China: Yatishiwa na Zuio la Mtandao Lililofanywa na Marekani

Siku chache baada ya hotuba ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Hillary Clinton juu ya uhuru wa mtandaoni, mtandao huria wa alama za tarakilishi wa SourceForge.net umefungia upatikanaji wa anuani mahsusi za kompyuta za nchini Cuba, Iran, Korea Kaskazini, Sudani na Syria.

SourceForge wanahalalisha hatua hiyo kwa kusema wanafuata tu sheria ya Kimarekani. Ambayo ni kama hoja inayotolewa na wasemaji wa serikali ya Uchina wanapoulizwa juu ya zuio la mtandao la nchi hiyo.

SourceForge imewahi kufungiwa na China kabla. Kwa kusika neno la ukuta huu mkubwa wa moto wa Marekani uliowaacha wataalamu wa alama hizo wa Kichina wakishangaa ikiwa wanaweza kuanza kufungiwa kutoka kwenye nchi nyingine na kile kinachoweza kufanywa kuhusu suala hilo.

Picha kutoka Blogu ya Moonlight ya william Lone

Picha kutoka Blogu ya Moonlight ya william Lone

Kwenye CNBeta katika siku ya habari hiyo, ugmbbc aliandika:

在今天,开源精神遭到了践踏,SourceForge会因为他们被要求屏蔽流氓国家而去美国国会抗议么?
这是个棘手的问题,难道仅仅因为这几个国家的极少数的一部分人的极端行为,就要整个国家遭到惩罚么?开源软件为这些受到压迫和发展中的国家提供了重要的基础设施。希望美国政府能够看到对这些国家基础设施和羽翼未丰的产业带来的打击。

Utamaduni wa Chanzo huria umeanguka leo. Tukiwa tumetakiwa kuyafungia mataifa haya, je, SourceForge itaandama kwenda kwenye Baraza la Wawakilishi la Marekani?

Ni hali yenye mtego, lakini je, nchi nzima inapaswa kuadhibiwa kwa sababu tu ya vitendo vilivyozidi mipaka ya watu wachache sana kwenye nchi hizi? Nyenzo ya chanzo huria inatoa muundombinu muhimu kwa mataifa haya yaliyokandamizwa na yanayoendelea. Ninatumaini serikali ya Marekani inaweza kuona hili ni pigo kubwa kiasi gani kwa miundombinu na viwanda vichanga katika nchi hizi.

Kule kwenye jamii ya wataalamu wa tarakilishi ya Solidot, huru kama kwenye uhuru anaona kwamba huu ni mkakati unaofanywa na SourceForge kufuatia masharti ya awali kwa watumiaji ndani ya nchi hizi tano, kuwaruhusu kuperuzi wavuti na kupakua alama za siri za mtandao, wakati huohuo masharti hayo yanawazuia kuchangia alama zozote. Maoni kule ni pamoja na:

Alpha.Roc:
SourceForge 还是要遵守美国法律的呀?

SourceForge yabidi wafanye kazi kwa mujibu wa sheria za Marekani!

alvan:
SourceForge为什么一定要遵从自由软件精神?软件只是代码,所以可以自由中立;但是网站是离不开服务器的,你的服务器放在哪个国家,就要遵从这个国家的法律——这个天经地义呀。

Kwa nini SourceForge wasibaki huru katika utamaduni wa vyanzo huria? Vyenzokazi ni alama tu, ambayo huifanya iwe huru na isiyo na upande; lakini wavuti haiwezi kukwepa watunzanyenzo(servers) ambao ndio wanaowasaidia, na ni lazima ukubali kuheshimu sheria za nchi yoyote ile aliko mtunzanyenzo wako, hivyo ndivyo ilivyo.

pynets:
这是人家的自由

Huu ni uhuru wao

erlv katika blogu yake ya kiteknolojia LingCC anatazama maana ya siasa zinazoingilia vuguvugu la chanzo huria:

每个喜欢互联网技术,拥护开源的人都不想让开源沦为政治工具,但这是一个政治主导的世界,你得听政府的,政府是老大,你在政府的地盘上混,管你什么道义,什么自由,什么开源,统统只是工具。
我不是在鼓吹网络长城多么利国利民,但我们确实需要一种手段,让我们与国外能自由交流的同时,能摆脱对他们的依赖。正如现在国内,开源爱好者们都很乐于将自己的代码贡献出来,给开源社区,但当它变成政治工具的时候,我们如何取得该属于我们的权利?
SourceForge.net好像在国内还没有官方的镜像服务器. 如果我们的官老爷们真的为我国的信息产业处心积虑,鞠躬尽瘁的话,倒不如拿支持防火长城项目1%的钱,作为政府鼎力支持,在国内建几个开源镜像服务器,这 样,至少我们还能有所有的源码,至少我们有了独立自主!

Hakuna shabiki wa teknolojia ama muunga mkono wa chanzo huria anayetaka kuona chanzo huria ikigeuka kuwa chombo cha kisiasa, lakini sasa hii ni dunia inayoongozwa na siasa; unaweza kusema vyote unavyotaka kusema kuhusu kanuni, uhuru ama chanzo huria, lakini unapokuwa kwenye uwanja wa serikali, serikali ndiyo yenye msemo, bora usikie: zile ni nyenzo tu.

Sisemi kwamba GFW ni nzuri kwa nchi au watu, isipokuwa kwamba tunahitaji kuchukua hatua za kuhakikiasha kuwa kwa wakati huo huo tunaweza kuwasiliana na watu wa ughaibuni, tunaweza kuacha kuwategemea. Hapa sasa katika sehemu ya bara, kwa mfano, mashabiki wote wa chanzo huria wako radhi kuchangia alama zao kwa jamii yote ya chanzo huria. Lakini hiyo inapokuwa nyenzo ya kisiasa, tunawezaje kupata haki zinazotuhusu?

Sidhani kama SourceForge wana mtunzanyenzo nchini China. Kama wale wanaohusika walitaka kufanya mpango kwa niaba ya biashara ya habari ya nchi hiyo na walitaka kufanya chochote kinachowezekana, isingewaumiza kuchukua asilimia 1 ya fedha wanazotumia kwenye GFW, kama msaada wa dhati wa serikali, na kutengeneza kitunzanyenzo ndani ya nchi. Angalau kwa namna hii, tunaweza kuwa na alama yetu wenyewe. Angalau bado tuna uhuru wetu!

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.