Wiki tunakupeleka Brazil, Urusi na Tanzania. Tunaongea na mhariri wa Global Voices Nchi za Caribiani Janine Mendes-Franco kuhusu mwitikio wa kujitoa kwa Uingereza kwenye Umoja wa Ulaya kwenye eneo lake na pia tunaongea na mwandishi wa Global Voices Arzu Geybulla kuhusu kukosekana kwa haki za kijamii nchini Azerbaijan.
Shukrani nyingi kwa waandishi wetu, watafsiri na wahariri waliosaidia kufanikisha maandalizi. Toleo la leo linaangazia habari ziliandikwa na Amanda Lichtenstein, Kevin Rothrock, Fernanda Canofre, Janine Mendes-Franco na Arzu Geybulla.
Katika kipindi hiki cha Juma Lilivyokwenda Global Voices, tunasindikizwa na muziki kutoka Maktaba ya Free Music ukiwemo wimbo wa Please Listen Carefully wa Jahzzar; It Always Rains in England wa Ergo Phizmiz; Anxiety wa Kai Engel; Camera-Eye wa happiness in aeroplanes; Linger wa David Szesztay; na False Note wa VYVCH.
Picha iliyotumiwa kwenye alama ya SoundCloud ni ujumbe unaosamba kwenye mitandao ya kijamii kwenye nchi za Caribiani ujumbe unaosamba kwenye mitandao ya kijamii kwenye nchi za Caribiani .
Podcast: Play in new window | Download