Ufaransa: Tuzo ya Fasihi Yaja na Masharti

Mwanzo wa msimu wa Fasihi ya Kifaransa mwaka huu ulishuhudia mwandishi wa riwaya na michezo ya kuigiza mwenye asili ya Kisenegali na Kifaransa Marie N’Diaye akipewa tuzo iliyosuburiwa sana ya Prix Goncourt. Lakini, N’Diaye na familia yake walikwishahamia mjini Berlin miaka miwili iliyopita, hasa kutokana na siasa za rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy. Mwaka jana, jopo la tuzo hii yenye hadhi walizusha hisia kali pale walipomchagua mwandishi wa Kiafghani Atim Rahimi, kwa kitabu chake cha Kifaransa, Syngué Sabour. Je hii itakuwa ni fursa nyingine ya kusherehekea mchanganyiko wa aina mbalimbali katika jamii inayobadilika ya Kifaransa? Au itakuwa ni wasaa utakaoharibiwa na utete wa tukio?

DW-World anaeleza:

Katika mahojiano na gazeti la “Inrockuptibles” kiangazi kilichopita, N’Diaye alisema kuwa aliamua kuondoka Ufaransa na kuhamia Berlin mwaka 2007 ‘kwa kiwango kikubwa kutokana na Sarkozy”

Sakata hilo lilianza baada ya Eric Raoult, mtungasheria na mwanachama wa chama tawala cha Sarkozy, UMP, aliandika barua kwa waziri wa utamaduni wiki iliyopita akishauri kuwa N’Diaye akumbushwe “wajibu wa kujiheshimu” ambao unaambatana na tuzo ya Goncourt.

Katika kutoa majibu, wenye nguvu katika sekta ya utamaduni walishutumu kuwa kuna uchujaji katika malumbano haya. Bernard Pivot, mwanachama katika jopo la Goncourt, alimshutumu Raoult kuwa hafahamu chochote katika uwanja wa fasihi.

N’Diaye, aliyezaliwa mwaka 1967 na mama Mfaransa na baba Msenegali, alishinda tuzo ya Goncourt kutokana na riwaya yake “Trois femmes puissantes” (”Wanawake watatu wenye nguvu”), hadithi inayohusu wanawake waliojikuta katikati ya Ufaransa na Senegal na katika mkasa wa dhiki mbaya ya uhamiaji usio halali kutokea Afrika.

“Hadithi ya hawa wahamiaji imesimuliwa mara nyingi kabla, lakini kama hii itawasaidia watu kufahamu hatima yao vyema zaidi, basi nitafurahi,” alisema N’Diaye.

Ni kitu gain kilichochochea hasira ya Eric Raoult? Si pungufu ya mahojiano ya mwanamke huyu mwandishi, wakati alipojibu swali la gazeti la Les Inrocks: “Je unajisikia vizuri katika Ufaransa ya Sarkozy?” alisema [Fr]:

« Je trouve cette France-là monstrueuse. Le fait que nous (avec son compagnon l’écrivain Jean-Yves Cendrey, et leurs trois enfants – ndlr) ayons choisi de vivre à Berlin n’est pas étranger à ça. (…) Je trouve détestable cette atmosphère de flicage, de vulgarité… »

Naiona aina hiyo ya Ugfaransa kuwa mbaya isiyovumilika. Ukweli kuwa sisi (N’Diaye, mpenzi wake, mwandishi Jean-Yves Cendrey, pamoja na watoto wao watatu) tuliamua kuishi mjini Berlin unahusiana na hili. (…) Naiona hali hii ya ulinzi mkali na tabia chafu inakifu…”

Mwanablogu wa sheria anayejulikana Maître Eolas anayabomoa bomoa madai ya Bw. Raoult katika makala ya kejeli iliyoandikwa kwa mantiki nzuri [Fr], na hatimaye anamtunukia tuzo ya “Prix Busiris” (“buse” inaweza ikatafsiriwa kama “upumbavu”)

Kwanza anasahihisha makosa ya sarufi:

Tout d’abord, et le ministre de la culture et de la communication aura rectifié de lui-même, le devoir de réserve ne peut en tout état de cause être dû aux lauréats mais dû par les lauréats : cette erreur de préposition fait du lauréat le créancier alors que dans la tête du député, il en serait évidemment le débiteur.

Kwa kuanzia, na Waziri wa Utamaduni na Mawasiliano hawezi kusahau kujisahihisha, wajibu wa kujizuia hauwezi katika mfano wowote kuwapa wajibu waliopokea tuzo, lakini badala yake huwajibika kwa waliopokea tuzo; mapendekezo haya yenye makosa yanamfanya aliyepokea tuzo kuwa kama mkopaji wakati katika mawazo ya mbunge anakuwa kama vile ni mkopeshaji.

Na kisheria? Kati ya maandishi, mwanablogu ananukuu Tamko la Haki za Mtu na za Raia la mwaka 1789 pamoja na Makubaliano ya Haki za Binaadamu ya Nchi za Ulaya. Na “Wajibu wa Kujizuia au Kujiheshimu” huwa unawawajibisha watumishi wa umma?

Le devoir de réserve est souvent invoqué à tort et à travers par des gens qui n’y ont rien compris comme interdisant à un fonctionnaire de s’exprimer, y compris parfois sur des affaires purement privées.

Wajibu wa Kujizuia auKujiheshimu huwa unatolewa hovyo hovyo na watu ambao hawafahamu lolote juu ya wito huo, kama vile kumkataza mtumishi wa umma asiongee, mara nyingine hata kuhusu mambo binafsi.

Mwanasheria anahitimisha kwa kutoaminika kwa mbunge, kabla ya kutoa pigo la mwisho:

Ajoutons à cela qu’en 2005, en tant que maire du Raincy, lors des émeutes de l’automne, il fut le premier à proclamer l’état d’urgence dans sa commune pourtant épargnée par les actes de violence afin de griller la politesse au premier ministre, ce qui montre une certaine tendance à la gesticulation inutile pour attirer l’attention sur lui.
Ce qui établit en même temps le mobile d’opportunité politique, et emporte la décision.

Hebu tuongeze juu ya yote haya ukweli kwamba mnamo mwaka 2005, kama Meya wa Le Raincy, wakati wa machafuko ya kipupwe, alikuwa wa kwanza kutoa tamko la hali ya dharura ndani ya mji wake, na aliponusurika na machafuko hayo, alimzunguka Waziri Mkuu, jambo ambalo linanyonyesha tabia yake ya vitendo visivyo na maana ili watu wamuangalie.

Jambo ambalo wakati huo huo linathibitisha kuwa sababu kubwa ya kuchukua uamuzi ni kutaka kunufaika kisiasa.

Wanablogu wengine pia walikuwa na maneno makali.

Kwenye Art contemporain, la peau de l'ours, Philippe Rillon anaandika [Fr]:

Nous comprenons fort bien que le devoir de réserve s’impose à tout serviteur de l’Etat; mais depuis quand la littérature et les auteurs sont ils assimilés aux fonctionnaires avec leurs droits et devoirs?
Nous avions déjà une “Culture administrée”, nous voici maintenant “artistes fonctionnaires” comme si Paris était Berlin-est d’avant la chute du mur…
(…)
Il serait quand même étonnant qu’au lendemain d’une hyper-médiatique commémoration de la chute du mur, ce godillot vienne gâcher le spectacle idylique des dominos qui tombent.

Tunaelewa vyema kuwa wajibu wa kujizuia ni sheria kwa kila mfanyakazi wa dola; lakini tangu lini fasihi na waandishi wamewekwa kwenye kundi sawa na watumishi wa umma pamoja na haki na wajibu wao?
Tayari tunao “utamaduni wa serikali”, na sasa tumegeuka kuwa “wasanii wa dola”, kana kwamba mji wa Paris umekuwa Berlini ya Mashariki kabla ya ukuta kuvunjwa…
(…)
Je isingekuwa jambo la ajabu siku baada ya kusherehekea kuanguka kwa ukuta, mshabiki huyu angeliweza kuharibu muonekano mzuri wa kete zilizokuwa zinaanguka.

Wakati huo huo, Marie N’Diaye baada ya jitihada za kushusha ukali wa maneno yake katika mahojiano na Radio Station Europe 1, ambayo katikati ya mzozo watu hawakuyaona, alimuomba Waziri wa Utamaduni wa Ufaransa, Frederic Miterrand. Waziri huyo ameuchukulia mzozo huo kuwa ni kitu kigogo na cha kijinga” [Fr], na wahusika wakuu wameshikilia misimamo yao. [Fr]

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.