Habari kuhusu Dini kutoka Machi, 2010
Moroko: Wafanyakazi wa Shirika la Misaada La Kikristu Wafukuzwa
Wiki iliyopita, wafanyakazi 20 wa Kijiji cha Matumaini, makazi madogo ya yatima katika mji mdogo wa Moroko vijijini, waliondolewa (walifukuzwa) nchini bila onyo, kwa madai ya kuhubiri dini.
Naijeria: Ghasia Zalipuka Huko Jos Kwa Mara Nyingine
Huko Jos, machafuko yanaelekea kujitokeza katika mizunguko inayozidi kuwa midogo: machafuko mabaya yaliukumba mji huo mwaka 1994, 2001, 2008, na – hata miezi miwili iliyopita – mnamo mwezi Januari 2010. Mgogoro wa sasa unasemekana kuwa ulianza katika tukio la kisasi kilichotokana na uharibifu uliotokea mwezi Januari, na, kama ilivyokuwa kwenye machafuko yaliyopita, mapambano ya sasa huko Jos yamekuwa yakipiginwa katika misingi ya kidini.