Mapinduzi Nchini Niger: Wanablogu Wapumua Pumzi ya Ahueni

Picha ya kuchora ya Mamadou Tandja iliyoning’inizwa katika ofisi ya Rais (Picha na Jacob Silberberg wa Panos Pictures)

Picha ya kuchora ya Mamadou Tandja iliyoning’inizwa katika ofisi ya Rais (Picha na Jacob Silberberg wa Panos Pictures)


Alhamisi Februari 18 mapinduzi ya kijeshi yalifanyika nchini Niger ambayo kwayo Rais Mamadou Tandja alikamatwa baada ya mapambano ya bunduki katika mji mkuu, Niamey, yaliyoongozwa na Kanali Abdoulaye Adamou Harouna (Amabaye alikuwa mpambe wa aliyekuwa kiongozi wa mapinduzi ya kijeshi yaliyopita Meja Daouda Mallam Wanke).
Katika hatua ambayo haikupendwa, miezi michache iliyopita Tandja alibadilisha katiba kinyume cha sheria ili ajiruhusu kuongoza kwa muhula wa tatu katika kile ambacho kilionekana kama dhuluma ya halaiki kwenye kura maoni (angalia muhtasari wa Jen Brea kuhusu maoni yaliyosababishwa na uamuzi huo).

Kwa masaa machache, hali ya kutoelewa kinachoendelea ilitawala. Raffaella Toticchi aliyekuwa mjini Niamey aliandika siku ya Alhamisi mchana [Es]:

Se han oído también disparos y algunas personas han sido heridas y trasladadas al hospital más cercano, pero de momento no se sabe mucho más.

Risasi zimesikika na baadhi ya watu wamejeruhiwa na kupelekwa katika hospitali ya Karibu zaidi, lakini kwa wakati uliopo hatufahamu vizuri kuhusu jambo hilo.

Katika tangazo lilitolewa kwa njia ya televisheni, msemaji wa waliofanya njama (za kupindua) Abdoul Karim Goukouyé alisema kuwa katiba imesimamishwa na vyombo vyote vya dola vimevunjwa. Instantanés du Niger [Fr], blogu ya mfanyakazi wa kifaransa anayeishi mjini Niamey, aliripoti kuwa wakati wa kuelekea kutolewa kwa tangazo hilo.idhaa ya taifa ya Televisheni ORTN ilirusha hewani muziki wa kijeshi kwa kipindi kirefu jioni ile. Pia aliritaarifu kwamba kwa muda wote uliobaki jioni ile na siku iliyofuata kulikuwa shwari.

Mwanablogu Texas in Africa anatoa picha na sababu za mapinduzi hayo ya kijeshi:

Kwanza, kadri ya raia milioni 7.8 (3/5) wa Niger wanaishi bila ya usalama wa chakula katika kiwango kibaya sana au kiwango wastani.

Jambo la pili, na muhimu zaidi, Rais Tandja aliwakasirisha Wa-Niger wengi wakati alipuvunja bunge na kusimika mageuzi ya kikatiba ambayo yalimpa nguvu kubwa zaidi huku kukiwa na udhibiti mdogo. Tandja alitakiwa na katiba kuondoka madarakani mwezi Disemba, kwani huo ndio ulikuwa mwisho wa muhula wake wa pili wa kipindi cha miaka mitano mitano madarakani, lakini mabadiliko aliyoyafanya kwenye katiba yalimruhusu akae kwenye madaraka kwa miaka mimgine mitatu. Hatua hizo hazikupendwa kabisa; waandamanaji 10,000 walijitokeza Jumapili ili kupinga vitendo vya Tandja.

Wazi, mapinduzi haya ya kijeshi ni matokeo ya mgogoro wa kisiasa unaoendelea.

Kama ilivyowekwa na mtoa maoni wa Ki-Niger Ali Dan-Bouzoua katika mjadala kuhusu intaneti katika Niger, kwa bahati mbaya hakuna kiwango cha kutosha cha uanahabari wa kiraia unaoandika juu ya tukio hili:

Tres peu de blogs ou de tweeter, de photo … sur la situation au Niger.

On consomme sur le net mais on ne produit rien. Les guinéens sont tres actifs et tres present sur le net.

Blogu chache mno au twita, picha… zinazohusu hali ilivyo nchini Niger.
Tunatumia yaliyoko kwenye mtandao lakini hatuyangenezi (maudhui) hayo. Wa-Guinea wako hai na wana uwepo kwenye mtandao wa intaneti.

Hata hivyo, Wa-Niger wamejieleza kupitia maoni yaliyoachwa katika tovuti za habari kama vile tamtaminfo.com wanaonekana kuunga mkono kuondolewa madarakani kwa rais Tandja licha ya kuwa na tahadhari kwa serikali ya mpito:

Ousman Diallo Yacoubou:

Militaires de notre cher pays tout le peuple nigerien vous salut vous avez prouve que vous etes les vrais garants du peuple et de la democratie. Mais il y'a une chose jusqu'a present on ne connait pas la duree de votre transition.

Kwa jeshi la nchi yetu tunayoipenda, Wa-Niger wote wanawasalimu, mmedhihirisha kuwa ninyi ni walinzi wa kweli wa wananchi na demokrasi. Lakini mpaka sasa kuna jambo tusilolifahamu: muda wa serikali yenu ya mpito.

Sabitou Oumarou:

C'est domage que des democrates comme nous applaudisse un coup d”Etat. Mais nous devons savoir qu'il y a deux manière de combattre : l'une avec la raison et l'autre avec la force. La première est propre aux hommes la deuxième nous est commun avec les animaux. Mais quand la première montre c'est limites il faut bien recourir a la deuxième pour remettre l'ordre et fait respecter la loi.

Ni aibu kwamba wanademokrasia kama sisi tunashangilia mapinduzi ya kijeshi. Lakini inatubidi tutambue kuwa kuna njia mbili za kupambana: moja kwa mantiki na nyingine kwa kutumia nguvu. Njia ya kwanza ni ya kipekee kwa wanadamu wote, njia ya pili ni sawa na ya wanyama. Ya kwanza inapoonyesha kikomo chake, ni lazima kifikia ya ile ya pili ili kurejesha amani na heshima kwa sheria.

Sawasawa na hivyo, wanablogu wachache wa Kiafrika na watumiaji wa twita wametoa mitazamo yao kuhusu mapinduzi hayo ya kijeshi, wengi wao wakielezea ahueni au kusherehekea kuondolewa kwa Tandja kutokana na mabadiliko haramu ya kikatiba aliyoyapitisha mwaka jana. Kama vile Ato Kwamena Dadzie wa Ghana, ambaye anatoa mwangwi wa hisia za wengi:

Awada Ehemir kutoka Chad [Fr] anafikiri kuwa mitazamo juu ya mapinduzi haya ya kijeshi ni ya kinafiki:

Mapinduzi ya kijeshi nchini Niger… mara moja yanashutumiwa, lakini mwezi ujao yatakubaliwa na kila mmoja. Ndio mtindo wa Afrika…

Na umoja wa Afrika ambao uanjidai kushutumu! Katika kikao kinachofuata, watatandaza zulia jekundu kwa “marafiki” zao wapya!

Tony Cassius Bolamba kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo [Fr] anaonyesha uelewa kwa waliopindua katika blogu yake:

Si je me penche du côté de la raison je condamnerai tout putsch et tout tripatouillage de constitutions en Afrique, mais la compréhension m’oblige de comprendre certains putschistes.

Raison aux pensées de Pascal ? « Ne pouvant justifier la justice, on a justifié la force ».

L’Homme ne récolte ce qu’il sème et t il faut avoir le flair de quitter les choses avant qu’elles ne vous quittent.

Espérant que ce nouveau coup de force au Niger bénéficiera au vrai détenteur du pouvoir: le peuple !

Kama itanipasa kuegemea kwenye upande wa mantiki, Ninashutumu mapinduzi yote na kuingiliwa kwa katiba barani Afrika, lakini inanibidi kuwaelewa viongozi wa mapinduzi haya.
Je Pascal alikuwa sahihi? “ Tunaposhindwa kuhalalisha haki, basi tunahalalisha nguvu”.

Watu huvuna wanachopanda na inawabidi wahisi muda wa kuyaacha mambo yaende yenyewe kabla mambo hayajawaacha.

Tunatumaini kuwa mapinduzi haya mapya ya kijeshi nchini Niger yatawanufaisha wenye nguvu wa kweli: wananchi!

Katika mkondo unaofanana na huo, blogu ya Guinée 50 [Fr] inatumaini kuwa mapinduzi yarejesha demokrasi nchini Niger.

Ni lui (Tandja) ni les militaires qui l’ont renversé, ne portent le manteau de la légalité constitutionnelle. Il n’est donc pas question pour nous citoyens africains, de juger la manière dont nous en sommes soulagés.
La bonne question n’est pas non plus de d’applaudir aveuglement ces militaires. Mais, d’exiger leur neutralité dans la restauration de la démocratie dans un bref délai.
[…]
Nous sommes optimistes pour la suite, car à force de mal aller, tout ira bien dans le sens voulu par nos peuples qui sont les seuls souverains.

Si yeye (Tandja) wala utawala wa kijeshi ambao umempindua wanaburudika na kisingizio cha uhalali wa katiba.
Kwa hiyo, hakuna njia ambayo sisi raia wa Afrika tunaweza kuamua njia ambayo tutapata ahueni.
Hakuna ubora katika kuwashangilia hawa waliopindua kama vipofu. Bali kuwataka wasipendelee upande wowote wakati wa kurejesha demokrasi.
[…]
Tuna matumaini kwa yale yatakayojiri baada ya hapa, kwani mambo yanavyozidi kwenda kombo, basi mambo yote yatakwenda sawa katika jinsi ambavyo watu watatataka, watu ambao ndio pekee wenye nguvu.

Katika tovuti ya uanahabari wa kiraia Sahara Reporters,, watoa maoni wengi wa kutoka Naijeria walionyesha yale yanayofanana kati ya hali ilivyo nchini niger na hali katika nchi yao. Hii ni mifano miwili:

OHYN:

Hiki ndicho kinachotokea pale ambapo raia na taasisi za kiraia zinapokwa dhaifu mno, zinazoogopa sana, na zenye “maneno matupu,” katika kulinda uhuru wao kutoka kwa wanyakuaji wa madaraka wanaoitwa viongozi. Hili linaielezea naijeria fika: kwa hiyo, Naijeria inafuata katika msululu huu wa mapinduzi; ni mantiki tu na mambo yameshaiva.


Toyin Ade:

Hakuna tofauti kati ya kilichotokea Niger & Naijeria, tunao wala njama wasio na roho, wachafu na wasio na uzalendo wanaotuweka rehani kama vile alivyofanya tandja nchini Niger. Kama kutakuwa na mapinduzi yoyote ya kijeshi nchini naijeria, yanapaswa yalengwe kwa vikaragosi wasio na maana wanaojiita jiko/choo cha baraza la mawaziri la Yar’Ardua amabo wamejipatia yale ambayo hawana.

Daniel Hongramngaye kutoka Chad, pia anaonyesha yale yanayofanana kati ya Niger na nchi yake katika blogu ya Makaïla [Fr]:

Ce qui se passe sous nos yeux chez nos voisins nigériens doit à plusieurs égards inspirer nos officiers supérieurs, nos militaires, nos dignes soldats s’il en existe encore. […]

La situation politique au Tchad est pourtant plus exécrable que celle du Niger.

En effet, Idriss Deby Itno est identique à Mamadou Tandja si non pire.

Kinachotokea chini ya macho yetu katika nchi jirani yetu ya Niger, kinatakiwa kwa namna kuwatia moyo maofisa, jeshi letu, wanajeshi wetu wenye thamani kama bado kuna waliosalia. […]
Hali ya kisiasa nchini Chad nim baya zaidi ya ile ya Niger.

Kwa kweli, Idriss Deby Itno anafanana kabisa na Mamadou Tandja kama ikiwa hajazidi kwa ubaya.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.