Nchini Tunisia, Swali ni Ikiwa ni Lazima Kupiga Kura au Kugomea Uchaguzi

2014 elections logo, via the Facebook page of the independent election commission

Nembo ya uchaguzi wa 2014, kupitia ukurasa wa Facebok wa tume huru ya uchaguzi


Kadri uchaguzi unavyokaribia nchini Tunisia, watumiaji wa mtandao wanajadiliana ikiwa uchaguzi huo una hadhi ya wao kupiga kura katika uchaguzi ujao wa wabunge na rais.

Uchaguzi wa Bunge la nchi hiyo utafanyika Oktoba 26 wakati duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais imepangwa kufanyika Novemba 23.

Hata hivyo, si kila mmoja anasisimka kukaribia uchaguzi huo baadae mwaka huu. Wale wasiopenda kupiga kura mara nyingi huzungumzia kutokuridhishwa kwao na utendaji wa kada ya wanasiasa katika miaka mitatu iliyopita, wakitumia hoja kuwa uchaguzi wa mwaka 2011 ‘hakuleta tija wala mabadiliko yoyote’.

Mwezi Oktoba 2011, Watunisia walipiga kura kuchagua Bunge la Katiba la Taifa (NCA) ambalo lilipewa jukumu la kutunga katiba mpya baada ya kung'olewa madarakani kwa dikteta Zeine el Abidin Ben Ali. Chama chenye mrengo wa Kiislam, Ennahdha kilipata asilimia 40 ya kura zilizopigwa.

Kama wengine wengi, Nymeria alishangazwa:

Nitafanya nini kwenye uchaguzi ujao> Sipendi chama chochote na najua kura isiyochagua chama chochote itaharibika

Mnamo Juni 24, mtumiaji wa twita Papillon, ambaye ana wafuasi 13,000 alibandika [fr] swali lifuatalo:

Personne de ceux qui encouragent au vote ne peut répondre à la question pourtant simple: a quoi ça a servi de voter le 23/10 ?

Hakuna yeyote kati ya hawa wanaowatia moyo [wengine] kupiga kura wanaweza kujibu swali hili, ambalo ni rahisi sana: je, uchaguzi wa Oktoba 23 [2011] ulileta faida gani?

Mwanablogu Saber Arabasta, mwenye wafuasi 12,000 alijibu [fr]:

@Papiillon: à connaitre l'équilibre des forces politiques dans le pays, à changer de gouvernement, à changer de président, à écrire une const

Ni kujua uwiano wa nguvu za kisiasa katika nchi hii, kubadilisha serikali, kubadilisha rais, kutunga katiba basi

Akaongeza kwenye twiti nyingine [fr]:

@Papiillon à débattre des lois, à débattre du budget, à décider d'un processus élctoral, de justice transitionnelle, changer de diplomatie

Kujadili sheria, kujadili bajeti, kuamua kuhusu zoezi la uchaguzi na kutolewa kwa haki ya mpito na kubadilika kwa diplomasia.

Mtumiaji Chikh Magon aliuliza [fr]:

@Papiillon à quoi sert de boycotter les élections, je te retourne la question ?

Ninawarudishia swali kwenu: kugomea kupiga kura kutasaidia nini?

Kwenye mtandao wa Facebook, Mwandishi wa habari na Mwanablogu Haythem El Mekki aliandika [fr]:

Bon les pro boycott et abstentionnistes : J'aurais bien aimé vous suivre et vous soutenir, mais il faudra me dire ce que vous avez prévu concrètement et de façon pragmatique… Quel résultat espérez-vous en prônant le boycott ? Enfin mis à part le fait de nous priver des voix de ceux qui souhaitent un changement plus que quiconque… Je suis aussi insatisfait et remonté contre la classe politique que vous, voire plus, mais je ne vois que du nihilisme dans votre approche que je trouve destructrice et infantile… Pourriez-vous me convaincre du contraire ?

Kwenu nyote mnaoshabikia kugomea au kuacha [kupiga kura], ningependa sana kuwafuata na kuwaunga mkono lakini hebu mniambie nini hasa mmekipanga kwa maana ya uhalisia na ufanisi…mtarajia kuona matokeo gani kwa kugomea kura? Ukiacha kuwanyima haki wale wanaotamani kuona mabadiliko kuliko mtu yeyote…mimi binafsi siridhishwi na tabaka la wanasiasa kama ambavyo siridhishwi na ninyi, tena zaidi. Lakini ninachokiona kwenu ni ubeuzi tu kwenye mbinu mnayotumia ambayo kwangu naiona kama isiyo na faida yoyote na ni ya kitoto…mnaweza kunishawishi kinyume chake?

Bechir Bizertino alitoa maoni [ar]:

قبل كل شي فسرلنا انت كيفاش بمشاركتك في الانتخابات لاختيار اي طرف من القذارة المفروضة علينا بش تغيير حاجة في البلاد … اما انا فمقاطع لانه صوتي لاي طرف حامج من الموجودين موش بش يصلح حتى شي وما عنده حتى قيمة بما انه الطبقة السياسية باكملها ما تسمع كان للسفراء الاجانب موش للشعب اللي وكلها لنيابته …. وبمقاطعتي فعلى الاقل رابح انه ما عطيتهمش اي شرعية ولم اوكلهم ولا يمكنهم ادعاء ذلك ….

Awali ya yote, umetueleza, namna ambavyo kushiriki uchaguzi kuchagua vyama vya hovyo tunavyoletewa kutabadili nchi. Kwangu, ninagomea uchaguzi kwa sababu kura yangu kwa chama chochote cha hovyo hakuna faida yoyote wala thamani yoyote kwa sababu tabaka lote la wanasiasa linasikiliza mabalozi wa kigeni na wala si watu waliowachagua…kwa kugomea uchaguzi, angalau siwapi uhalali wowote na kuwafanya wajifanyie mambo yao wenyewe bila kuigiliza kuwa [niliwasaidia]

Zenova Gamha Fehmi alibandika maoni haya [fr]:

A mon avis il faut aller voter, pour un parti ou un autre, dans cinq ans si on n'est toujours pas satisfaits on votera pour un autre et ainsi de suite, c le jeu.
Il faut aller voter, c un devoir envers ceux qui sont morts pour nous l'octroyer ce droit.
Ne vous attendez pas à un miracle suite aux élections, les tunisiens ont tendance à vouloir tout tout de suite ce qui relève de l'impossible!

Kwa maoni yangu, ni jukumu letu kupiga kura kwa chama chochote. Kwa muda wa miaka mitano, kama tutaendelea kutokuridhika, tunaweza kupiga kura kwa chama kingine tofauti na kadhalika, ndivyo mambo yanavyopaswa kwenda. Kupiga kura ni jukumu letu kwa wale wote walioyatoa maisha yao wakafa kwa ajili ya kutuletea haki. Msitarajie miujiza baada ya uchaguzi, Watunisia wana tabia ya kutaka kila kitu kwa haraka bila kungoja, jambo ambalo haliwezekani

Wakati huo huo, tume huru ya uchaguzi ya nchi hiyo (ISIE) ilizindua kampeni ya kuwasihi Watunisia kujiandikisha kabla ya tarehe 22 Julai, kama wanataka kupiga kura kwenye uchaguzi ujao. Wale wote ambao hawatakuwa wamejiandikisha hawataweza kupiga kura.

Kampeni hiyo inawalenga wapiga kura wenye sifa wapatao milioni 4 ambao hawakujiandikisha kwenye uchaguzi wa Oktoba 2011 wa kuchagua bunge la katiba.

Kufuatia kujitokeza watu wachache sana waliokadiriwa kuwa asilimia 50 tu mwaka 2011, tume ya uchaguzi na makundi ya asasi za kiraia yana wasiwasi kwamba katika uchaguzi wa mwaka huu watu wachache zaidi watajitokeza hasa baada ya kukatishwa tamaa na yanayofanywa na vyama vya siasa.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.