makala mpya zaidi zilizoandikwa na ndesanjo macha
Afrika Kusini Yakumbuka Mashindano ya Kombe la Dunia 2010 Yalivyokuwa
Mnamo Juni 11, 2010, Afrika Kusini ilikuwa mwenyeji wa mashindano makubwa ya michezo duniani. Ni mara ya kwanza kwa mashindano hayo kufanyika barani Afrika.
Kuhusu Uamuzi wa Mahakama wa Haki ya Kusaidiwa Kufa Nchini Afrika Kusini
Profesa Pierre de Vos anaingia rasmi kwenye mjadala mkali kuhusu uwezekano wa kumsaidia mtu kufa nchini Afrika Kusini baada ya Mahakama Kuu nchini humo kuamua kwamba mtu anayekufa ana haki ya kusaidiwa kufa na daktari ili aweze kuyahitimisha maisha yake: Ni muhimu kuona kwamba hukumu hii haimlazimishi mtu kuyakatisha maisha...
Lugha za Pili Zinazoongozwa Kuzungumzwa Zaidi Afrika
Don Osborne anajadili habari iliyowekwa kwenye tovuti ya Chuo Kikuu cha Olivet Nazarene ikionesha ramani ya “Lugha za pili kuzungumzwa zaidi duniani.” Anaeleza matatizo makuu kutokana na habari hiyo: Suala la kwanza ni kudhani kwamba “lugha inayozungumzwa zaidi kwenye nchi yoyote huwa wazi; mara nyingi, ni lugha ya taifa husika.”...
Filamu ya Malawi Yawasaidia Wakulima Kujikinga na Mabadiliko ya Tabia Nchi
Filamu ya “Mbeu Yosintha” ilitengenezwa kuwasaidia wakulima na wanavijiji kujikinga na madhara ya mabadiliko ya tabia nchi, hususani kubadilika kwa majira ya mvua kwenye ukanda wa Afrika Kusini Mashariki. Filamu hiyo ni tamthlia inayowatumia wasanii wa ndani ya nchi hiyo na iliandaliwa na mwandishi wa Kimalawi Jonathan Mbuna baada ya...
Muswada wa Uhalifu wa Mtandaoni Unawapa Mamlaka Zaidi Polisi, Kuliko Wananchi
Wapinzani wakuu wa muswada huo kutoka kwenye asasi za kiraia wanasema wataipeleka serikali mahakamani kama rais ataidhinisha muswada huo kuwa sheria.
Afrika Kusini Imejitenga na Waafrika Wengine?
Mashambulizi ya hivi karibuni huko Afrika Kusini yanahusisha wahamiaji kupigwa, kuuawa, kuchomwa moto, wizi madukani pamoja na wizi wa mali zao. Watu watano wameshauawa, miongoni mwao akiwamo mvulana wa miaka 14 aliyeuawa siku ya jumatatu.
Upigaji Kura Unaendelea Tuzo za Blogu Nchini Kenya 2015
Sehemu ya kupiga kura kwenye Tuzo za Blogu Nchini Kenya inaendelea mpaka Aprili 30, 2015: Tuzo za Blogu Nchini Kenya hutafuta kuwatuza wanablogu wanaoandika mara kwa mara, wanaoandika madhui yanayosaidia, na wenye ubunifu na ugunduzi. Tuzo hizi ni jitihada za Chama cha Wanablogu Kenya (BAKE) katika kukuza ubora wa maudhui...
Baada ya Magaidi Kuua Watu Wasiopungua 147, Kulikoni Dunia Haiungani na Kenya?
Shambulio la Charlie Hebdo liliibua simanzi na mshikamano duniani kote, lakini shambulio la kigaidi nchini Kenya halijapewa uzito unaostahili.
Watu 147 Waliouawa Garissa Ni Zaidi ya Takwimu
Watumiaji wa mtandao wa Twita wameanza kutumia alama habari #147notjustanumber kuadhimisha maisha ya wahanga wa shambulio la kigaidi lililotokea kwenye Chuo Kikuu cha Garissa.
Jiandae kwa Mkutano wa MozFest Afrika Mashariki 2015
MozFestEA ni tukio litakalofanyika kuanzia Julai 17 – 19, 2015 kwenye Chuo Kikuu cha Victoria, Kampala, Uganda likiwa na maudhui makuu, “Kutafuta Majibu ya Changamoto za Afrika, kwa pamoja mtandaoni”: MozFest Afrika Mashariki ni tukio la kila mwaka linalowaleta pamoja wataalam wa elmu, wabunifu, wasomi na mafundi wa Afrika Mashariki...