Below are posts about citizen media in Swahili. Don't miss Global Voices in Swahili, where Global Voices posts are translated into Swahili! Read about our Lingua project to learn more about how Global Voices content is being translated into other languages.

Habari kuhusu Kiswahili

Tanzania: Mgomo wa Walimu Watikisa Nchi

Zikiwa zimebaki siku chache kabla ya kufanyika zoezi la sensa, walimu nchini Tanzania wako katika mgomo kuishinikiza serikali kuwalipa madai yao pamoja na kuboresha mishahara yao. Hatua hiyo imevuta hisia za watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii wanaojadili madhara ya mgomo huo.

Tanzania: Kufungiwa ‘Mwanahalisi’, uhuru wa habari mashakani?

  30 Julai 2012

Mnamo tarehe 30 Julai, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Msajiri wa Habari ilitangaza kulifungia kwa muda usiojulikana gazeti la Kiswahili linalotoka mara moja kila wiki la 'MwanaHalisi'. Ulimwengu wa habari umepokea taarifa hiyo kwa mshtuko mkubwa. Hivi ndivyo wanaharakati wa mtandaoni wanavyoeleza hisia zao kuhusu tangazo hilo.

Wanablogu wa Kenya: Je, ungependa kushiriki kwenye Mkutano wa Global Voices kuhusu Vyombo vya Habari vya Kiraia pasipo kulipia?

  22 Mei 2012

Mtandao wa Global Voices unawapa wanablogu sita (6) fursa ya kushiriki pasipo kulipia kwenye Mkutano wake unaohusu Vyombo vya Habari vya Kiraia utakaofanyika jijini Nairobi. Ili uweze kushinda moja ya nafasi hizo, andika makala ya walau maneno 500 au pungufu kidogo kuhusu mada hii: "Jinsi gani vyombo vya habari vya kiraia vinaweza kusaidia kufanya uchaguzi mkuu wa Kenya wa mwaka 2013 uwe wa amani".

Tanzania: Matumizi ya Vyombo vya Habari vya Kijamii kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2010 Nchini Tanzania

Tanzania inaelekea katika uchaguzi wake mkuu mnamo Oktoba 31 mwaka huu na hivi sasa kampeni za uchaguzi zinaelekea kileleni. Wakati kampeni zikipamba moto, wagombea wa nafasi ya urais, ubunge na udiwani wameanza kutumia zana mpya za mawasiliano ya jamii ili kuwasiliana na wapiga kura. Sanjari na mikutano ya kampeni, ambayo hulenga watu wengi zaidi, idadi ndogo ya wanasiasa wameanza kutumia zana za mawasiliano ya kijamii kama vile blogu, picha za video za mtandaoni, Facebook na Twitter ili kukuza mawasiliano na wapiga kura.

Wapiga picha wa Kiafrika, waandishi na wasanii wapata sauti zao kwenye blogu

Kadri Waafrika wengi wanavyozidi kugundua nguvu ya kublogu kama zana ya kutoa maoni kwa kiwango cha dunia nzima, tarakimu ya wanablogu imeongezeka na pia maudhui yanayopewa kipaumbele. Kwa tarakimu hiyo ya kukua kwa blogu, wasanii wengi wa Kiafrika wamejiunga, na ongezeko kubwa likionekana kwenye blogu za mashairi kama ilivyo kwa upigaji picha unaochipukia na blogu za sanaa za maonyesho. Tunazipitia baadhi.

Mwanamuziki mmoja wa Afrika Mashariki awashinda wengine wote kwa umaarufu wa mtandaoni duniani

Si wengi wanamfahamu kama Mwanaisha Abdalla bali Nyota Ndogo, ni jina linalojulikana kwenye kila nyumba katika Afrika Mashariki. Amekuwa akikusanya mashabiki wa mtindo wake wa kipekee wa Afrika Mashariki kwa miaka zaidi ya 4 sasa. Blogu yake, katika upande mwingine, imekuwa ikiendeshwa kwa muda wa miaka 3. Hapana shaka kuwa blogu hiyo imechangia ongezeko la kambi ya mashabiki kwenye mtandao wa intaneti.

Afrika: Ujio wa Mkonga wa Seacom Wazua Mjadala

Ujio wa mkonga unaopita chini ya bahari utakao ongeza uwezo na kupunguza gharama za intaneti barani Afrika umewasha majadiliano na mvuto katika ulimwengu wa blogu wa Afrika. Seacom, ambayo inaunganisha Afrika Kusini, Tanzania, Kenya, Uganda na Msumbiji na Ulaya pamoja na Asia, ilianza kutumika moja kwa moja Alhamisi, kwa kuziunganisha nchi za Afrika ya mashariki na Afrika ya kusini kwenye mtandao wa dunia wenye wigo mpana.

Kuhusu habari zetu za Kiswahili

sw