Wabunge wa Yuan nchini Taiwan walipitisha muswada wa kwanza ya “Usawa kwenye Ndoa“ [zh] mnamo Oktoba 25, 2013. Novemba 30, zaidi ya watu 300,000 walipinga muswada huu, hasa dhidi ya pendekezo juu ya ndoa za jinsia moja. J. Michael Cole, mwandishi wa habari wa kujitegemea mkaazi wa Taipei, alielezea kile yeye alichokiona katika maandamano hayo katika blogu yake.