Shujaat Bukhari, mhariri wa gazeti maarufu la kila siku huko Kashmiri la Rising Kashmir, alipigwa risasi na kufa huko Srinagar, mji wa majira ya joto wa Jammu na Kashmiri na kutuma mawimbi ya mshituko katika ukanda wote.
Gari lake lilizingirwa na watu waliohisiwa kuwa wanamgambo waliompiga risasi yeye na walinzi wake. Walinzi wake wawili walifariki baadaye wakiwa hospitalini kwa sababu ya majeraha.
Wenzake na Bukhari walisema kuwa ndi alikuwa ametka tu nje ya ofisi yake baada ya kumaliza shughuli zake za kila siki na alikiwa anaelekea kufuturu shambulio hilo lilipotokea.
(Onyo: Picha hapo chini kutoka tweeter.)
Mwanahabari Shujaat Bukhari alishambuliwa katibu na Koloni la Vyomho vya habari huko Srinagar.
Mlinzi wake pia amejeruhiwa vibaya. pic.twitter.com/g6AsFuudyr— Jyoti NS Pachnanda (@PachnandaJyoti) June 14, 2018
Baada ya shambulio dhidi ya Shujaat Bukhari ni ishara iliyowazi kuwa hakuna mtu ambaye yu salama ndani ya Kashmir. Tukio limetukia ndani ya moyo wa mji Lal Chowk. Shujaat Bukhari alikuwa akitoka ofisini kwake aliposhambuliwa na magaidi. Yeyote aliyefanya hivi lazima atakuwa mtu wake wa karibu.
— Ibne Sina (@Ibne_Sena) June 14, 2018
Hakuna siku moja inayopita bila damu kumwagika ndani ya #Kashmir. Napitia kazi za Shujaat Bukhari ili kutambua ni nani anayeweza kuwa aliyataka maisha yake. Kila kitu hakiko sawa. Mtu yeyote anaweza kuuawa saa yoyote na mahali popote.
— Burhan Gilani (@Katar_Koshur) June 14, 2018
Bukhari alikuwa kati ya watu wachache wenye ujasiri ndani ya Kashmiri ambao walisimama kati ya India na Pakistani kusuluhisha mgogoro wa Kashmiri.
Soma zaidi: Watu wa Kashmiri dhidi ya watu wa taifa la India
Maandamano ya kudai uhuru (yaliyoitwa “azadi”) na utawala binafsi ndani ya Bonde la Kasmiri yamekuwa hai tangu mwaka 1989, na tangu hapo Jammu na Kashmiri imekuwa chini ya Jeshi la India kwa kifungu cha amri ya Jeshi maalumu lenye silaha na Kifungu cha sheria cha Usalama wa Raia ukiwapa uwanja mpana wa mamlaka. Serikali ya India imetamka rasmi kwamba inaamini kuwa Jammu na Kashmiri sehemu muhimu ya India.
Bukhari alifanya kazi na kampuni kubwa za uchapishaji za kitaifa na zile za kimataifa na aliandika makala nyingi zilizogonga vichwa, hakuwai kuona aibu kuchukua msimamo ambao hakuungwa mkono na wengi. Alikuwa mwandishi maalum wa gazeti la Hindu kuanzia mwaka 1997 hadi 2002 na aliendelea kuandikia jarida la Mstari wa Mbele. (Frontline).
Klabu ya Wanahabari ya India imeelezea mshtuko wake na kusikitishwa na tukio hilo lililotokea ndani ya Bonde la Kashmiri.
Chama cha Wahariri wa India kilitoa taatifa yake huko twita:
Chama cha Wahariri cha India kwa pamoja tunalaani mauaji ya Mhariri wa Rising Kashmiri ndugu Shujaat Bukhari. Hili ni shambulio la kikatili dhidi ya uhuru wa habari na sauti ya demokrasia. Tutatoa taarifa nyingine ya kina hivi karibuni
— Editors Guild of India (@IndEditorsGuild) June 14, 2018
Salamu za rambirambi zinamiminika kupitia mitandao ya kijamii.
Siddharth Varadarajan, mhariri wa Wire news portal, alitwiti:
Mimi na Shujaat Bukhari tulifanya kazi pomoja kwenye gazeti la Hindu. Alikuwa mwandishi asiye na hofu na kama mhariri wa Rising Kashmiri alikuwa sauti yenye nguvu iliyopigania umoja wa vyombo vya habari, sauti ya kweli katika umakini na fikra. Hakuna maneno ya kutosha kuwalaani washenzi waliomuua.
— Siddharth (@svaradarajan) June 14, 2018
Marvi Sirmed, mjumbe wa baraza kuu la Kamisheni na Haki za Binadamu la Pakistani (HRCP) na mwandishi maalum wa Daily Times wa Pakistan, alitwiti:
Shujaat Bukhari alikuwa sauti yenye fikra ndani ya Kashmir. Mwandishi bora ambaye hakuukuwadia uovu. Aliifanya kazi yake kwa haki mpaka mwisho wa pumzi yake na amelipa gharama za kuwa muungwana. Kwa lengo la kutoa taarifa za uvunjwaji wa haki za binadamu unaofanywa na majeshi katili ya India huko Kashmir.
— Marvi Sirmed मार्वि ماروی (@marvisirmed) June 14, 2018
Hii haikuwa mara ya kwanza Bukhari kulengwa.
Hapo Julai 8, 1996, kikundi cha wanamgambo waliwateka waandishi wa habari 19 katika wilaya ya Anantnag na kuwashikilia kwa masaa saba. Bukhari alikuwa mmoja wao.
Pia alipewa ulinzi na polisi baada ya shambulio dhidi yake hapo mwaka 2000..
Mwanafunzi mwanasiasa Shehla Rashid alitwiti:
Hata katika eneo lisilo na maana kama Kashmiri mauaji ya Shujaat Bukhari hayaleti maana. Kila mtu hapa anauliza swali moja tu kuwa: “Kwanini mtu yeyote angetaka afe?”
Isipokuwa serikali ambayo ingekuwa imefikia suluhisho.
Ninatoa wito wa @MehboobaMufti kuhakikisha uchunguzi wa kina unafanyika.
— Shehla Rashid (@Shehla_Rashid) June 14, 2018
Waziri wa zamani wa Jammu na Kashmiri iliyosimamiwa na India, Omar Abdullah, alitwiti:
Lazima mambo yaendelee. Kama ambavyo Shujaat angependa yawe. Hili ni jambo @RisingKashmir la leo. Kitendo cha Wafanyakazi wenza wa Shujaat kuweza kuchapisha na kulitoa gazeti hilo wakati huu wa maombolezo haya makubwa ni ushuhuda wa ukomavu wa taaluma yao na salamu za rambi rambi za kumfaa bosi wao aliyefariki. pic.twitter.com/ADP70D4F1q
— Omar Abdullah (@OmarAbdullah) June 14, 2018
Kulingana na waandishi wa habari wasio na mipaka, Shujaat Bukhari alisalimika jaribio la kumuua lililofanywa na watu wenye silaha hapo Juni 2006. Shujaat Bukhari aliwaambia Waandishi wa Habari wasio na mipaka kuwa, ” Ni vigumu kutambua ni nani ni maadui zetu na ni nani ni marafiki zetu.”
Pamoja na hili, bunduki haziwezi kuinyamazisha kalamu yake.