Habari kuhusu Habari za Wafanyakazi

Lebanoni: Wafanyakazi wa Ndani Wanaotoroka

“Mfanyakazi wa ndani anapotoroka kutoka kwenye nyumba ya mwajiri wake, kituo cha polisi hakiwezi kufanya lolote kwa sababu hakuna sheria dhidi ya wafanyakazi wa ndani wanaotoroka. Kwa hiyo ofisa wa kituo cha polisi anamwambia mwajiri wa ki-Lebanoni aseme kuwa (mtoro huyo) aliiba pesa,” anaandika Ethiopian Suicides.

Misri: Wafanyakazi wa IslamOnline Wagoma

Mamia ya wafanyakazi, wahariri, na waandishi wa habari walianza mgomo wa kuonyesha hasira yao katika mtandao unaosomwa sana wa jiji la Cairo unaojulikana kwa jina la Islamonline baada ya kuwa wafanyakazi wapatao 250 wamefukuzwa kazi. Kwa mara ya kwanza, wagomaji wanatumia kwa ufanisi na vizuri kabisa aina mpya ya chombo cha habari ili kuvuta usikivu na uungwaji mkono katika kile wanachokipigania, kuanzia na Twita inayoendelea mpaka mmiminiko wa habari wa hapo kwa hapo.

Japan: Mkeo anapougua

  2 Novemba 2009

Pale utamaduni wa “mifugo ya mashirika” au kwa maneno mengine “utamaduni wa ujumla wa wafanyakazi” (社蓄 shachiku) na maadili ya ndoa vinapogongana – zaidi ya watu 300 walitoa majibu kuhusiana na swali lililoulizwa kwenye jukwaa kubwa la mijadala lijulikanalo kama Hatsugen Komachi: Je, mwanaume aombe ruhusa kazini pale mkewe anapougua?...