Waandishi wa habari wa Urusi wauawa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati

Orkhan Dzhemal mwenye miaka 51 ambaye alikuwa mwandishi wa habari mkongwe wa Urusi aliuwa tarehe 31 Julai, 2018 katika Jamhuri ya Afrika ya kati// Picha ya YouTube kutoka Moscow,

Waandishi wa habari watatu waliuwa usiku wa tarehe 30 Julai katika Jamhuri ya Afrika ya kati kwenye kituo cha ukaguzi nje kidogo ya mji mkuu wa nchi hiyo wa Bangui.

Mwandishi wa habari mkongwe Orkhan Dzhemal, mshindi wa tuzo ya mtengeneza filamu Aleksandr Rastorguev na mpiga picha Kirill Radchenko walipigwa risasi na kuuawa walipokuwa wanakaribia kuingia mjini na wauaji wasiojulikana waliokuwa wamejificha katika vichaka kando kando ya barabara kuu inayoingia mji mkuu Bangui.

Shambulio hilo limetokea wakati kuna mgogoro unaoendelea kati ya serikali na vikundi mbambali vya waasi.
Vifo vyao vilithibitishwa na kituo cha kudhibiti uchunguzi(TsUR) kinachotoa taarifa za uchunguzi kinachodhaminiwa na Mikhail Khodorkovsky ambaye ni mfanyabiashara wa zamani wa mafuta anayeishi uhamishoni hoko London.

Kutokana na gazeti la Moscow Times, Urusi imetoa askari na mafunzo ya kijeshi kusaidia majeshi ya usalama ya serikali.

Kutokana na taarifa ya kituo cha kudhibiti uchunguzi, waandishi wa habari hao walikuwa wanafuatilia taarifa ya kikundi cha mamluki wa jeshi la Urusi ambao wapo katika nchi ya Afrika.

Kundi hilo la jeshi halijawahi kuthibitishwa rasmi kuwepo ingawa uchunguzi mwingi wa kijeshi zinataja kundi linalojiita ‘Wagner Group’ kuwa lipo katika maeneo ya hatari ya Syria na mashariki ya Ukraine. Ingawa mfanyabiashara mashuri Evgeny Prigozhin amabye ana mahusiano makubwa na Vladimir Putin anahusishwa na kulidhamini kikundi hicho cha ‘Wagner Group’ ingawa yeye amekanusha madai hayo mara nyingi.
Kutokana na madai hayo Evgeny Prigozhin aliwekewa vikwazo na Marekani vya kutoshiriki katika uchaguzi wa Rais wa mwaka 2016— hata hivyo hakukubali.

Dzhemal, Rastorguev and Radchenko walikuwa ni wanahabari mahiri walioheshimika sana na waliokuwa wanatambuliwa katika taaluma hiyo. Orkhan Dzhemal alikuwa mashuhuri kwa kuripoti taarifa za vita, na kazi yake ilianza mwanzoni mwa miaka ya uhuru wa habari Urusi. Alexander Rastorguev alipongezwa sana kutokana na kuandika tahiri mwaka 2013 ya kuongezeka kwa upinzani dhidi ya Putin. Neno Kirill Radchenko lilitumika kama mtangazaji wa runinga katika kanda za vita kama za Siria.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.