· Julai, 2013

Habari kuhusu Dini kutoka Julai, 2013

Hali ya Uislamu Katika Asia ya Kusini

  27 Julai 2013

Murray Hunter wa Chuo Kikuu cha Malaysia Perlis anajadili hali ya jamii ya Kiislamu katika Asia ya Kusini pamoja na masuala yanayohusiana na kukua kwa Uislamu katika eneo hilo. Umaskini, kujua kusoma na...

Al Jazeera Yatuhumiwa Kutangaza “Habari za Upendeleo”

Al Jazeera iko kwenye wakati mgumu nchini Misri kwa kile kinachoelezwa na wengi kuwa ni "upendeleo" wake katika kutangaza habari zake wakati na baada ya kuondolewa madarakani kwa rais wa zamani wa Misri Mohamed Morsi mnamo Julai 4. Kituo hicho cha televisheni kilichopo nchini Qatar kinatuhumiwa kuegemea upande wa wafuasi wa Muslim Brotherhood na kimegeuka kuwa mdomo wa kikundi hicho.

Mama na Watoto Wake Wauawa kwa Kucheza kwenye Mvua

  6 Julai 2013

Mama na watoto wake wawili wa kike waliuawa kwa kufyatuliwa risasi mara baada ya watu watano waliokuwa wamefunika nyuso zao kuvamia nyumba alimokuwa akiishi mama huyu na watoto wake katika mji mdogo wa Chilas nchini Pakistan, tukio linalosadikiwa kuwa ni la mauaji ya kulinda heshima. Video iliyorekodiwa kwa simu inayowaonesha wasichana hao wakicheza kwenye mvua imekuwa ikisambaa kiholela na ambayo imeonekana kama ni kashfa na hivyo kuharibu heshima ya familia.

Misri: Wasalafi Washambulia Makazi ya Washia, Wanne Wauawa

Watu wanne nchini Misri ambao ni wafuasi wa imani ya Shia wameuawa leo nchini Misri mara baada ya nyumba waliyokuwa wanakutania kushambuliwa na Waislam wenye msimamo mkali, shambulio hili linafuatia wiki mbili za uchochezi dhidi ya waumini wa Shia. Kwa mujibu wa taarifa za awali, nyumba ambayo waumini hao wa Shia waliyoitumia kukutania, iliyopo huko Giza, Cairo, ilishambuliwa na kuchomwa moto. Kwa mujibu wa taarifa za habari za Al Badil, shuhuda mmoja alikaririwa akisema kuwa mmoja wa watu waliouawa alichinjwa na wengine watatu walijeruhiwa vibaya vichwani mwao. Tukio hili la kutisha lilizua ghadhabu kubwa mtandaoni.