India: Ugaidi Waikumba Pune

Picha kwa hisani ya http://twitpic.com/photos/abhi_bol

Picha kwa hisani ya http://twitpic.com/photos/abhi_bol


Mnamo majira ya saa 1:30 jioni (Februari 13, 2010) mlipuko wa bomu uliua watu 9 na kuwajeruhi wengine 57 katika mgahawa maarufu kwa watalii uliopo katika mji wa Magharibi wa Pune, India. Bomu hilo lilikuwa katika mkoba wa mgongoni na lililipuka wakati mhudumu alipojaribu kukagua mzigo huo. Shashi Bellamkonda anaripoti katika My Digital Thoughts:

Masaa machache yaliyopita (tarehe 13 Februari, 2010) bomu lililipuka katika mgahawa wa ‘Tanuri la Ujerumani’ mjini Pune, India. Wakati wa kutuma makala hii vyombo vya habari vilikuwa vinaripoti kuwa watu 8 wamefariki na wengine 40 wamejeruhiwa katika mlipuko huo ambao uliiacha miili ikiwa imekatwakatwa na haitambuliki. Tanuri hilo la mikate ni maarufu kwa watalii kutoka nje.

Kadhalika Shashi alibaini haya yafuatayo:

• Hili limetokea siku moja baada ya India na Pakistani kukubaliana kuanza tena mazungumzo ambayo yalikuwa yamesitishwa tangu mashambulio ya mjini Mumbai mwaka 2008. (Miezi 14 iliyopita)
David Headley ambaye yuko jela mjini Chicago alitembelea Pune kukagua eneo la utawa la Osho karibu na neo la mlipuko
• Eneo la mlipuko lipo karibu na jumba la Chabad huko Pune na jumba la Chabad la Mumbai lilikuwa ndio kusudio la mashambulizi ya 26/11 mwaka 2008.
• Eneo la mlipuko lipo karibu na eneo la utawa la Osho linalitembelewa sana na watalii, jambo ambalo linafanana na mlipuko wa Mumbai.

Pragmatic Euphony anaonya:

Wana-jihadi wameshambulia tena ndani ya bara Hindi; hivi sasa huko Pune, japokuwa ni zaidi ya mwaka mmoja baada ya mashambulizi mabaya ya kigaidi mjini Mumbai ya mwezi Novemba 2008. Hisia za awali, wakati tukifuata dhana maarufu inayowezekana ya kwamba mlipuko huo ulikuwa ni kazi ya makundi ya jihadi yenye makazi nchini Pakistani, ni hisia za hasira. Pengine inaweza kueleweka kwa nini jazba zinaweza kupanda sana. Nahisia hizi zinaweza kuongezeka zaidi kwa vile vyombo vikuu vya habari vya India vinahaha na kukimbia kila mahali na matangazo yake yaliyokithiri ya tukio hilo.

Watu tayari wameshaanza kugundua uhusiano (wa tukio hilo) na Pakistani. Offstumped anataarifu kuwa mlipuko wa Pune ulifuatia vitisho vya Laskar-e-Taiba. Kiongozi wa juu wa Lashkar-e-Taiba aliitaja Pune kama mji unaolengwa katika maandamano ya umma yaliyoruhusiwa huko Pakistani. The Acorn anasema:

Pamoja na tishio la la Lashkar-e-Taiba, ni mapema mno kuhusisha shambulio hilo kwa uhakika na mfumo wa uanajeshi wa jihadi wa Pakistani. Lakini ni wazi kwamba mfumo wa uanajeshi wa jihadi wa Pakistani una sababu zote za kuzidisha mfarakano na India kwa njia ya ugaidi. Bila ya kisingizio cha “mfrarakano wa Mashariki”, Pakistani haitabakia na chochote ambacho itaweza kuifafanulia Washington kuhusu ushirika wake na taliban.

Dilip D'Souza katika Death Ends Fun anatukumbusha kuwa India inapaswa kuchukua hatua kuhusu ugaidi ulioasisiwa ndani ya nchi:

Mpaka hapo tutakaupotambua ugaidi ulioasisiwa ndani ya nchi kwa jinsi ulivyo – na si pungufu ya ule ulioletwa kutoka nje ya nchi – na mpaka pale tutakaposimama dhidi ya ugaidi wa ain azote, hatutaweza kuushinda ugaidi.

Ulimwengu wa Twita uliunguruma na jumbe za twita na zile zilizotumwa tena na tena kusambaza habari hii. Hay ani baadhi ya maoni:

IndiaHappening: Tisa wameuwawa, 32 wameumia katika mlipuko wa kigaidi Pune http://bit.ly/arLssZ #India

r_shekhawat: ugaidi wautikisa mji wangu – ‘Pune’: kwa mara nyingine tena, watu wasio na hatiawameuwawa na magaidi wasio na akili. Pune, mji mzuri sana, umeumizwa na kuchunwa.

pragmatic_rebel: Ni mwanzo wa kusikitisha kwa siku ya Valentino huko #Pune! Bado katika mshtuko wa mlipuko #India inafanya jambo tofauti kabisa wakati huu.

bhuvan_chelsea: Tunahitaji askari wa kujitolea (sungusungu) kama batman hapa #India. ;-)

tweetSAMRAT: Anawaombea waliodhurika na mlipuko wa bomu huko Pune.

nehasasi: RT @deepitganjoo: taathali tuma tena ujumbe huu hospitali ya jahangir mjini pune inahitaji damu ya Blood AB+ve na B+ve Wasiliana na: 1066 kwa wale walioko pune… tafadhali

_india_: Mlipuko wa Pune unatia kivuli juu ya mazungumzo na Pakistani

Bila ya shaka mlipuko wa pune utaathiri mazungumzo ya kujenga imani kati ya India na Pakistani. Lakini inaonekana kuwa magaidi wanapewa nguvu kwa vile hisia zinavyopanda juu kila mahali.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.