Habari kuhusu Dini kutoka Novemba, 2009
Marekani: Mauaji ya Fort Hood Yasababisha Kumulikwa kwa Waislamu Walio Jeshini
Shambulizi la upigaji risasi la kushtukiza lililofanywa na mwanajeshi wa Jeshi la Marekani, Meja Nidal Malik Hassan, na kusababisha vifo vya watu 13 na kujeruhi wengine 31 katika kambi ya kijeshi ya Fort Hood, jimbo la Texas, kwa mara nyingine limesababisha Waislamu nchini Marekani kumulikwa - hasa wale wanolitumikia jeshi.
Vijana wa Kiyahudi na Kipalestina Watumia Video Kuuelewa Mgogoro
Mashirika mawili tofauti nchini Israel na katika Majimbo ya Palestina yanatumia zana za video ili kuwasaidia vijana wa Kiarabu na Kiyahudi kuuelewa mgogoro na kujenga daraja kati yao.
Misri: Mwanablogu wa Kiume Aagizia Bikra ya Bandia
Mengi yalisemwa na kuandikwa juu ya zana ya kutengeneza bikra ya bandia - mpaka mwanablogu Mmisri wa kiume Mohamed Al Rahhal akanunua moja. Marwa Rakha anatuletea habari hiyo.
Georgia: Aibu Katika Kanisa la Orthodox
Katika nchi inayofuata dini zaidi kwenye maeneo ya kusini mwa Caucasus ambako mkuu wa Kanisa la Orthodox (madhehebu ya Kanisa la zamani au kihafidhina) anaweza kuhamasisha ongezeko la watoto, kukosoa watumishi wa kanisa bado ni mwiko. Kuwatania, hata hivyo, ni jambo baya zaidi na lililojaa hatari.