Mwanamuziki mmoja wa Afrika Mashariki awashinda wengine wote kwa umaarufu wa mtandaoni duniani

Si wengi wanamfahamu kama Mwanaisha Abdalla bali kama Nyota Ndogo, ni jina linalojulikana kwenye kila nyumba katika Afrika Mashariki.

Kazi ya sanaa ya kasha la Albamu ya Nyota Ndogo iitwayo – Mpenzi

Kazi ya sanaa ya kasha la Albamu ya Nyota Ndogo iitwayo – Mpenzi


Amekuwa akijikusanyia mashabiki wa muziki wa mahadhi ya Afrika Mashariki kwa zaidi ya miaka mine sasa. Blogu yake kwa upande mwingine imekuwa ikifanya kazi kwa miaka mitatu. Hakuna shaka kwamba blogu yake imechangia kukua kwa umarufu wake wa mtandaoni.
Akiwa amezaliwa mwaka 1981 kwenye Jimbo la pwani la Mombasa, Nyota Ndogo ametokea kwenye historia ya kinyenyekevu. Aliacha shule akiwa na umri mdogo na baada ya muda, akafanya kazi kama mfanyakazi wa ndani mpaka alipogunduliwa na Andrew Burchell kama mtu mwenye kipaji cha kuimba.

Sasa ana CD tatu zilizotoka kwa jina lake, CHEREKO, NATOKA MBALI NA WEWE na MPENZI. Ameshirikishwa vilevile katika makusanyo matatu ya kimataifa kama WORLD 2003, THE ROUGH GUIDE TO KENYA na OFF THE BEATEN TRACK. Pia anashikilia mbili ya Tuzo za muziki za Kisima za Kenya: Mwimbaji bora wa Taraab 2003 na Mwimbaji bora wa kike 2005.

Nyimbo zake ambazo nyingi ni za Kiswahili zenye maneno machache ya Kiingereza zinaimbwa kwa mahadhi ya Taarab yanayosikika zaidi kwenye ukanda wa mwambao wa Afrika Mashariki na pia Kapuka na Genge, mahadhi ya muziki unaosikika zaidi maeneo ya bara ya Kenya.

Je ni namna gani mtu mwenye historia kama hiyo anaweza kujifunza kuutumia mtandano wa intaneti kwa faida yake kama Msanii wa Kenya anayechipukia? Hili ni swali linalokujia kichwani unapotembelea blogu yake.

Humo, anasema kila kitu kinachomhusu yeye kama msanii kwa kutumia mtazamo binafsi ukilinganisha na habari na taarifa za vyombo vya habari zinazohaririwa ambapo mtu anaweza kuzipata kwenye sehemu ya burudani wkenye magazeti na majarida.

Kutoka kwenye video za nyimbo zake mpaka kwenye mashairi ya nyimbo zake mpaka kwenye picha zake zinazomwonyesha akitumbuiza na wasanii wenzake na mashabiki wake, mtu anaweza kujisikia kuunganishwa na kuwekwa karibu zaidi na Nyota Ndogo kwa kupitia blogu yake.

Kublogu hakujawa uzoefu rahisi kwake kama alivyokiri kwenye makala yake ya blogu ya tarefhe 27 Julai, 2006 saa 7.43 mchana.

Almanusura niachane na blogu yake kwa sababu ilikuwa inaniwia vigumu kupata mtundiko mpya. Kumbe ilikuwa ni mimi niliyekuwa natumia kivinjari kisichopatana. Kwa hiyo nimerejea na kivinjari cha zamani Internet explorer. Kama hii itafanya kazi tegemea picha kadhaa hivi karibuni sababu mengi yametokea.x

Kwa kuangalia kwenye posti za hivi karibuni kwenye blogu yake, kwa hakika mtu anaweza kuona kuwa Nyota amefahamu vizuri sana kutumia vyenzo za kublogu. Hili kwa bahati mbaya sana haliwezi kusemwa kwa Wasanii wengi wengine wa Afrika Mashariki kwa sababu sikuweza kupata blogu yoyote ya msanii mwingine.

Inaonekana, mtu hahitaji kuwa msomi kujua namna ya kublogu, baada ya yote, ni nyenzo tu.

1 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.