotoa malalamiko yasiyo na maana hawaadhibiwi:

Responsabilizo de esta censura en primer lugar a Facebook porque sus políticas promueven conductas de sapeo [delación] anónimo. Considero que esta política es injusta, porque no me da derecho de saber quién me está denunciando ni sus razones […] Al denunciante se le agradece, sin saber si su denuncia es válida. Aunque las condiciones de publicación son claras, las razones de censura no lo son, porque en la actualidad (no siempre fue así) se supone que sus intenciones son excluir la pornografía o imágenes sexuales explícitas, por lo tanto quedarían exentas las imágenes científicas o artísticas pero ¿cómo diferenciar imágenes pornográficas o vulgares de imágenes artísticas?

Mtandao wa Facebook ndio wa kwanza kabisa kulaumiwa kwa mtindo huu wa kufuatilia watumiaji wake kwa sababu sera zao zinalinda malalamiko yanayoficha jina la mlalamikaji. Ninaamini sera hii haina haki, kwa sababu hainipi fursa ya kujua nani ananiharibia na kwa sababu gani […]. Wao humshukuru mtumiaji anayelalamika, bila hata kujua kama alichokilalamikia kina mantiki. Ingawa masharti ya kutumia yako wazi sana, sababu zinazoweza kutumiwa kwa ufuatiliaji haziko wazi, kwa sababu siku hizi (na imekuwa hivi siku zote) inaaminiwa kwamba nia kufuta kabisa picha za ngono au zenye maudhui ya kimapenzi, sera ambazo inaweza kuhusisha hata picha za kisayansi au za sanaa. Lakini unawezaje kutofautisha picha za ngono na zile za sanaa?

Uamuzi wa mtandao wa Facebook kuficha utambulisho wa wale wanaolalamikia picha unatoa taswira ya kufanya mambo haya kuleta migogoro kwa watumiaji wa mtandao huo. Lakini pia inaleta changamoto mpya, kama wasanii wanavyoonesha.

Solís Mora, ambaye picha za mwili wake zimekuwa zikifuatiliwa kwa lengo la kudhibiti kazi zake, anaona vigezo vya kufuatilia picha za sanaa kwenye mitandao ya kidigitali haikuzi demokrasia:

…las celebridades tienen mayores libertades. Prueba de ello es el famoso wallpaper de Kim Kardashian exhibiendo el trasero, que se volvió viral a través de las redes sociales. Hay algo interesante que uno nota nada más al abrir el Instagram: a diario se publican este tipo de imágenes, que tienen miles de likes y son sexismo puro, pero hay obras de arte que son automáticamente bloqueadas…

…watu maarufu wana uhuru zaiidi. Ushahidi wa hili ni picha inayomwonesha Kim Kardashian akionesha makalio yake iliyosambaa sana kwenye mitandao ya kijamii. Kuna jambo la kufikirisha unapofungua mtandao wa Instagram: kuna picha za kingono zinazochapishwa kila siku zenye maelfu ya watu wanaoweka alama ya kuvutiwa nazo wakati kazi za sanaa zikizuiwa bila mjadala…

Hivi karibuni Solís Mora alichapisha tahadhari —au ilani—kwenye ukurasa wake wa Facebook:

Sí en esta cuenta, que en gran medida está manejada como herramienta de trabajo, me desnudo y tú que lees (sé no son tod@s) la denuncias o sencillamente no te gusta, pasa la página…Recomiendo entonces que si eres mi amigo o amiga virtual, entiendas que soy un artista y mi libertad creadora es total, aquí solo muestro arte.

Kama kwenye akaunti hii, ambayo inatumika kama zana ya kazi zaidi, ninaonesha mwili wangu ukiwa uchi na kama wewe, mpendwa msomaji wangu, usingependa kuona picha hizo, funga ukurasa…ninashauri, kwamba kama wewe ni rafiki yangu au mtu tunayewasiliana mtandaoni, jaribu kuelewa kwamba mimi ni msanii mwenye uhuru kamili w akiubunifu na kwmaba ninachokionesha hapa ni sanaa.

Kama ilivyo kwa Ordosgoitti, Mora amekuwa akidhalilishwa na hata kupata vitisho vya kifo kwa sababu ya kazi zake. Kwake, ufuatiliaji unaofanywa kwa lengo la kudhibiti kazi zake kutoka kwenye taasisi za utamaduni limekuwa ni jambo ambalo amejifunza kushughulika nalo, lakini vikwazo kwa uhuru wa kazi zake za sanaa mtandaoni, anasema, vinaendelea kuongezeka:

El problema va más allá de la mera denuncia, es la imposibilidad de ser libre. Sin embargo, me gusta que hoy se hable del desnudo, aún cuando es el tema más antiguo del arte…

Tatizo ni zaidi ya kulalamikiwa—tatizo halisi ni kukosekana kwa uhuru. Hata hivyo, ninapenda kusikia watu wakizungumzia sanaa ya uchi, hata kama ni mada ya zamani sana kwenye ulimwengu wa sanaa…

Maelezo ya Mhariri: Makala haya yalianzisha mjadala wa pamoja kuhusiana na sanaa ya uchi kwneye ukurasa wetu. Wakati wenzetu walitaka kuambatanisha kazi zinazozungumziwa hapa, wengine walikuwa wazito. Kwa hiyo, kwa kutumia mazungumzo hayo, tulifungua mjadala kwenye blogu ya jamii yetu. Unaweza kuona mjadala hapa na kuongeza mawazo yako kwenye kisanduku cha maoni.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.