Tetemeko la ardhi la wastani lilitikisa jiji la Dhaka siku ya tarehe 27 Julai mnamo muda wa saa 00:51 kwa saa za Bangladeshi (+6 GMT). Russell John anaripoti katika blogu yake:
Nilikuwa nimelala kwenye kitanda changu huku nikongea kwa simu na rafiki yangu, na ghafla nikahisi kitanda kikitetemeka. Ndani ya sekunde 3 kikasimama. Kwa mtazamo wangu wa kwanza nilidhani ni paka aliyeingia kwenye uvungu wa kitanda na alikuwa akikisukuma-sukuma kitanda, lakini nikagundua kuwa hilo lisingewezekana kwani kitanda ni kizito mno. (aidha hapakuwa na paka, nilihakikisha!)
Niliwauliza marafiki zangu haraka kwa kutumia IRC, na wao wakasema walihisi (tetemeko) pia.
Kwa hiyo lilikuwa ni tetemeko kwa hakika! Tetemeko ndani ya Dhaka saa 6.51 za usiku.
Russell alituma ujumbe wa tweeter mara moja:
Mungu wangu, nimelihisi tetemeko la ardhi!
Katika dakika chache zilizofuata, jumbe za tweeter zikaanza kutokea zikithibitisha kwamba nao pia walilihisi tetetmeko.
Munaz wa Nothing to lose and Nothing to Gain akaanza kuonyesha jumbe nyingine za tweeter zilizotumwa na marafiki zake:
Ilikuwa ni vigumu kupata habari katika mtandao (isipokuwa kwenye blogu za lugha ya ki-bangla) na kila mtu alikuwa akijaribu kupata habari zilizosasishwa. Hivyo Bauani wa Information blogs akawasiliana na U.S geological Survey, National Earthquake Information na akabadika ujumbe wa alichokipata:
Ukubwa: 4.9
Tarehe-saa: Jumamosi, Julai 26, 2008 saa 18:51:49 UTC
Sehemu: 24.773°Maskasini, 90.480°Mashariki
Urefu kwa kwenda chini: km5.2 (maili 3.2)
Eneo: BANGLADESHI
Alikuwa pia akituma jumbe zilizosasishwa kama na wakati habari mpya zilivyopatikana.
Hapakuwa na majeruhi walioripotiwa lakini (tetemeko) lilitikisa na kuwaathiri watu wa jiji kubwa lenye wakazi wengi la Dhaka.
Rumi wa In the Middle of Nowhere anaandika:
Kama naweza kuiona Bangladeshi kwenye ramani ya dunia, utaona mipaka ya sahani mbili, yaani, mistari ya inayokutanisha (au kutenganisha) magamba ya miamba-nchi inapita katikati ya Bangladeshi… wanasayansi wengi wamekuwa wakionya kuhusu uwezekano wa kutokea kwa tetemeko la ardhi lenye athari kubwa, 8-9 kwa vipimo vya skeli ya rikta huko kaskazini-mashariki na kusini-mashariki mwa Bangladeshi.
Kwa hiyo (a) kuna uwezekano wa kutokea tetemeko kubwa la ardhi katika Bangladeshi. Je tupo tayari?
3 maoni
Congrats on this outstanding new development. Best of luck!
Welcome to GVO, a Malagasy GVO traductor congrats you
Wonderful! Hurray for the 16th Lingua site:)