Wewe ni Mwanasiasa Mbovu Mexico? Unaweza Kurushiwa Nyanya Usoni

JitomatazoMx

Picha: Flickr / Alan Levine. CC 2.0

Mwanahaakati na mtumishi wa umma wa zamani nchini Mexico anaongoza kampeni isiyozoeleka ya kuwa kuchafua nyuso za wanasiasa kama namna ya kuonesha kutokuridhika na mienendo yao. Arne aus den Ruthen Haag anatangaza vuguvugu linaloitwa #JitomatazoMx, linalowahamasisha watu kwenye mitandao ya kijamii kukusanya nyanya — au jitomates kama zinavyofahamika kwenye mji wa Mexico City — ziwe silaha ya kuwarushia maafisa wa serikali wenye kashfa za ufisadi.

Vuguvugu hilo la nyanya lina nyanya lina akaunti yake ya Twita , yenye maelezo yanayofafanua malengo ya kampeni hiyo:

Cuando hay abusos de la clase política y no hay mecanismos legales de defensa, el jitomatazo es la vía para expresar nuestro repudio.

Kunapokuwa na ufisadi miongoni mwa tabaka la wanasiasa na hakuna namna tunaweza kupambana nao kisheria, kampeni ya jitomatazo ni namna yetu ya kuonesha kutokuridhika kwetu.

Na hakuna makosa: #JitomatazoMx inalenga hasa kukusanya nyanya na kuwarushia maafisa wa serikali.

Siku zimebaki chache. Wiki hii tunaanza kufanya kazi kama kikundi cha watu wanaopinga mwenendo tusioridhika nao. #PoliticsWithoutPrivileges

Mtumishi wa kwanza wa umma kupata kadhia ya Jitomatazo alikuwa mbunge Cesar Camacho anayetoka chama cha Institutional Revolutionary Party (PRI), ambacho kimekuwa madarakani kwa miaka 70 kikiongza serikali ya Mexico, na hivi karibuni kimerudi madarakani chini ya Rais Enrique Peña.

Wakosoaji wa Camacho wanasema alipokea “Zawadi ya Krismasi ” Desemba iliyopita, na kuibua maswali na wasiwasi mwingi katika kipindi ambacho nchi inaendelea kukabiliana na mdororo wa uchumi na kupanda kwa bei za mafuta.

Kwa kutumia kura za maoni za mtandaoni, Mlengwa anayefuata wa vuguvugu la #JitomatazoMx atakuwa nimwigizaji mwenye miaka 83 aitwaye Carmen Salinas — ambaye pia ni mbunge wa chama cha PRI aliyeshinda kiti hicho pamoja na kutokuwa na uzoefu wa elimu na siasa.

Akizungumzia umaarufu unaoongezeka wa Jitomatazo, mtaalam wa sayansi ya siasa Luis Rodolfo alitengeneza kura ya maoni kwenye mtandao wa Twita kupima mtazamo wa watu wanaofuatilia habari zake kwenye mtandao huo kuhusu aina hii ya upinzani wa hali ya mambo:

Unakubaliana au unapingana na #jitomatazo? ???

Camacho, wakati huo huo, amefungua mashitaka ya jinai  dhidi ya Arne aus den Ruthen Haag, akimtuhumu kwa kufanya kile anachokiita “utovu wa nidhamu wa kisheria.”

Wengine kwenye mtandao wa Twita wanasema hawakubaliani na Camacho, wakipinga kitendo cha kurusha nyanya kinachoonesha matumizi ya nguvu:

@DarioJimenezL Kuhusu “jitomatazo,” ninapinga namna yoyote ya kitendo kinachotumia nguvu kinachoondoa fursa ya mapatano ya kijamii.

Ninapinga “jitomatazo” kwa sababu ni kitendo cha kutumia nguvu ambacho hakipunguzi tatizo na kinahamasisha matumizi ya siala, kwa hiyo tusiishabikie.

Mwaka jana, Arne aus den Ruthen Haag waliwaomba wananchi kutumia zana tumizi mubashara iitwayo Periscope kwa ajili ya kutangaza ushahidi wa tabia zozote zinazoonekana kuwa kinyume cha sheria,cha kidhalilishaji au kuumiza watu kinachofanywa na wananchi. Miezi michache baadae, aliachana na ajira ya umma na kuamua kutumia muda wake wote kwenye unaharakati.

*Angalizo la matumizi ya lugha: Kwenye mji wa Mexico City, wenyeji hutumia neno jitomate kumaanisha nyanya zenye rangi nyekundu. Tofauti hii inatokana na neno la asili náhuatl tomatl, ambalo ni mzizi wa  neno la sasa kama linavyotumiwa kaskazini mwa Mexico kumaanisha tunda hili.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.