GV Face: Kupigania Mtandao Huru wa Intaneti Nchini Brazil

Je, unajali uhuru wa maoni kwenye mtandao? Vipi kuhusu faragha yako mtandaoni? Vipi kama serikali yako ingetunga sheria ambayo ingeweza kulinda haki hizi, badala ya kuzitishia?

Watetezi wa haki za kidijitali nchini Brazili wamekuwa wakifanya kazi kwa miaka mingi kupitisha Marco Civil da Internet, sheria ya aina yake inayolinda haki na uhuru mtandaoni.

Mipango ya kufuatilia mawasiliano ya watu ya Serikali ya Marekani imelifanya suala lipewe kasi mpya, likipata uungwaji mkono kutoka katika vyama vya kiraia na hata rais wa Brazil, Dilma Rousseff.

Wiki hii kwenye sehemu ya , Mhariri wetu wa Utetezi Ellery Biddle (@ellerybiddle) alizungumza na wataalamu waliobobea kwenye suala, mmoja wapo akiwa ni mwandishi wa GV Raphael Tsavkko @Tsavkko, Carolina Rossini (@carolinarossini) naJoana Varon (@joana_varon) mwandishi wa mwanzo wa muswada huo.

Kwa viungo zaidi na maoni katika suala hili, tazama kwenye ukurasa wetu wa matukio wa Google +.

1 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.