Habari kuhusu Dini kutoka Februari, 2013
Wakati Papa Anajiuzulu, Warusi Wajiuzulu kwa Putin
Pasipokutaka kujua matokeo ya kujiuzulu kwa Papa Benedict na athari yake kwa imani ya Kikatoliki au tafsiri ya hatua hiyo kufuatia kashfa ya udhalilishaji iliyowakabili kwa watawa, RuNet walioweka habari hiyo kwenye safu za vichekesho.
PICHA: Maandamano ya Pamoja ya Watu wa Shia Nchini kote Pakistan Yamalizika Kwa Amani.
Baada ya milipuko ya mabomu huko Quetta kuua zaidi ya watu 100, maanadamano ya watu wa jamii ya Hazara ya Shia yalisambaa kama moto katika maeneo mbalimbali ya Pakistani. Watu kutoka katika makundi makuu ya dini na makabila mbalimbali waliungana kwa pamoja na watu wa Hazara wakiimba kwa kurudiarudia#Sisi sote ni watu wa Hazara. Maandamano ya kuishinikiza serikali kusikiliza madai yao yalianzishwa katika zaidi ya majiji 100 na miji.