Mamlaka za Tanzania Zamshikilia na Kumfukuza Nchini Kiongozi wa Haki za Binadamu wa Uganda

Dr. Wairagala Wakabi [Picha na CIPESA na imetumiwa kwa ruhusa]

Wairagala Wakabi ni wakili kutoka Uganda anayeongoza shirika linalotetea haki za kidijitali alishikiliwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam Tanzania tarehe 25 Aprili.

Wakabi alialikwa katika siku ya kilele cha mkutano wa mwaka wa watetezi wa haki za Binadamu Tanzania ambao mwenyeji wake ni muungano wa walinda haki za Binadamu Tanzania (THRDC). Wakabi ni mtendaji mkuu wa muungano wa sera ya TEHEMA kimataifa Mashariki na kusini mwa mwafrika (CIPESA), moja ya shirika linalojihusisha na sera ya mtandao na uhuru wa kutoa maoni mtandaoni katika Afrika.

Wakabi alifukuzwa na kupelekwa Uganda baada ya masaa kadhaa ya mahojiano ambapo alinyimwa kuwasiliana na mwanasheria.

Wanasheria kutoka muungano wa watetezi wa haki za Binadamu Tanzania walijaribu kumtetea lakini waliambiwa tu kwamba Wakabi anarudishwa Uganda kwa sababu ya “maslahi ya taifa”:

Baada ya masaa ya mahojiano, Dkt. Wakabi amerudishwa Uganda Jioni hii. Hata hivyo, wanasheria walishindwa kujua chanzo cha kuzuiliwa na kufukuzwa. Waliaarifu kuwa mamlaka zilikataa asiingie nchini kwa sababu ya “maslahi ya taifa”

Ingawa tatizo liliisha baada ya masaa machache lakini lilisababisha fadhaa na mshangao mkubwa kwa wanasheria wa haki za binadamu ambao wameonesha wasiwasi juu ya namna Tanzania inavyoshughulikia wanaharakati na waandishi wa habari. Novemba mwaka jana Angela Quintal na Muthoki Mumo wote wakiwa wajumbe wa Kamati ya kutetea waandishi habari walishikiliwa na pasipoti zao kwa masaa kadhaa Dar es Salaam, Tanzania.

Je, Tanzania ina mpango wa makusudi wa kunyamanzisha watetezi wa haki za binadamu kwa kuwanyanyasa ili kuwazuia kuja nchini? Mwishoni mwa mwaka jana alikuwa sio Dkt Wakabi? Hii haiwezi kutunyamanzisha!

Shirika la haki za binadamu la Human Rights Watch lilieleza kuwa Tanzania chini ya uongozi wa Rais John Magufuli limeshuhudia “kushuka kwa hali ya juu katika uhuru wa kutoa maoni, kukusanyika na kukutana.”

Mwaka 2015, Jamhuri ya Tanzania ilitangaza rasmi sheria ya makosa mtandaoni . Ndani ya mwaka ambao sheria hiyo ilipitishwa watanzania 14 walikamatwa na kushitakiwa kwa sheria hiyo kwa kumtukana Rais kupitia mitandao ya kijamii. Mwezi Machi 2018 tuliona kupitishwa kwa Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (Maudhui ya habari za mtandaoni), na kuwalazimisha mabloga kujisajili na kulipa dola 900 za Marekani kwa mwaka ili kutuma habari mtandaoni. Hii ilisababisha blogu nyingi za kujitegemea kufungwa .
Kuzuia vyombo vya habari binafsi kupitia vikwazo mbalimbali dhidi ya vyombo vya habari na vitisho vya kisheria dhidi ya waandishi wa habari imejenga mazingira ya vitisho, udhibiti binafsi na woga wa kueleza habari mbalimbali kuhusu viongozi wa nchi.

Kushikiliwa na baadaye kurudishwa Uganda kwa Wakabi kunaonekana kuwa mwendelezo wa serikali ya Tanzania kushambulia uhuru wa kutoa maoni na hasa yanayokinzana na serikali.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.