20 Mei 2009

Habari kutoka 20 Mei 2009

Uchaguzi wa India 09: India Imepiga Kura, Imeamua kuimarisha Utulivu

  20 Mei 2009

Matokeo ya Uchaguzi yanamiminika kutoka kila upande wa nchi na ni dhahiri kwamba India imepiga kura kwa kishindo ili kuchagua serikali imara ya mseto ya UPA, chini ya uongozi wa chama cha Congress. Dr Manmohan Singh atakuwa Waziri Mkuu kwa mara ya pili mfululizo. Hata kabla matokeo hayajatimia, kwa kuangalia tu mwelekeo, kundi la vyama vya mseto la NDA linaloongozwa na chama cha BJP limetangaza rasmi kushindwa kwake katika uchaguzi.