Taarifa ya raia mtandaoni ya Advox inatoa picha ya haraka kimataifa juu ya changamoto, ushindi na mienendo inayoibuka katika haki za kimtandao duniani.
Mahakam kuu ya Gambia imezuia marekebisho yaliyofanywa ya sheria ya habari na mawasiliano ya mwaka 2013, na kutamka kuwa yanapingana na Katiba. Pia, mahakama imetetea vifungu muhimu vya sheria ya uhaini wa nchi. Vifungu hivyo vilikuwa vikitumika kama zana za kukandamiza vyombo vya habari.
Hukumu hiyo ni matokeo ya shauri lililosajiliwa mahakamani mwaka 2015 na umoja wa waandishi wa habari wa Gambia ukihoji kikatiba kuhusu uhaini, kuasi, uhalifu wa kukashfu. Hivi karibuni mahakama ya jumuia ya uchumi ya nchi za Africa Magharibi ilitoa hukumu juu ya sheria kama hiyo , kwa waandishi wa habari wanne wa Kigambia walioko uhamishoni ambao walikutwa na hatia ya kikatiba.
Lakini Mahama kuu ya Gambia ilifikiri tofauti. Wakati hukumu iliyotolewa inakumbatia sheria ya uhaini ambayo inaweza kutumika kuadhibu taarifa muhimu au uchunguzi wa wanahabari unaomuhusu Rais,inaondoa marekebisho ya sheria ya habari na mawasiliano ya mwaka 2013 ambayo yalifanya kashfa mtandaoni na kusambazwa kwa “habari za uongo” mtandaoni kuwa jinai. Wakiukaji wa sheria hiyo walilazimika kulipa faini kubwa na kufungwa mihula ya vifungo hadi miaka 15 gerezani.
Kupitia mtandao wa Tweeter, Sanna Camara, mwandishi wa habari wa gambia anaeleza sheria ya habari na mawasiliano ni moja ya “sheria mbaya” ya mtandao katika Afrika. Camara alikabiliwa na vitisho vya kisheria kwa kuchapisha habari katika gazeti la Standard kuhusu utoroshaji wa binadamu nchini Gambia . Mwaka 2014 Camara alishtakiwa kwa kuchapisha “habari za uongo” na muda mfupi baada ya kushtakiwa alikimbia nchi.
Kamati ya kulinda wanandishi wa habari ya Angela Quintal ilieleza uamuzi huo ni “hatua moja mbele na mbili nyuma.”
“[Hukumu] inatuma ujumbe kuwa waandishi wa habari bado hawako huru kufanya kazi bila ya vitisho vya kushitakiwa kwa makosa ya jinai,” alisema.
Hukumu hiyo ni maamuzi makubwa ya kwanza ya mahakama ambayo yanaathiri uhuru wa kutoa maoni tangu mwaka 2017 ambacho kilikuwa kipindi cha mpito wa madaraka kutoka kwa mtawala wa muda mrefu Yahya Jammeh kwenda kwa Rais wa sasa Adam Barrow. Punde tu baada ya kuingia ofisini, Rais Barrow aliwaachia mamia ya wafungwa na kuanzisha uchunguzi mfululizo juu ya ukiukwaji wa haki za binadmu kipindi cha utawala wa Jammeh. Lakini wanaharakati na watumiaji wa mtandao wanaotoa mawazo yao katika mitandao ya umma na isiyo ya umma wameendelea kufanya hivyo kwa shinikizo.
Mwezi Februari 2018,mhadhiri wa Chuo Kikuu aliwekwa kizuizini kwa sababu ya maoni aliyoyatoa kupitia vyombo vya habari nchini. Wiki hii iliyopita, wanaharakati vijana walikamatwa baada ya kutoa wito wa tahadhari ya kitisho cha uharibifu wa mazingira ambacho kilisababishwa na Golden Lead kiwanda cha kusindika samaki kinachomilikiwa na Wachina kilichopo makazi ya pwani ya Gunjur.
Kwa sasa, mahakama ya Tanzania imezuia kodi ya kublogu
Mahakamu kuu ya Tanzania imezuia utekelezaji wa ”kodi ya kublogu” dola za kimarekani 900 iliyoamuriwa na Serikali kama sehemu ya kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (Maudhui Mtandaoni) ambayo inataka wanaoblogu kulipa faini au kuacha kublogu.
Makundi sita ya haki za binadamu nchini yaliomba mahakama kurudia na kurekebisha sheria kwa hoja kwamba waziri wa mawasiliano alitumia madaraka yake vibaya na kulikuwa na ukiukwaji wa haki ya kutoa maoni. Hata hivyo, hukumu ya mahakama kuu ni ushindi juu ya uhuru wa kuongea Tanzania kwa muda.
Mwandishi wa habari wa Hundrus alifuatiliwa baada ya kupokea vitisho vya kifo kupitia mtandao wa Facebook
Mauricio Ortega mwandishi wa habai wa Hindrus alipokea kitisho cha kifo kupitia ujumbe wa Facebook baada tu ya kuripoti mfululizo matukio ya wasafiri kuvamiwa kwa nguvu katika usafiri wa umma. Baadaye siku hiyo, alifuatwa na gari iliyokuwa haina namba rasmi za gari. Katika mahojiano na kamati ya uhuru wa kutoa maoni, alisema:
…las amenazas en contra de nosotros es lamentablemente hasta normal, estamos acostumbrados a que los que se sienten ofendidos nos insulten, amenacen y nos desacrediten y tristemente no hay confianza ni eficiencia en los entes encargados de administrar o impartir justicia, esto nos vuelve más vulnerables.
…kwa bahati mbaya vitisho juu yetu vimekuwa ni kawaida, tumezoea kutukanwa, kutishwa na kuaibishwa na wanaovunja sheria kazini kwetu. Na mbaya zaidi, kuna uaminifu au ufanisi mdogo sana kwa wanaotakiwa kusimamia haki, ambao hutuacha katika hali ya kudhurika.
Mitandao ya simu ni dhaifu wakati waandamanaji wa Urusi wakipinga kuapishwa kwa Rais Plutin
Kadri siku zinavyokaribia uzinduzi rasmi wa muhula wa nne wa Vladimir Putin kama Rais, waandamanaji wameongezeka nchi nzima ya Urusi , baadhi ya wanaharakati wameripoti kwamba ishara za mawasiliano katika simu zao zinakuwa dhaifu au hazipo kabisa. Baadhi wameeleza kuwa waendesha mitambo ya mawasiliano ya simu walipunguza makusudi kabisa ubora wa huduma au hata kufuta namba za simu zao kutokana na amri ya mamlaka. Mwanaharakati Denis Styazhkin alilipoti kwamba mwendesha mitambo ya mawasiliano ya simu anayeitwa Beeline alimwambia kuwa namba yake ya simu ilifutwa kutokana na amri ya polisi.
Wakaguzi wa China macho yao yapo kwenye Peppa Pig
Sehemu ya utamaduni wa mtandao wa China ni kuunganisha kipindi cha katuni katika televisheni. “Peppa Pig” na “Shehuiren”, ni isitilahi yenye maana ya umoja wa wachapishaji wa uharifu wa katuni, imetumbukia katika matope mazito kwa sababu ya nyama maarufu ya nguruwe. Baada ya kuongoza vyombo vya habari vya taifa watoa maoni walikosoa uandishi, jukwaa la video maarufu za kichina la Douyan kwa kuondoa video zaidi ya 30,000 ambazo zilikuwa na rangi nzuri ya pinki na ilifanya isitilahi ya “Peppa Pig” isipatikane kwenye tovuti yake na kudhani kuwa Peppa imepigwa marufuku.
Wabunge Misri walenga kufatilia wanaoendesha huduma usafiri wa haraka
Tarehe 7 Mei, Bunge la Misri ilipitisha sheria ambayo inawataka watoa huduma za usafiri wa haraka unaotumia mtandao kama Uber na UAE kuanzisha kituo cha kutunza taarifa kwa ajili ya kuchakata taarifa zote zinazohusiana na watumiaji wa Misri. Sheria ambao inasubiri idhini ya utendaji, inawajibisha makampuni haya kutoa taarifa za mtumiaji (zikijumuisha taarifa kuhusu eneo walipo madereva na wasafiri) kwenye mamlaka za usalama zinapohitajika. Makampuni hayo yalisimamishwa kwa muda mwezi Machi, 2018 baada ya kundi moja la wazawa wanaondesha teksi kuyashtaki kwa sababu ya leseni.
Kadi za kibayometriki zitakuwa ni lazima Ulaya?
Tume ya Ulaya imependekeza mikakati mipya ya kupambana na ugaidi ni kujumuisha kwa lazima taarifa za kibayometriki katika kadi za vitambulisho na nyaraka za makazi kwa wakazi wa Ulaya na familia zao. Mkakati huu unawahitaji wakazi wengi wa Ulaya kuchukuliwa alama za vidole ili vitambulisho vya kibayometriki viweze kukaguliwa kwenye vituo vya mpakani.
Mpiga kura mmoja alitumia Cambridge Analytica kukabidhi taarifa zake. Je vipi kuhusu tuliosalia?
Ofisi ya kamishina wa habari wa Uingereza imeipa Cambridge Analytica siku 30 kukabidhi taarifa zote na taarifa binafi walizonazo za mpiga kura wa Marekani, au kukabili mashitaka ya uhalifu. Mpiga kura, David Carroll, aligundua kuwa adai haki yake kupitia sheria za Uingereza kwa sababu Cambridge Analytica imefanya mchakato wa taarifa za wapiga kura wa Marekani katika Uingereza. Wiki hii, Cambridge Analytica ilitangaza kuwa imefilisika.
Azimio la siku ya uhuru wa habari ulimwenguni
Washiriki katika Mkutano wa kimataifa wa siku ya uhuru wa habari duniani iliyoandaliwa na UNESCO walitangaza Azimio la Accra wakiomba nchi wanachama wa UNESCO kuunda na kuimarisha mifumo ya sheria na sera ili kuhakikisha kuheshimiwa kwa uhuru wa kutoa maoni na faragha na kulinda usalama wa wanahabari na wafanyakazi wa vyombo vya habari.
Tafiti Mpya
- Chukia sheria za habari katika India – Kituo cha Utawala wa Mawasiliano, Chuo Kikuu cha Taifa cha Sheria cha Delhi
- Kwa hiyo hii ni demokrasia? Hali ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika 2017 – Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika
Jiunge na taarifa ya raia mtandaoni
Afef Abrougui, Ellery Roberts Biddle, Nwachukwu Egbunike, Mohamed ElGohary, Rohith Jyothish, Demba Kandeh, Leila Nachawati, na Sarah Myers West walichangia taarfa hii.