Habari kuhusu Kiswahili
Miradi Ifuatayo Inalenga Kuifanya Simu yako Ikusemeshe kwa Kiswahili
Kiswahili ni lugha ya pili kuzungumzwa zaidi barani Afrika. Hata hivyo, mfumo wa utambuzi wa sauti bado haupatikani katika lugha hiyo, na kuwanyima watumiaji wengi taarifa wanazozihitaji.
Mwanaume wa Tanzania Ahukumiwa Kifungo cha Miaka Mitatu Jela kwa “Kumtukana” Rais kwenye Mtandao wa Facebook
Hukumu hii inakuja baada ya Sheria ya Makosa ya Jinai ya Tanzania kupitishwa mwaka 2015, ambayo wakosoaji wengi wanasema inawapa polisi mamlaka makubwa bila udhibiti wowote
Wa-Tanzania Wamkumbuka Baba wa Taifa Lao kwa Alama ya #DearNyerere
"#DearNyerere, enzi zako, umaarufu ulitokana na matendo mazuri kwa nchi yako, lakini siku hizi ni idadi ya wafuasi kwneye mitandao ya Instagram na Twita."
Fuatilia Uchanguzi wa Kihistoria Kuwahi Kutokea Nchini Tanzania
"Lowassa ni Robin Hood wa Kimasai. Au El Chapo wa Kitanzania. Itazame mikono aishikayo na siyo vidole avikanyagavyo."
Muswada wa Uhalifu wa Mtandaoni Unawapa Mamlaka Zaidi Polisi, Kuliko Wananchi
Wapinzani wakuu wa muswada huo kutoka kwenye asasi za kiraia wanasema wataipeleka serikali mahakamani kama rais ataidhinisha muswada huo kuwa sheria.
Wanafunzi Nchini Tanzania Kufundishwa kwa Lugha ya Kiswahili, si Kiingereza
Rais Jakaya Kikwete amezindua sera mpya ya elimu nchini Tanzania juma lililopita, ambayo pamoja na mabadiliko mengine, inaingiza rasmi Kiswahili kama lugha ya kufundishia na kujifunzia katika mfumo wa elimu.
Kupambana na Utapiamlo Nchini Rwanda Kupitia Muziki
Wanamuziki maarufu wa Rwanda King James, Miss Jojo, Riderman, Tom Close, and Urban Boyz walijiunga na mapambano dhidi ya utapiamlo nchini Rwanda kupitia video ya muziki kwenye mtandao wa YouTube. Video hiyo pia inapatikana kwa maandishi ya Kiswahili .
Kutangaza Mkutano wa Global Voices, Dar es Salaam, Novemba 2, 2014
Mkutano wa kwanza unaowakutanisha waandishi na watafsiri wa Global Voices na wadau wa Uandishi wa Kiraia hapa nchini unafanyika Dar es Salaam, Tanzania
Mkataba Uliovuja Waonyesha Hali Halisi Inayoikabili Sekta ya Gesi Nchini Tanzania
Kuvuja kwa mkataba kati ya kampuni ya Norway, statoil na serikali ya Tanzania waonesha hali ya mashaka kuhusiana na suala la mapato kwenye uvunaji wa gesi nchini Tanzania na suala la nani kunufaika na mkataba huo
Mkusanyiko wa Makala za Kuvuliwa Madaraka kwa Mbunge Maarufu Nchini Tanzania
Ben Taylor aweka mkusanyiko wa makala zinazohusiana na kuvuliwa madaraka kwa Zitto Kabwe,mbunge maarufu na kijana wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, Chadema. Zitto: […] alivuliwa nyadhifa zote rasmi na viongozi wakuu wa chama mapema siku ya ijumaa asubuhi. Zitto Kabwe hatakuwa tena Naibu katibu Mkuu wa chama wala...