Habari kuhusu Cuba

Mazungumzo ya GV: “Mtandao wa Twita” wa Siri wa Kimarekani Nchini Cuba

GV Face  4 Aprili 2014

Mpango wa siri wa Marekani wa kubadili utawala nchini Cuba wenye huduma ya ujumbe inayofanana na Twita iitwayo ZunZuneo sasa unaangaliwa kwa mashaka baada ya kuwepo kwa taarifa kuwa maelfu ya wa-Cuba walidanganyika kujisajili kupata huduma hizo. Je, kutakuwa na madhara kwa wanaharakati wa kidijitali duniani kote? Wengine wana mashaka...

Cuba: Madiba Alifanya Mengi Mazuri Pamoja na Mapungufu Aliyokuwa Nayo.

  19 Disemba 2013

Blogu ya Cuba Without Evasion yatanabaisha kuwa, namna pekee ya kumuenzi Nelson Mandela ni kwa “kuiga mfano wake wa kusamehe na Usuluhishi”: Ninakusamee…kwa urafiki uliokuwepo kati yako na…dikteta aliyekuwa muovu kiasi ambacho watu wangu hawakuwahi kuushuhudia…kwa kuweka mkono wako– kwa ajili ya kuwaokoa watu wako- kwenye mabega yavujayo damu ya...

Caribbean: Kwaheri, Nelson Mandela

  10 Disemba 2013

Tangazo la kifo cha Nelson Mandela limepokelewa kwa mshtuko. Wanablogu wa maeneo mbalimbali wanashirikishana mawazo yao kuhusu kuondoka kwa mmoja wa magwiji wa upinzani kwa njia za amani duniani aliyetutoka.

Madaktari 400 wa Cuba Waenda Brazil

  3 Oktoba 2013

Daudi Oliveira de Souza, daktari na profesa wa Taasisi ya Utafiti wa Hospitali ya Sirio-Libanés, alituma barua ya wazi kwa madaktari zaidi ya mia nne wa Cuba ambao hivi karibuni waliwasili nchini Brazil wanaoanzisha kundi la kwanza la jumla ya madaktari 400 ambao wanatarajiwa kuja nchi hii kabla ya Desemba mwaka huu....

Cuba: Maandamano yafanyika Mara Mbili, Wengi Wakamatwa

  7 Julai 2012

Kikundi cha wanawake kijiitacho ‘wanawake wavaliao mavazi meupe’ (Ladies in White) kwa mara nyingine wametawala fikra za wanablogu wa Cuba waishio nje ya nchi. Maandamano ya amani ya kikundi hicho ambacho ni moja wapo ya vyombo vya upinzani vinavyoheshimika zaidi katika visiwa hivyo –pamoja na kukamatwa kwao mara kwa mara na vyombo vya dola –yanaendelea kuvuta hisia za watu. Mapambano ya hivi karibuni yalitokea mwishoni mwa juma lililopita wakati wanachama wa kikundi hicho walipojaribu kufanya maandamano mara mbili mjini Havana.

Cuba: Ukweli wa Sanchez Kutiwa Mbaroni Waibuka

  8 Novemba 2009

Kukamatwa, kupigwa na kuachiwa huru kulikofuata kwa wanablogu Yoaní Sánchez, Claudia Cadelo na Orlando Luis Pardo kulikofanywa na majeshi ya usalama ya Cuba tarehe 6 Novemba, kunapata matangazo mengi katika vyombo vikubwa vya habari na katika ulimwwengu wa blogu pamoja na ule wa Twita. Yoani ameandika (es) kuhusu tukio hilo...

Yoani Sanchez Pamoja na Wanablogu Wengine wa Cuba Wakamatwa na Kupigwa

  8 Novemba 2009

Jioni ya tarehe 6 Novemba, blogu ya Babalú iliweka kiungo kuelekea makala iliyoandikwa na Penultimos Dias (es) ilitoa taarifa kuwa baadhi ya wanablogu mashuhuri wa Cuba, wakiwemo Yoaní Sánchez na mchangiaji wa Global Voices Claudia Cadelo, walitiwa mbaroni na majeshi ya usalama. Habari mpya kutoka kwa Penultimos Días zinataarifu kuwa...