Wanablogu wa Kenya: Je, ungependa kushiriki kwenye Mkutano wa Global Voices kuhusu Vyombo vya Habari vya Kiraia pasipo kulipia?

sana njeri

Global Voices, ambao ni mtandao wa kimataifa wa vyombo vya habari vya kiraia utafanya Mkutano wa Global Voices 2012 kuhusu Vyombo vya Habari vya Kiraia jijini Nairobi kati ya tarehe 2 – 3 Julai, 2012. Wanablogu, wataalamu wa miundombinu ya teknolojia na wanaharakati kutoka zaidi ya nchi 60 watashiriki katika tukio hilo litakaloendeshwa katika Hoteli ya PrideInn Barabara ya Raphta Westlands.

Mtandao wa Global Voices unatoa nafasi kwa wanablogu sita (6) wanaoishi nchini Kenya kushiriki kwenye Mkutano huo bila malipo yoyote. Ili kuwania moja kati ya nafasi hizo sita, andika insha ya walau maneno 500 kuhusu mada hii: “Jinsi vyombo vya habari vya kiraia vinavyoweza kutumiwa kuhakikisha uchaguzi mkuu nchini Kenya wa mwaka 2013 unakuwa wa amani”, na tuma kiungo cha makala yako kwa georgiap at globalvoicesonline dot org, huku ukitaja “GV Summit 2012 Blogging Contest” kama kichwa cha habari.

Tarehe ya mwisho ya kupokea insha hizo ni 11 Juni, 2012. Insha zote zitasomwa na paneli ya majaji kutoka Mtandao wa Global Voices.

Tunasubiri kwa hamu kusoma makala yako!

Kwa taarifa zaidi kuhusu Mkutano wa Global Voices kuhusu Vyombo vya Habari vya Kiraia wa mwaka 2012 tafadhali tembeleahttps://summit2012.globalvoicesonline.org/.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.