Katika toleo hili tunakupeleka Somalia, Japan, China, Pakistan na Cuba.
Kwanza, tunakusimulia kuhusu tembo mpweke aliyepachikwa jina la Morgan aliyesafiri umbali wa maili 137 kutoka Kenya na namna anavyoweza kuwa ishara ya matumaini kwa nchi ya Somalia iliyoharibiwa na vita.
Kisha tunakuletea habari iliyoletwa kwetu na mhariri wetu wa Japan Nevin Thompson kuhusu mradi wa kufuatilia mienendo ya hivi karibuni ya wahanga wa janga la Tsunami mwaka 2011. Baada ya hayo tunakwenda Pakistani, ambako tunazungumzia mwisho mwema wa habari iliyoendelea kuandikwa kwa miaka mitano ya utekeji nyara, kutengwa na kutokuwa na tahayaruki.
Nchini China, tunakusimulia kuhusu watuamiji wa mtandao ambao hawana kingine zaidi ya kejeli kwa mwasisi wa Facebook Mark Zuckerberg, baada ya kuchapisha picha — kwenye ukurasa wake wa Facebook– ikimwonesha akifanya mazoezi kwenye eneo lisiloruhusiwa jijini Beijing. Mhariri wetu wa Asia Kaskazinimshariki Oiwan Lam anazungumzia habari hii.
Tunamalizia na mahojiano na Ellery Roberts Biddle, mkurugenzi wa mradi wetu wa utetezi [Advocacy], kuhusu ziara ya Rais Obama wa Marekani nchini Cuba iliyofanyika juma lililopita. Ilikuwa ni ziara ya kwanza ya rais wa Marekani aliye madaraka tangu 1928.
Katika toleo la Yaliyojiri Juma hili kwenye Global Voices, utapata wasaa wa kusikiliza muziki wenye haki miliki ya Creative Commons kutoka kwenye Maktaba ya Muziki wa Bure, ikiwa ni pamoja na Tafadhali Sikiliza kwa Makini ulioimbwa na JahzzarMexico ulioimbwa na Jimmy Pe, Matembezi ya Tembo na Podington Bear; Aguirre, Hasira ya Mungu na Gary Lucas; Fairy wa Second Hand Rose; na De Cuba na SONGO 21.
Matangazo ya Yaliyojiri Wiki hii yanaratibiwa na Mhariri wa Habari wa Global Voices Lauren Finch akishirikiana na mimi — Mhariri Mtendaji wa Global Voices. Tarajia kutusikia tena baada ya majuma mawili.
Picha iliyopamba habari hii imetumiwa kutoka Soundcloud: Tembo na Mtumiaji wa Flick Pauline Guilmot. Ilipigwa tarehe Juni 15, 2014. (CC BY-NC-ND 2.0)
Podcast: Play in new window | Download