Habari kutoka 7 Oktoba 2013
‘Mwanablogu Mzuri Lazima Awe na Sifa za Asili za Waandishi Wazuri wa Habari’
Dorothée Danedjo Fouba, mshindi wa tuzo ya “Blogu Bora ya Teknolojia Afrika, iliyotolewa Tuzo za Uandishi wa Kiraia za Telkom-Highway Africa 2013“, alizungumza na Dibussi Tande (@dibussi) kuhusu maendeleo yake katika tasnia hii, na sifa zinazohitajika ili kufanikiwa.
Fuatilia SafariYaGariAfrika Mtandaoni
Kikundi cha watengenezaji na wabunifu wa teknolojia kutoka Ulaya ambao wanadadisi ukuaji wa vituo vya teknolojia barani Afrika wanaendelea na safari yao ya gari barani humu. Tazama blogu yao au Tumblr na ufuatilie mjadala kuhusu safari yao kwenye mtandao wa Twita.
Mwenendo wa Mashitaka ya Wanasiasa wa Kenya Mjini Hague
Mashitaka ya Kenya Hague ni mradi wa Dawati la Afrika la Radio Netherlands Worldwide kwa ushirikiano na This is Africa (Hii ni Afrika): Namna gani ghasia za baada ya uchaguzi nchini Kenya mwaka 2007 na 2008 ziliathiri maisha yako? Unataka kufahamu nini kuhusu haki ya kimataifa? Changia habari ulizonazo, mawazo...
Je, Kutakuwa na Fungate kwa Marekani na Irani?
Raia wa Iran hawakubaliani ikiwa mahusiano mazuri yaliyoashiriwa na tukio la kupigiana simu kati ya Marais Obama na Rouhani ni jambo jema.
Uhispania Si Taifa la Watu Wenye Furaha Sana
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Carlos III University mjini Madrid, wa-Hispania wameshika nafasi ya 49th ya furaha kati ya nchi 112
Wali Unaonata Haufai kwa Watoto, Akina Mama Waambiwa
@LaotianMama anawakumbusha akina mama wa Lao kutokuwalisha watoto wenye njaa wali unaonata ambao ni chakula cha asili kwao. Wali unaonata kwa watoto wachanga ni sawa na punje za wali katika utamaduni wa ki-Magharibi. Wazo ni lile lile kuwa kuwapa watoto wachanga chakula kigumu kutawashibisha. Kwa hiyo, kuwaanzishia watoto wachanga chakula...
Masuala Matano ambayo Raia wa Brunei Wanahitaji Kuyajadili
Teah Abdullah anaorodhesha masuala matano ambayo raia wa Brunei citizens wanahitaji kuyajadili: Kuimarisha lugha halisi, ngono baina ya ndugu wa damu, maisha ya anasa, ulaji unaozidi kiwango wa “baga” [aina ya mandazi yenye nyama], utegemezi uliopitiliza kwa serikali. Anafafanua kwenye suala la mwisho: …serikali ni sehemu muhimu katika maisha yetu...
India: Saa Nzuri Kapata Huduma za Afya Hospitalini kwa Punguzo la Bei
Kamayani wa mtandao wa Kracktivist anasema kuwa dhana ya saa nzuri kupata punguzp la bei, ambayo ni maarufu sana kwenye vilabu vya pombe, mahotelini na hata kwenye majengo ya sinema, imeingia hadi kwenye sekta ya afya nchini India. Hospitali binafsi iliyoko Bangalore siku za hivi karibuni imekuwa ikitoa punguzo la...
Nani ni Muislamu Halisi? -Hatari ya Madhehebu Madogo ya Waislamu Pakistan
Raza Habib Raja wa Pak Tea House ana maoni haya: ‘Kosa’ kubwa nchini Pakistani ni kuwa kile ninachokiita, Muislamu asiye Muislamu. Kwa hiyo hata ukiwa Ahmedi, Shiite, na hata muumini wa Mtakatifu Sufi bado utaitwa Asiye Muislamu na baadhi ya watu. Hilo linatuleta kwenye swali “nani ni Muislamu?” Raja anaeleza:...