Mamia ya watu walikusanyika kwenye bustani ya jiji la Havana, makao makuu ya Cuba, JUmapili iliyopita kushiriki kwenye zoezi la ugawaji wa vitabu. Mradi huo, uliongozwa na mwanablogu [es] na mwandishi wa Global Voices Rafael González [es], ulikusudia [es] kuviacha vitabu mahali kokote kwenye bustani hiyo vikiwa na maelezo kwenye ukurasa wa kwanza yanayosomeka: “Kitabu hiki kinamilikiwa na yeyote atakayekipata na kukigawa kifurahiwe na wengine baada ya yeye kukisoma.”
Mradi halisi, ulianza kwenye mtandao wa Facebook [es], na kuchukuliwa na González, aliyewasiliana na waanzilishaji. Lu Di Piertro alitoa maoni kuhusu mradi huo:
La idea no es nuestra, ya existe desde hace un tiempo y no sé exactamente quién la empezó. Un amigo, Rodri, que está también de organizador de este evento pensó en armar una suelta masiva y me propuso que hiciéramos este evento y gratamente fue muy aceptado. Nos parece bueno (el evento) por muchas razones (…): lo importante de leer, lo hermoso de dar, lo emocionante de soltar y la incertidumbre de no saber y confiar; fomentar la solidaridad y el espíritu del compartir social y culturalmente, abrir el corazón y atravesar fronteras.
Wazo hili si letu, limekuwepo kwa muda sasa na sijui nani hasa alilianzisha. Rafiki yangu, Rodri, ambaye pia ni mwandaaji wa tukio hili alifikiri kutoa vitabu hivi vingi na kupendekeza kwangu kuwa tufanye tukio hili na kwa kweli limekubalika sana. (Tukio hili) linaonekana kuwa jema kwetu kwa sababu nyingi (…): Umuhimu wa kusoma, uzuri wa kutoa, furaha ya kuachia ulicho nacho na kutokuwa na uhakika wa kujua na kuamini; kuhamasisha ushirikiano na moyo wa kushirikiana kijamii na kiutamaduni, kufungua moyo wako na kuvuka mipaka.
Wakati huo huo, mwandaaji mwingine, Rodri Bristot, added:
En lo personal, lo que me impulsa a organizar este evento de Suelta Masiva, tiene que ver con una idea un poco romántica: creo que hay cosas en la vida que debieran ser gratis, como la educación y la lectura; los libros no debieran ser solo para quienes pueden pagarlos, si no que deberían ser más accesibles, que la gente los encuentre en los espacios públicos sin tener que resignar algo (dinero o trabajo) para adquirirlos.
Kibinafsi, kilichonihamasisha kuandaa tukio hili la kugawa vitabu, ni wazo ambalo lina mvuto: Ninaamini kuwa kuna vitu kwenye maisha ambavyo vyapaswa kuwa bure, kama elimu na kusoma: vitabu havipaswi kuwa kwa ajili ya wale wanaovilipia pekee, vyapaswa kupatikana zaidi, watu walipate kwenye maeneo ya umma bila kuvilipia (iwe fedha au kazi) ili kuvipata.
Asubuhi ya Jumapili, Aprili 6, González akiwana na kikundi cha vijana 50, wakubwa kwa wadogo, aligawa vitabu kwenye Bustani yaH y 21, iliyopo El Vedado, Havana. Watu walitafuta kwenye mabenchi ya bustani hiyo, kwenye mizunguko ya katikati ya bustani na kati kati ya mizizi ya miti, na hata kuwafuata watu waliokuwa wanakuja bustanini hapo ili kupata vitabu hivyo.
Mwandishi wa Cuba Dazra Novak alielezea uzoefu huo [es] kupitia blogu yake [es]:
He soltado cuatro libros hoy -con el mes, el año y la ciudad anotados en la primera página-, espero que los beneficiados la pasen tan bien como yo al leer dos de esos títulos, tan bien como la pasé al escribir los otros dos. No sé por qué sospecho que en algún momento volverán a mí para que yo pueda enrumbarlos de nuevo. Ahora que lo pienso, hoy –mañana, siempre- todos deberían hacer lo mismo.
Niligawa vitabu vinne leo -vikiwa vimeandikwa mwezi, mwaka na mji kwenye ukurasa wa kwanza -, ninaamini kuwa watakaovipokea watavifurahia kama nilivyovifurahia mimi wakati navisoma viwili kati ya hivyo, na kama nilivyoviandika viwili kati ya hivyo. Sijui ni kwa nini nina mashaka kuwa kwa wakati fulani vinaweza kunirudia ili na mimi nivitoe kwa mara nyingine. Sasa ninapofikiri tukio hilo, leo -kesho, na siku zote -kila mmoja afanye hivyo hivyo.
*Picha kuu imepigwa na Fernando Medina.
1 maoni
Mimi ;maoni yangu ni kwamba..je,naweza kupata je kitabu hicho hali yakuwa nipi burundi, bujumbura city?…na niliwaandikia ila hamkunipa jibu khusu maoni yangu…nawashukuruni saana…namba yangu ya simu ni +25776640916.