Syria: Simulizi Ya Ufukweni

Profesa wa Fasihi ya Kiingereza kutoka mji wa mdogo wa Tartous huko Mediterranean na mwandishi mwenye asili mchanganyiko ya Siria na Canada wakiwa safarini kuelekea kwenye nchi yake ya asili wanatizamana wakiwa kwenye mgahawa unaoitwa Sea breeze. Hivyo ndivyo Mariya na Abu Fares walivyoamua kuanza shani yao na kunaswa kwa wasomaji wao.

Mngurumo mdogo tumboni mwangu uliingilia ndoto yangu ya mchana wakati harufu ya viungo na samaki iliponipita. Nilijisikia kana kwamba sijakula kwa siku kadhaa. Niliangalia nyuma kupitia dirishani nikamuona muhudumu wa kike, akipumzika karibu na mlango ulioonekana kana kwamba ni wa jikoni. Alikuwa amezama kwenye kitabu lakini kana kwamba alikuwa na hisia ya sita, alibaini macho yangu ndani ya sekunde chache baada ya kuanza kumuangalia. Alitabasamu kwa ufahamu na kuijongelea meza yangu.
“Una njaa?”
“Oh, ndio! Je una orodha ya vyakula?”
“Sinayo hapa. Lakini nitakueleza ni chakula kipi kinachopikwa leo.”
“Ah mbingu.” Nilijiwazia na kumrejeshea kutabasamu, kwa hamu nikisubiri ufafanuzi wa chakula cha jioni.

Hadithi inaanza kwa urahisi kama hivyo. Waandishi hao wawili, ambao wanabadilishana sehemu kila juma, waliendelea kutokea hapo. Tunajifunza juu ya Yasmina, mwanafunzi wa zamani wa Profesa Youseff na mhudumu kwenye mgahawa wa Sea Breeze, na Yazan, mpishi asiyejali, yote yakiwa katika mandhari ya ufukweni mwa mji Tartous, pamoja na uandishi maridhawa wa Abu Fares na Mariyah.

Pale Yasmina alipojitambulisha kwangu macho yangu yalivutwa na mwanamke mwingine. Na vidole vyake laini, alichukua samaki wa moto mdogo kwa kumkamata mkiani, akamtosa kwenye bakuli la mchuzi, akamsogeza Karibu na midomo yake, akapuliza ili ampoze halafu akammeza wote, kichwa, mifupa pamoja na mkia kama vile mtaalamu wa chakula wa kweli. Alifumba macho yake na akjitosa katika bwawa la kilele cha hisia. Kisha… kwa kutumia mkono wake mwingine, alivuta kiasi cha nywele zake zilizokuwa zimezagaa usoni kwake na kuzirejesha kuungana na nyingine zilikuwa nyuma ya sikio lake. Namna alivyovyozirekebisha nywele zake kwa usahihi mkubwa ndiko kulikonifanya niwe mdhaifu bila kinga yoyote.

Tuko katika sehemu ya 16 hivi sasa, lakini hakikisha unaipata hadithi yote kuanzia mwanzo.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.