Habari kuhusu Mawazo kutoka Novemba, 2009
Palestina: Mtaa wa Twita
Eman katika AquaCool anatoa maoni kuhusu mtaa wa kwanza kupata jina linalotokana na huduma ya Twita, katika kambi ya wakambizi huko ukingo wa Magharibi.
Syria: Simulizi Ya Ufukweni
Profesa wa Fasihi ya Kiingereza kutoka mji wa mdogo wa Tartous huko Mediterranean na mwandishi mwenye asili mchanganyiko ya Siria na Canada wakiwa safarini kuelekea kwenye nchi yake ya asili wanatizamana wakiwa kwenye mgahawa unaoitwa Sea breeze. Hivyo ndivyo Mariya na Abu Fares walivyoamua kuanza shani yao na kuwanasa kwa wasomaji wao. Yazan Badran anatupasha.
Misri: Mwanablogu wa Kiume Aagizia Bikra ya Bandia
Mengi yalisemwa na kuandikwa juu ya zana ya kutengeneza bikra ya bandia - mpaka mwanablogu Mmisri wa kiume Mohamed Al Rahhal akanunua moja. Marwa Rakha anatuletea habari hiyo.
Azerbaijan: Bikra
Mwanablogu wa Emotions on Air, Mind Mute anatafakari marajio ya jamii kwamba wanawake watabakia mabikira mpaka watakapofunga ndoa. Japokuwa ipo nchini Azerbaijan, blogu hiyo inabaini mfumo unaofanana wa maadili katika...