Ungana na wanablogu wa Naijeria Blossom Nnodim (@blcompere) na Nwachukwu Egbunike (@feathersproject), pamoja na mhariri wa Global Voices Ndesanjo Macha (@ndesanjo) kutoka Tanzania kwenye kampeni ya kutuma twiti barani Afrika kuwaunga mkono wanablogu na waandishi tisa waliokamatwa mwishoni mwa mwezi Aprili na kwa sasa wanashikiliwa nchini Ethiopia.
Jumuiya ya Global Voices na mtandao wa marafiki na washirika wetu tunadai kuachiwa kwao, kwa kuwa walifanya kazi kwa bidii katika kupanua fursa ya uchambuzi wa kijamii na kisiasa nchini Ethiopia kupitia uandishi wa kiraia na ule wa kawaida. Tunaamini kukamatwa kwao ni kuvunja haki yao ya kimataifa ya uhuru wa kujieleza, pamoja na haki ya kutokukamatwa bila utaratibu. Unaweza kupitia habari hii na kampeni ya kuachiliwa kwao hapa.
Jumatano hii, kuanzia saa 8 mchana za Afrika Magharibi, tunapanga kutwiti kwa viongozi wa kijamii, serikali na wanadiplomasia, na vyombo vikuu vya habari (kwa kutumia anuani zao za twita) ili kufanya suala hili lisikike zaidi. Tunawahamasisha wanablogu na watumiaji wa mitandao ya kijamii barani Afrika kutuunga mkono –lakini kila mmoja anakaribishwa!
#FreeZone9Bloggers: Zoezi la kutuma twiti Kudai Kuachiliwa kwa Wanablogu wa Ethiopia Waliokamatwa
Tarehe: Jumatano, Mei 14, 2014
Muda: Saa 8 – 11 jioni Kwa saa za Afrika Magharibi/ Saa 10 – 1 Jioni Kwa saa za Afrika Mashariki (bofya hapa kujua itakuwa saa ngapi nchini kwako)
Alama Habari: #FreeZone9Bloggers
Waratibu: Blossom Nnodim (@blcompere), Nwachukwu Egbunike (@feathersproject), Ndesanjo Macha (@ndesanjo)
Ungana nasi Jumatano hii — twiti mpaka vidole vyako viume na dai kuachiliwa huru kwa wanablogu wa Zone 9!
Twiti unazoweza kutumia (bonyeza hapa kuchagua zaidi)
- Waachie wanablogu wa Zone 9… kwa sababu kublogu sio jinai! #FreeZone9Bloggers http://bit.ly/1g65ijg
- “Tunablogu kwa sababu tunajali” #FreeZone9Bloggers http://bit.ly/1g65ijg
- Unagana nasi kutia saini @globalvoices barua ya kuomba kuachiwa kwa waandishi habari na wanablogu nchini #Ethiopia #FreeZone9Bloggers bit.ly/1njZMRH
- Tuma picha yako kwa #FreeZone9Bloggers mtandao wa Tumblr na unga mkono kuachiwa kwao! bit.ly/1g6qmWT
- Kukamatwa kwa wanablogu nchini #Ethiopia ni kuvunja Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu #FreeZone9Bloggers http://bit.ly/QlzRuG
- Mkataba wa Afrika unalinda haki ya uhuru wa kujieleza #FreeZone9Bloggers http://bit.ly/QlzRuG
- Kukamatwa kwa wanablogu nchini #Ethiopia kunavunja Tamko la Kimataifa la Haki za Kiraia na Kisiasa #FreeZone9Bloggers http://bit.ly/1g1MUNM
- Kukamatwa kwa wanablogu nchini #Ethiopia kunavunja Ibara ya 9 & 14 ya ICCPR #FreeZone9Bloggers http://bit.ly/1g1MUNM