Baada ya Magaidi Kuua Watu Wasiopungua 147, Kulikoni Dunia Haiungani na Kenya?

Relatives line up at the Chiromo funeral home in Nairobi to identify bodies of their kin killed after Al-Shabaab attacked Garissa University College in northeastern Kenya. Photo by Boniface Muthoni. Copyright Demotix

Ndugu wakiwa kwenye foleni kwenye sehemu itoayo huduma za mazishi jijini Nairobi kwa ajili ya kuwatambua marehemu waliouawa katika shambulio ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Garissa kilicho kaskazini mwa Kenya. Picha na Boniface Muthoni. Haki Miliki Demotix

Wanamgambo wa Al-Shabaab walishambulia Chuo Kikuu kishiriki cha Garissa nchini Kenya mnamo Aprili 2 2015, na kuwaua watu wasiopungua 147, wengi wao wakiwa ni wanafunzi, na kuwajeruhi wengine 79. Idadi hii ni mara nane ya watu waliouawa wakati wa  shambulio la Charlie Hebdo  nchini Ufaransa, liliua watu wapatao 17, lakini inashangaza kwamba tukio baya kabisa la Garissa halijaonekana kuifanya dunia itoe mshikamano kwa kiwango kile kile kama ilivyokuwa kwenye shambulio la Paris.

Hali kama hiyo ilijitokeza baada ya  mauaji ya Baga  nchini Naijeria, yaliyotokea karibu wakati huo huo wa mauaji ya Charlie Hebdo. Wakati tukio la Charlie hebdo lilivuta  hisia za hisia za watu wengi huku zaidi ya wakuu 40 wa nchi  walishiriki kwenye mkutano  wa mshikamano wa kitaifa, tukio la Mauaji ya Baga halikupewa uzito unaostahili.

Katika shabulio la kutisha la Garissa, watumiaji wa mtandao wa twita walikuwa wepesi kugundua kwamba dunia haikustuka. Shekhar Kapur kutoka Mumbai, India, alihitimisha:

Kutokuwepo kwa mwitikio wa kimataifa kwenye shambulio la Garissa ukilinganisha na Lile la Charlie inaonesha jinsi dunia isivyojali wengine

While Idriss Ali Nassah observed:

Ulikimbilia kampeni ya #ShambuliolaCharlie. Ukabadili mpaka picha ya utambulisho wako, lakini hujasema lolote kuhusu #ShambuliolaGarrisa. Hebu jiulize kwa nini?

Ngoja tusubiri tuone marais wangapi wa Afrika waliokimbilia kwenda Paris kuandamana kuonesha mshikamano watakwenda Kenya kulaani shambulio la Garissa

Mtumiaji wa mtandao wa twita ajiiate Life is sacred everywhere, @borderlessciti aliandika akielekeza twiti yake kwa mhariri mkuu mtendaji wa vyombo maarufu vya habari vya Oprah Winfrey na Huffington Post Arianna Huffington:

@ariannahuff Kila uhai wa mwanadamu una thamani, iwe ni Paris au Garissa!

‘Zima taarifa za habari’

Wachunguzi walikosoa kile kilichokuwa kikitangazwa na vyombo vya habari vya ki-Magharibi na walishambulia, hali kadhalika.

Baada ya CNN kukosea na kuiweka Tanzania kwenye eneo la Uganda na Nairobi kuonekana iko Nigeria kwenye ramani ya Afrika Mashariki, Blogu ya Africa is a Country blog ilishauri kwamba watu wazime televisheni zao ili waweze kuelewa shambulio hili:

Ili kuelewa shambulio hili lililofanywa na Al Shabaab kwenye Chuo Kikuu cha Garissa karibu na mpaka wa Kenya na Somalia (takwimu rasmi ni vifo 148; wengine wanasema 200), pengine utahitaji kzima taarifa za habari kwenye televisheni. Hasa kwa sababu CNN imeihamishia Nairobi kwenda Naijeria na Tanzania kwenda Uganda. Tusichokijua ni namna gani mashambulizi haya yataelezewa ndani ya masaa machache yajayo na namna gani serikali ya Kenya itashughulikia janga hili (tayari wanalaumu mahakama na siku za nyuma waliwahusisha wa-Somali pamoja na kuwa na ushahidi mdogo). Kilichomuhimu ni maoni ya umma. Kwa hiyo, kama tulivyofanya wakati wa shambulio lililopangwa na Al Shabaab kwenye jengo la kibiashara la Westgate kwenye mji mkuu wa Kenya, Nairobi, tumekusanya viungo vingi, ikiwa ni pamoja na anuani za mtandao wa twita, tunapendekeza uzisome au kuzifuatilia.

Idriss Ali Nassah alisisitiza uhitaji wa Afrika kutangaza habari zake yenyewe:

BBC wanatangaza mdahalo, CNN haina habari na mambo mengine ziadi ya mpango wa nyuklia wa Iran. Afrika inahitaji vyombo vyake vya hbari kusimuliza habari zake yenyewe

Mtandao wa KiGossip.Com uishangaa kwa nini mwandishi wa habari wa CNN alimwuliza mtu aliyenusurika kifo kama ameogopa:

Kwa hiyo, mwandishi wa habari wa CNN alimwuliza mtu aliyenusurika kifo kwenye shambulio la Garissa: “HIVI ULIOGOPA'? Huu ni UPUUZI…kwa nini hajafukuzwa?

Hata hivyo, watumiaji wachache wa mtandao wa twita walibaini kwamba hata vyombo vya ndani ya bara la Afrika havifanyi kazi nzuri:

Tukubaliane kwamba vyombo vya ndani navyo vimefanya kazi mbaya katika kutangaza habari za shambulio la Garissa. Vichwa vya habari vya kidaku na kutoa habari zisizojitosheleza

Gazeti la @StandardKenya limechapisha picha za familia zinazoomboleza lakini likinukuu wanasiasa. Aibu yenu.

Waafrika wanazilaumu nchi za Magharibi kwa kuachana na habari za Shambulio la Garissa mapema lakini hata vyombo vyenu navyo viliachana na habari hizo mapema

JuwelsM alihoji kwamba Waafrika waanze kuamua mambo gani yana uzito kwao:

Sote tuna hatia kwa kujipuuza wenyewe. Labda tuanze kuachana na kasumba ya kusubiri nchi za Magharibi ziamue nini kina umuhimu kwetu.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.