Caribbean: Kwaheri, Nelson Mandela

Si kwamba Caribbean – au jumuiya ya kimataifa – raia wa mtandaoni hawakujiandaa kusikia habari za za kifo cha Nelson Mandela . Rais huyo wa zamani wa Afrika Kusini na mwanaharakati aliyepambana na ubaguzi wa rangi, na baada ya yote, alikuwa na umri wa miaka 95 na afya ikazorota, baada ya kulazwa hospitalini mara kadhaa mwaka huu akisumbumbuliwa na maradhi ya kupumua. Hata hivyo, tangazo la kifo chake lilipokuja mwishoni mwa juma la jana, lilileta pigo kubwa. Wanablogu wa sehemu mbalimbali na watumiaji wa vyombo vya habari vya kijamii walitoa mawazo yao kuhusu kufariki kwa moja wa magwiji wa amani duniani aliyedumu zaidi duniani.

Wananablogu, kwa sehemu kubwa, walionekana kukosa maneno, na walionekana kupendelea – angalau kwa sasa – kusambaza taarifa za habari au kunukuu za Hayati Mandela. Chombo cha habari cha “PropagandaGuyana” kilichapisha sehemu ya hotuba ya Rais Jacob Zuma kwa raia wa Afrika Kusini, pamoja na wasifu mfupi wa Mandela, wakati Bajan Mwandishi wa Bajan aliweka posti ya heshima kwa marehemu rais na Katibu Mkuu wa zamani wa Jumuiya ya Madola Sir Shridath Ramphal.

Wengi wa raia wa mtandaoni wa Caribbean waliamua kutumiana maoni yao kwenye mtandao wa Facebook na Twita. Raynier Maharaj, raia wa Trinidad anayeishi nje na pia mwandishi wa habari, alitoa maoni kwenye Facebook:

Sawa, kama inaonekana mimi nafikiri sana juu ya kufariki kwa Mandela, ni kwa sababu tukio hili lina maana kubwa kwangu. Kwa watu wote ‘maarufu’ mimi kuwahi kukutana nao katika maisha yangu – na hii ni pamoja na Malkia na Dalai Lama – kukutana na Nelson Mandela ilikuwa ni moja ya mafanikio makubwa katika maisha yangu. Alikuwa mfano wa heshima na neema.

Mwandishi mwingine wa Trinidad, Vernon O'Reilly Ramesar, alisema:

Ushahidi wa umuhimu wake ni kwamba hata vyombo vya habari Marekani vilikatiza programu na kutangaza kufariki kwa Nelson Mandela.

Mtumiaji Facebook Skye Hernandez alifadhaishwa kusikia kifo cha Mandela:

Nasikitika ajabu kwa habari ya kufariki kwa Madiba. Yeye hatimaye amekwenda kupumzika na hakika ni jambo jema. Lakini hadithi yake na Afrika Kusini imekuwa hamasa, wakati mwingine ya kuudhi, lakini daima yenye kuvutia. Yeye amekuwa na sisi siku zote kwa maisha yetu yote. Safiri vizuri, Nelson Mandela.

Franz Gillezeau alipendekeza kuwa watu:

Kumuomboleza sawa, lakini tukumbuke kumsherehekea gwiji huyu.

Mtandao wa Facebook pia ulijaa albamu za picha mpya zilizowekwa kuonyesha ziara za Mandela maeneo mbalimbalih- hii moja, kwa niaba ya Huduma ya Habari ya Jamaica, ya ziara yake ya kisiwa hicho katika miaka ya 1990, na hii nyingine, kwa hisani ya Amber Media Productions, na nyingine ya ziara yake ya mwaka 2004 nchini Trinidad na Tobago.

Kwenye mtandao wa flickr, Georgia Popplewell aliposti picha ya Mandela, akibainisha:

Mimi nahofia itachukuwa muda mrefu kabla ya kuona kiongozi mwingine wa aina yake tena. Buriani, mpendwa Madiba. #Mandela

Nelson Mandela; image by caribbeanfreephoto

Nelson Mandela; picha kwa hisani ya caribbeanfreephoto

Si kila mtu aliyekubaliana na tathmini hii, hata hivyo. katika blogu ya ‘babablogu’, drillanwr aliandika:

Historia itakumbuka maisha yake, kwa uhakika.
Wakati mimi nafahamu na kuheshimu mapambano ya Nelson Mandela na kule kuwa mfungwa wa kisiasa ndani ya nchi yake mwenyewe kwa sehemu kubwa ya maisha yake, lakini sifahamu itikadi zake za kisiasa baada ya kifungo na urafiki aliokuwa nao na baadhi ya viongozi wabovu wa dunia.

Katika posti ya majibu katika blogu hiyo, Carlos Eire alipendekeza kuwa:

Utakatifu wa Mandela haiambatani na sifa zote za ulimwengu, hasa kati ya raia wa Cuba. Wakati yeye alijitolea kimaadili na kwa sababu za haki – kumaliza ubaguzi dhidi ya Waafrika weusi nchini Afrika Kusini – Mandela hakupinga kutumia vurugu kama njia ya sababu zake. Mbaya zaidi, alitoa pongezi kwa Fidel Castro pamoja na vita yake kwa ubaguzi wa rangi, lakini kamwe hakuacha kuimba sifa za Fidel.

Kwa upande mwingine, blogu ya Capitol Hill Cubans walitoa mtazamo huu:

Nelson Mandela hayuko tena kimwili kati yetu, lakini urithi wake wa kujitolea, uvumilivu na uhuru utashamiri milele.

Licha ya kutetea vurugu wakati wa siku za kwanza za harakati zake, safari ya maisha ya Mandela inaonyesha nguvu ya mageuzi ya amani, pasipo uvunjaji wa sheria.

Kufariki kwake ni ukumbusho wa kujitolea kwa wafungwa wa kihistoria wa kisiasa duniani, kama vile Cuba Eusebio Penalver Mazorra, mfungwa wa kisiasa aliyefungwa kwa muda mrefu mwenye asili ya Afrika katika historia ya kisiasa, baada ya kutumikia kifungo chake kwa miaka 28. Cha kusikitisha, Penalver alifariki mwaka wa 2006, bila kuushuhudia uhuru wa nchi yake aliyoipenda.

Pamoja na kiongozi wa zamani wa Czech Vaclav Havel, Mandela ni mwakilishi wa mwisho wa mfungwa aliyefunguliwa kuchaguliwa kuwa kiongozi wa kisiasa. Kutoka Cuba hadi Korea ya Kaskazini, maisha yake ya ajabu yanatoa matumaini na matarajio ya demokrasia ya wapinzani, wafungwa wa kisiasa na wanaharakati duniani kote.

Pumzika kwa amani na uhuru.

Watumiaji Twita – duniani kote – wamekuwa wakitumia alama habari #mandela #death kutoa rambirambi zao. Jumuiya ya blogu Caribbean bila shaka ina mengi ya kusema kuhusu Nelson Mandela na urithi wake pamoja hali halisi ya kifo chake kukubalika; timu ya GV Caribbean itatoa habari ipasavyo katika kipindi hiki.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.