Uchaguzi wa India 09: India Imepiga Kura, Imeamua kuimarisha Utulivu

Makala hii ni sehemu ya makala maalum za Global Voices za uchaguzi wa India 2009

Matokeo ya Uchaguzi yanamiminika kutoka kila upande wa nchi na ni dhahiri kwamba India imepiga kura kwa kishindo ili kuchagua serikali imara ya mseto ya UPA, chini ya uongozi wa chama cha Congress. Dr Manmohan Singh atakuwa Waziri Mkuu kwa mara ya pili mfululizo. Hata kabla matokeo hayajafika, kwa kuangalia tu mwelekeo, kundi la vyama vya mseto la NDA linaloongozwa na chama cha BJP limetangaza rasmi kushindwa kwake katika uchaguzi.

Mwenyekiti wa UPA, Mama Sonia Gandhi aliwapongeza wapiga kura kwa kuwapa dhamana hii. Katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika nyumbani kwake saa 10 jioni Gandhi alisema, “Watu wa India wanafahamu ni nini kizuri kwao na wamefanya uteuzi sahihi.”

Mpaka hivi sasa (saa 11.45 jioni) matokeo kitaifa ni kama ifuatavyo:

Jumla ya viti = 543

Idadi ya viti vinavyotakiwa ili kushika hatamu = 272

————————————————————–

Mseto wa vyama wa UPA – wanapoongoza+waliposhinda = 258

Mseto wa vyama wa NDA – wanapoongoza+waliposhinda = 162

Mseto wa 3 – wanapoongoza+waliposhinda = 68

Wengine (vikijumuishwa vyama vya mseto wa 4) wanapoongoza+waliposhinda = 55

——————————————————————————————-

Uchaguzi wa India (#indiavotes09) ndiyo mada inayoongoza kwenye huduma ya Twita leo hii. Haya ni maoni ya baadhi ya watumiaji wa huduma hiyo:

@jraghu – Wananchi wa India wametoa hukumu. Ushindi wa mseto wa UPA unaoongozwa na chama cha Congress ni salama, uchaguzi huru katika demokrasia kubwa zaidi. Ahsanteni nyote Iindia # Indiavotes09

@dina – dhamana hii ni kwa ajili ya utawala bora – utulivu & maendeleo & matumaini mema tofauti ya hofu. Utawala na si uana siasa. #indiavotes09

@calamur – #indiavotes09 – Singh ni mfalme – Advani dhidi ya PM. Ulalamishi dhidi ya ushupavu. Roho ya chuki dhidi ya maono. Kupenda ukubwa dhidi ya wajibu. India imechagua vizuri.

Wakati kuna chereko chereko sehemu mbalimbali, pia kuna masikitiko kati ya wanaokiunga mkono chama cha BJP. Mwanablogu Chakresh Mishra anaandika katika blogu yake:

[…]moyo wangu mkubwa wa huruma upo na BJP, chama ambacho nilikipigia kura. Chama cha Kizalendo. Ni aibu kwa BJP. Rafiki zangu, kuna wakati katika historia ya taifa ambapo kila kitu huonekana kimepotezwa na nguvu za kiza zimeshinda vita kuu ya mwisho. Lakini rafiki zangu wapendwa, huu ni mchakato, ambao unaendelea. Miaka 5 inaweza ikawa ni muda wa muhimu sana katika maisha ya binaadamu, lakini katika maisha ya taifa (na taifa kama India) ni sawa tu na kupepeseka kwa jicho.

Kipindi cha baada ya kushindwa siyo wakati wa maasikitiko na kutupiana lawama. Ni wakati wa kujichunguza na kuanza kujipanga ili kuibuka kama mshindi katika vita ijayo.

Japokuwa matumaini yamevunjwavunjwa na majinamizi bado yanatawala, mapambazuko yatawadia tu. Hii si siku ya kwanza ya giza katika historia ya India, tulijikusuru na kupigana. Na tufanye hivyo tena.

Habari mpya:

Matokeo saa 7 mchana tarehe 17/05/09:

Jumla ya viti = 543

Idadi ya viti vinavyotakiwa ili kushika hatamu = 272

————————————————————–

Mseto wa vyama wa UPA – wanapoongoza+waliposhinda = 262

Mseto wa vyama wa NDA – wanapoongoza+waliposhinda = 157

Mseto wa 3 – wanapoongoza+waliposhinda = 67

Wengine (vikijumuishwa vyama vya mseto wa 4) wanapoongoza+waliposhinda = 57

——————————————————————————————-

Mseto wa UPO unahitaji kuungwa mkono kwa viti 10 tu. Je ni nani watakayemualika kujiunga na kundi lao? Kaa chonjo.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.