Ellery Biddle awa Mkurugenzi Mpya wa Kitengo cha Utetezi, Global Voices

Ellery kwenye Mkutano wa Global Voices 2015 mwezi January. PHOTO: Jeremy Clarke

Ellery kwenye Mkutano wa Global Voices 2015 mwezi Januari. PICHA: Jeremy Clarke

Tunayo furaha kutangaza kwamba baada ya kuwa mhariri wetu wa kitengo cha Utetezi kwa miaka miwili, Ellery Biddle atakuwa Mkurugenzi mpya wa kitengo cha Global Voices Utetezi.

Tangu ajiunge na Global Voices kama mwandishi wa kujitolea mwaka 2010, Ellery amethibitisha kuwa mtetezi mwenye ari na nguvu wa haki ya uhuru wa kujieleza mtandaoni. Alipokuwa Mhariri wa kitengo cha Utetezi mwaka 2013, aliongeza viwango vipya vya uimara na mchanganyiko mzuri wa kimaeneo kwenye habari zetu, sambamba na kuwa na uelewa mkubwa wa sera za mtandao wa intaneti na utetezi wa uhuru wa kujieleza. Jitihada za Ellery zimewafanya waandishi wa habari za utetezi kiwango cha juu cha habari zao kuonekana na kadhalika wao kufahamika, ikiwa ni pamoja na vyombo vikuu vya habari kama vile The Guardian, The Washington Post, na Slate. Amefanya kazi kwa bidii kuwaunganisha waandishi wa Global Voices na wataalam wa sera za mtandao wa intaneti duniani kote, jitihada ambazo zilifanikiwa kuwafanya waandishi wengi wapate fursa ya kushiriki majadiliano ya kimataifa kuhusu haki za kidijitali.

Ellery with Global Voices friends in Berlin, July 2014. PHOTO: Subhashish Panigrahi

Ellery akiwa na marafaiki wa Global Voices jijini Berlin, Julai 2014. PICHA: Subhashish Panigrahi

Uelewa mpaka wa masuala mbalimbali alionao Ellery umemfanya apate heshima kama mtafiti wetu huru katika Global Voices. Anaendelea kujikuza kiujuzi kwa kutumia uelewa wake kama mtaalam wa Kituo cha Intaneti cha Berkman cha Chuo Kikuu cha Harvard. Mwaka huu, mapenzi yake ya muda mrefu na ufadhili alioupata kwa ajili ya kujifunza masuala ya Intaneti nchini Cuba yamekuwa mambo muhimu sana. Kadri uhusiano wa Cuba na Marekani na hata nchi nyingine za Amerika ya Kusini unavyobadilika, Ellery alileta mawazo mazuri sana kwenye mjadala wa sera na uandishi wa habari za teknolojia na haki za binadamu katika kisiwa hicho.

Ellery anachukua majukumu ya Mkurugenzi kwenye wakati muhimu sana katika Global Voices na kwenye uhuru wa kujieleza. Kazi yake iliyothibitika kuwa ni mchanganyiko wa uzoefu, mapenzi ya anachokifanya, fikra pana kimkakati, vyote kwa pamoja vitaendelea kuitumikia jumuiya na maono ya Utetezi vizuri. Tunasisimuka tunaposonga mbele chini ya uongozi wake!

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.