Uhispania Si Taifa la Watu Wenye Furaha Sana

Inaonekana Uhispania si taifa lenye watu wenye furaha. Kwa mujibu wa utafiti ulifanywa na Chuo Kikuu cha Carlos mjini Madrid (uc3m) [es], Wahispania wanashika nafasi ya 49 kwa furaha katika ya nchi 112 duniani zilizohusishwa na utafiti huo.

kdmskdfnwkjd Hiki Kielelezo cha Furaha (pdf) hakitokani na maswali huru yaliyoulizwa, bali kimetokana na “utashi uliogunduliwa,” kwa kutumia uhamaji kama kigezo; yaani, kile watu wanachokifanya, na sicho kile wanachokisema. Per Juan de Dios Tena [es], profesa wa takwimu katika  Chuo Kikuu cha Carlos anasema: “Wimbi la Uhamiaji lina uhusiano na masuala la kisaikolojia yanayohusiana na furaha,” yaani, watu huhama nchi kama wanakosa mazingira ya furaha, na hivyo kupendelea maeneo mengine wanayodhani yatawapa furaha.
Watafiti walizingatia sababu za kiuchumi na zile zisizo za uchumi zinazomfanya mtu kuwa na furaha, ambazo zinaingilia na na kile kinachoweza kuchukuliwa kuwa mambo yanayosababisha uhamaji: kipato kisichotosha, sura ya idadi ya watu wa mahali, maendeleo ya kijamii, mahusiano na watu wengine na sifa za mahali anakoishi mtu, pamoja na vibadilika (viriables) kama umbali au kupakana kwa nchi na lugha.

Kwa kuzingatia sababu zote hizi, huku ikiongozwa na Hong Kong, Singapore na New Zealand, Uhispania imeshikilia nafasi ya 49 kati ya nchi 112 katika orodha hiyo, ikifuatiwa na Mexico, Iran na Costa Rica, kw auchache. Zilizoshika mkia ni Afghanistan, Afrika Kusini na China.

Mwandishi Tena pia anadai kuwa uhamiaji hautegemeani tu na uwezekano w akupata kazi, kama inavyofikiriwa mara nyingi, bali pia na uharibifu wa mazingira, ugaidi na kutokuwepo usawa wa kiuchumi, vibadilika (variables) ambavyo wanasaikolojia wanadhani ni vielelezo vya furaha.

Utafiti huo unahitimisha kuwa ustawi wa watu hauwezi kupimwa kwa kipato pkee na unabainisha kuwa sea nzuri huongeza ari ya watu kusihi nchini mwao, wakati zile mbaya hupunguza ari hiyo.

Hapa kuna twiti kadhaa zinazojibu utafiti huo:

Uhispania iko mbali kutoka kwenye kilele cha orodha hiyo ya furaha kwa mujibu wa  UC3M.. wala huwa hatucheki, ni wazi hata hiyo nafasi hatustahili sasa  

— Beatriz Bonmatí (@b_bonmati) September 23, 2013

@marianorajoy Tunahitaji kandanda, ni dharura!: Orodha nyingine ya furaha inaonyesha Uhispania iko mbali kabisa na kilele cha orodha http://t.co/kNJqZKXZDZ

— Hrœrekr (@iGNUrante) September 23, 2013

NANI ANADHANI HII SI KAWAIDA???? KWA KASI HII TUTAKUWA WA 112 NDANI YA MIEZI MICHACHE…. http://t.co/ppWpTHl9TZ

— AutonomosEnLaLucha (@UNI_CAES) September 23, 2013

1 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.