Ombi kwa Papa Francis Kuchukua Hatua Kupinga Madikteta wa Afrika

Abdoulaye Bah, mchangiaji wa Global Voices na mwanablogu wa Konakry Express ameanzisha ombi la mtandaoni kumwomba Papa Francis kuchukua hatua dhidi ya madikteta wa Afrika. Bah, ambaye aliwahi kuandika namna anavyokubaliana na baadhi ya misimamo ya kisiasa ya Papa, anapinga sifa zilizotolewa na Papa kwa viongozi watano wa Afrika kwa kuwakaribisha jijini Vatican. Ombi hilo linaomba kutokewa kwa adhabu kwa madikteta kama ilivyosemwa na wanachama wa Mafia wakati Papa Francis alipotembelea Calabria.

Papa Mtakatifu hivi karibuni alimpokea Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe, Rais Eduardo dos Santos wa Angola, Rais Obiang Nguema wa Guinea ya Ikweta, Rais Paul Biya wa Kameruni, na Rais Sassou Nguesso wa Jamhuri ya Kongo. Marais hawa watano walivunja rekodi ya dunia kwa kubaki madarakani kwa muda mrefu. Kwa kufanya hivi, wamejenga himaya zinazovuna raslimali za nchi, kuua watu wasio na hatia, kubaka wanawake, kutesa wapinzani na watetezi wa haki za binadamu. Himaya hizi zinafisidi taasisi, zinaharibu matumaini ya watu wao kwa kuharibu uchaguzi, na kugawa watu wao kwa kutengeneza chuki na kusababisha harakati za kuwapinga.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.