Jinsi Mauaji ya mwanamuziki Hachalu Hundessa yalivyochochea uvunjifu wa amani nchini Ethiopia: Sehemu Ya ll

Hachalu Hundessa akifanya mahojiano na OMN kupitia Firaabeek Entertainment / CC BY 3.0.Dondoo ya Mhariri: Haya ni mahojiano ya pande mbili yenye uchambuzi wa Hachalu Hundessa, mwanamuziki mkubwa wa Oromi ambaye mauaji yake yalisababisha vurugu za itikadi za kidini na kikabila yakichochewa na uvumi ulioenea mitandaoni. Soma sehemu ya I hapa

Ndani ya saa moja baada ya mauaji ya Mwanamuziki Hachalu Hundessa yaliyotokea Juni 29 huko Addis Ababa, wananchi mitandaoni walikuja na picha zikionesha nadharia za makubaliano ya uovu, hotuba za chuki na kampeni za uvumi wa uongo hasa katika mtandao wa Facebook, Tweeter na YouTube.  

Nadhari hizi nyingi zinaunganishwa na jambo la Kihistoria ambalo limekuwa mwiba katika mahusiano baina ya jamii za Amhara na Omoro. Hachalu ni Muoromo ambaye aliandika nyimbo za kukosoa na kuongelea wazi kuhusu mpasuko wa Kisiasa ndani ya Ethiopia. 

Habari zilianza kuvumishwa kwamba mauaji ya Hachalu yaliratibiwa na mamlaka za serikali na kwa kiasi kikubwa na Waziri Mkuu Abiy Ahmed, na watu wanaoishi nje ya nchi wao wanaona kama vile watu wa kabila la Amhara ndio wahanga wa jambo hilo.  Matumizi ya neno neftegna au “mtumia bunduki,” mara zote hutumika kama tafsida kwa filimbi ya mbwa katika lugha ya watu wa Amhara, ambao ni kabila la pili kwa ukubwa nchini Ethiopia wakilifuatia kabila la Oromi.

Kati ya nadharia hizi, moja ambayo ni maarufu zaidi ni ile inayodai kwamba maoni ya kudhalilisha ya Hachalu dhidi ya sanamu ya Menelik II wakati akifanya mahojiano na Oromia Media Network (OMN) wiki moja kabla ya kifo chake yalichochea “neftegna” na kupelekea kuuawa kwake. (Sanamu imeendelea kuwa chanzo cha uhasama baina ya viongozi wa Kisiasa kutoka Oromo na wale wa Amhara).

Tangu kuuawa kwa Hachalu  OMN imerusha vipande vidogo vidogo vya makala huko YouTube na Facebook, na inakadiriwa kwamba kurasa hizo zimetembelewa na idadi ya watu kuanzia 10,000 mpaka 200,000, na hii inaonesha sura tofauti tofauti ya nadharia hii – kwamba watu wa Amhara walihusika kwa namna fulani katika mauaji ya Hachalu.

Inaonekana kama vile wanaoiunga mkono nadharia hii wanapitia mistari ya maneno katika mahojiano aliyoyafanya na OMN  wakitafuta upenyo wa kuyapa matamanio yao nafasi wanayoitaka. 

Mitazamo hii yenye shutuma inasambaa kirahisi sana mpaka kufikia vituo vya runinga za setilaiti. Baadhi ya “vichwa” ambavyo viko diaspora vimerudia shutuma hizi ambazo hazijathibitishwa- hasa kwa vyanzo vikuu vya habari pinzani ambavyo ni: OMN na Tigray Media House (TMH).

Nadharia hii ilipewa uzito mkubwa zaidi hasa pale wanasiasa wakubwa akiwemo Ilhan Omar Mwakilishi wa Jimbo la Minnesota, ambapo ni nyumbani kwa Waoromo wengi wa diaspora huko Marekani aliposhirikisha taarifa ya New York Times kuhusu mauaji ya Hachalu ikiwa na maoni yenye shutuma:

Wakati huo huo shutuma za uongo na za kupotosha ziliibuka katika mjadala wa wapi Hachalu anapaswa kuzikwa. Baadhi ya wanaharakati wa Oromo waliopo nje ya nchi walisema kuwa mamlaka za serikali ziliilazimisha familia ya Hachalu kumzika huko mjini kwao Ambo. Wengine wakazilaumu mamlaka kwa kuyaharakisha mazishi huko Addis Ababa ili kuficha ushahidi wa mauaji.  Tuhuma hizi zilichochea zaidi hamaki baina ya makundi ya kikabila. Familia ya Hachalu na rafiki zake wa karibu walizipinga tuhuma hizo kwa kuutaarifu umma kwamba yalikuwa ni maamuzi yao kumzika kijana wao huko Ambo.

Baada ya vurugu na uharibifu wa mali uliokuwa ukiwalenga watu wasio Waoromo au Waislam katika maeneo ya Oromo, wananchi wengi wa mitandaoni walilitazama jambo hilo kama matokeo  yasiyozuilika kutokana na shutuma zilizolenga utambulisho wa wauaji wa Hachalu – zilienezwa zaidi kupitia Facebook na OMN. 

OMN, tayari wako kikaangoni kwa kukata vipengele muhimu katika mahojiano waliyofanya na Hachalu na kisha walirusha moja kwa moja wito wa mauaji dhidi ya watu wa Amhara, muda mchache baada ya kuuawa kwa Hachalu:

Baadaye tena, wanajamii wa jumuiya ya Waoromo wa diaspora waliendelea kusisitiza kwamba vurugu zilizofanywa na vyombo vya serikali ni kwa sababu vinaongozwa na watu wa Amhara.

Wananchi wengine wa mitandaoni walisema kwamba mamlaka za Ethiopia ni ushirika wa baadhi  ya vikundi vya watu – makundi ya wanaharakati na wanasiasa – ambao wamebeba chuki za kidini na kikabila ndani na nje ya mitandao. 

Kuliweka pamoja fumbo la siasa.

Wakati shutuma tele zikiendelea kuenea katika mitandao ya kijamii, mamlaka za serikali zimetoa nadharia moja kuhusu kifo cha Hachalu, ambapo inaonekana kuwa na mashiko.

Mamlaka sasa zinashikilia nadharia ya kwamba mauaji yalifanywa na makundi mawili pinzani yakiwa na malengo tofauti lakini wakiwa na nia moja ya kumuua Hachalu. Kikundi cha kwanza ni Tigrayan People's Liberation Front (TPLF) na kundi la pili ni OLF-Shane. 

 TPLF (mwanzo walikuwa sehemu ya chama tawala cha sasa Ethiopian People's Revolutionary Democratic Front) iliratibu usalama wa Ethiopia kwa miaka 27 kabla ya kuondolewa madarakani hapo Aprili 2018. Hachalu alikuwa akiupinga wazi wazi uongozi wa TPLF na alitumia maisha yake kupigana dhidi yao. 

Mwaka  2017, katika tamasha lililorushwa nchi nzima kwa runinga,  likiwa na lengo la kuwasaidia watu wa jamii ya Oromo ambao walikuwa wakimbizi kutoka ukanda wa Somali, aliwakosoa TPLF kwa ujasiri mkubwa. 

https://www.youtube.com/watch?v=UoQiCFN0Ag4

Tukiongea kisiasa, TPLF inamuhusisha Abiy  na Ethiopia ya Kifalme, wakimtuhumu Abiy kwa kuleta masalia yake katika serikali ya sasa. Wanafaidika na tuhuma za kwamba vurugu za sasa ni makosa ya serikali ya Abiy ambaye ameshindwa kutoa usalama kwa Taifa . 

Utawala wa Abiy umezipinga shutuma hizo na kuitupia lawama TPLF, ambapo wanawatuhumu kwa kutaka kuleta vurugu na kulazimisha mabadiliko ya uongozi nchini Ethiopia.

OLF-Shane ni sehemu ya shirika la kikosi cha wanamgambo cha  OLF ambacho hutumia mbinu za vurugu katika siasa wakiwa na lengo la kuijenga Oromo Huru. Kikundi hicho kinaripotiwa kuendesha kikosi cha siri cha kufanya mauaji na hujiita Abbaa Torbee, – ambapo ni msemo wa  KiAfan-Oromo unaomaanisha, “Ni zamu ya nani wiki hii?”

Abbaa Torbee inao ukurasa wake hai  huko Facebook. Kuna mamia ya akaunti za watumiaji na kwa kukadiria kuna kurasa 28 na makundi kadhaa yaliyojitoa kiuthabiti kuunga mkono kundi hili la wafanya vurugu wabobezi. Karibu kurasa zote na akaunti za watumiaji wote zilitengenezwa miaka miwili iliyopita wakati magenge kadhaa ya OLF yalipokuwa yakikaribishwa tena Ethiopia kutoka uhamishoni na ilivutia maelfu ya wafuasi huko Facebook.

Miezi iliyofuatiwa na mauaji ya Hachalu wanachama wa Abbaa Torbe waliwatishia, waliwapiga na katika mazingira mengine waliwaua wanaokiunga mkono chama Tawala cha Prosperity Party, wakiwemo raia wazawa na wageni. Wanadhani kuwa makundi hayo yananyonya isivyo sawa rasilimali za watu wa Oromo. 

Mauaji hayakuripotiwa sana  katika vyombo vya habari vya Ethiopia, sembuse vyombo vya kimataifa. 

Inaonekana Abbaa Torbee ina taarifa za ndani kuhusu vurugu zilizofuata baada ya mauaji ya Hachalu. Kubwa zaidi katika ukurasa wake maarufu walionya kwamba wataanza “kuisafisha Addis Ababa” siku moja kabla ya mauaji ya Hachalu.

Moja ya Picha za skrini ya  ikionesha bandiko katika ukurasa wa Abbaa Torbees Facebook . Picha ilipigwa Agosti 5, 2020.

Kwa kweli tufani iliibuka ndani ya Addis Ababa na makundi madogo ya kidini na kikabila yalikumbana na vurugu katika maeneo ya Oromo. Ukurasa huohuo ulibandika picha ya maiti ya Hachalu masaa machache  baada ya kuuawa kwake wakiituhumu serikali kumuua. 

Pia baadhi ya kurasa za Abbaa Torbe Facebook zilitoa wito kwa waandamanaji wa ki-Oromo kujongea kuelekea Addis Ababa na kuibomoa sanamu ya Menelik II

Picha ya skrini kuonesha bandiko kutoka katika ukurasa Abbaa Torbee huko Facebook. Picha ilipigwa  Agosti 5, 2020.

Kwa waangalizi wa karibu wa kampeni hii ya kupotosha nchini Ethiopia, jambo hili sio geni kabisa. Inakukumbusha wakati wa majira ya joto mwaka 2019, wakati makundi pinzani ya kikabila na kidini miongoni mwa wanazuoni wa ki-Amhara walipozuia shambulio la mauaji ya viongozi wakuu wa serikali katika jimbo la Amhara. Kurasa za Facebook zilizohusishwa na wazalendo wa ki-Amhara zilisambaza uvumi kwamba mashambulizi hayo yalikuwa sehemu ya hujuma zilizoandaliwa na wanazuoni wa ki-Oromo ili kufuta kabisa uongozi wa watu wa Amhara.

Kampeni zile zile za kusambaza habari potofu kuhusu mauaji ya kusikitisha ya Hachalu zinadhihirisha mgawanyiko uliopo miongoni mwa wanazuoni wa ki-Oromo. 

Kwa upande mwingine kuna wale wanaowahusisha Waamhara na mauaji ya Hachalu ikiwa ni sehemu ya kuendelea kuusimika ukabaila katika Ethiopia ya sasa  ambayo ni sehemu ya koloni la ukabaila  – na mauaji hayo ni muendelezo wa mradi huo.

Kwa upande mwingine pia kuna wale wanaoamini kwamba Waoromo wamecheza nafasi kubwa katika kuijenga Ethiopia ya sasa na mauaji ya Hachalu ni kufikisha ukingoni siasa zao zilizolegalega kwa kumuua nyota wao wa ki-Oromo na kuiimarisha mbinu yao ya siasa za utengano.

Hachalu Hundessa akifanya mahojiano na  OMN kupitia Firaabeek Entertainment / CC BY 3.0.

Nasaha za Mhariri: Huu ni uchambuzi wa sehemu mbili juu ya Hachalu Hundessa, mwanamuziki   maarufu wa ki-Oromo ambaye mauaji yake yameamsha vurugu kubwa za kidini na kikabila yaliyochochewa kutokutolewa kwa taarifa sahihi mitandaoni.  Soma Sehemu  I hapa.  

Ndani ya saa moja baada ya mauaji ya mwanamuziki Hachalu Hundessa hapo Juni 29 huko Addis Ababa, wananchi wa mitandaoni wa Ethiopia waliibuka na nadharia mbalimbali katika mitandao ya kijamii pamoja ma hotuba za chuki na & kampeni za uongo — hasa katika mitandao ya Facebook, Twitter na YouTube.

Nadharia hizi nyingi zilikenga historia ya mgawanyiko katika nchi zikiwa na maneno ya uchochezi yaliyoendeleza moto baina ya jamii za Amhara dhidi ya Oromo. Hachalu alikuwa mu-Oromo aliyeandika nyimbo za kukosoa na aliongea wazi kuhusu siasa mbovu ndani Ethiopia. 

Taarifa zilianza kusambaa kwamba mauaji ya Hachalu yakiratibiwa na serikali na kwa sehemu fulani na Waziri Mkuu Abiy Ahemd mwenyewe, baada ya taarifa hizi wanaharakati wengi wa ki-Oromo wanaokaa nje ya nchi,waliona taarifa hizi kama mzaha wa watu wa Amhara.  Neno neftegna au “mshika bunduki,” hurushiwa yakiwakilisha mbinja ya kuitia mbwa kwa watu wa Amhara, ambalo ni kabila la pili kwa ukubwa nchini Ethiopia baada ya lile la Oromo. 

Katika nadharia hizi, mojawapo inadai kwamba maoni mabaya ya  Hachalu dhidi ya sanamu ya Menelik II aliyotoa  wakati akifanya mahojiano   na chanzo cha habari cha Oromia Media Network (OMN) juma moja kabla ya kuuwawa yalichochea “neftegna”  na  kuwafanya wamuue. (Sanamu hiyo imekuwa chanzo cha hamaki baina  ya wanasiasa  wa ki-Amhara na Oromo).

Tangu kuuwawa  Hachalu, OMN imetengeneza makala mbalimbali huko YouTube na Facebook, zikiwa zimeangaliwa na wastani wa watu  10,000 mpaka zaidi ya 200,000, ambao walitoa maoni mbalimbali  kuhusu nadharia hii kwamba kwa namna fulani watu wa Amhara wamehusika na mauaji ya Hachalu.

Wanaoiunga mkono nadharia hii wameonekana kuchukua neno moja moja kutoka katika mahojiano baina ya Hachalu na OMN  na kuyatumia kwa namna wanavyotaka kuendeleza uchochezi waliokusudia.  

Madai haya yenye kufikirisha yamesambaa mpaka katika vituo vya runinga vya setilaiti.   Baadhi ya “vichwa vinavyoongea”  kutoka diaspora wamerudia madai  hayo ambayo hayajathibitishwa hasa dhidi ya vyanzo vikuu viwili vya habari vyenye upinzani vya: OMN na Tigray Media House (TMH).

Iliendelea  kuenea zaidi pale baadhi ya wanasiasa wa juu akiwemo Ilhan Omar , mwakilishi wa Marekani Wilaya namba 5 Minnesota, ambapo ni makazi makubwa ya Waoromo wanaoishi  nchi huko Marekani.  Pengine bila kukusudia alishirikisha habari ya New York Times ikiwa na nukuu yenye kiashiria:

Wakati huo huo madai ya uongo na ya kupotosha yaliibuka katika mjadala kuhusu wapi Hachalu anatakiwa kuzikwa. Baadhi ya wanaharakati Waoromo wanaokaa nje ya nchi  walisema kuwa serikali imewalazimisha familia ya Hachalu kumzika huko Ambo, kijijini kwao. Wengine walizituhumu mamlaka kwa kupeleka shughuli za maziko huko Addis Ababa, kuficha  ushahidi wa uhalifu wao. Madai hayo yalichochea zaidi moto wa ukabila. Familia ya Hachalu na marafiki wa karibu walijaribu kunanusha tuhuma hizo kwa kuutaarifu umma kuwa yalikuwa maamuzi yao kumzika mtoto wao huko Ambo.  

Baada ya vurugu na uharibifu wa mali uliolenga wale wasio Waoromo, na familia zisizo za kiislamu  wanaoishi katika maeneo ya Oromia, wananchi wengi mitandaoni wanayatazama hayo kama mambo yasiyoepukika  kutokana na madai yaliyosambaa mitandaoni  kuhusu kabila la watu wanaotuhumiwa kumuua Hachalu yaliyoeneza zaidi kupitia Facebook na OMN. 

Tayari OMN, wapo kikaangoni kwa kukata vipengele muhimu katika mahojiano baina yao na Hachalu na kisha wakarusha matangazo ya wazi wakitaka Waamhara kuuwa muda mfupi tu baada ya mauaji ya Hachalu: 

Baadaye, wanachama wa jumuiya ya Waoromo walioko diaspora waliendelea kusisitiza kuhusu vurugu zilizofanywa na serikali  ambayo imeshikiliwa na wasomi wa ki-Amhara.

Wananchi wengine mitandaoni walisema kwamba mamlaka za Ethiopia ni vikundi vya wahalifu, makundi ya wanaharakati na wanasiasa ambao wamewekeza katika chuki za kikabila ndani na nje ya mitandao ya kijamii. 

Kulitatua fumbo la Kisiasa

Wakati tetesi hizi ziliendelea kuenea huko mitandaoni, mamlaka za serikali zimetoa nadharia moja kuhusu mauaji ya Hachalu ambapo yanaonekana kuwa na vithibitisho.

Mamlaka sasa zinashikilia nadharia hiyo kuwa mauaji hayo yalifanywa na makundi mawili pinzani yakiwa na malengo tofauti lakini yanayoamini kuwa Hachalu lazima auawe. Kikundi cha kwanza ni  Tigrayan People's Liberation Front (TPLF) na cha pili ni  OLF-Shane. 

Hao TPLF (mwanzo kilikuwa sehemu ya chama ambacho kwa sasa kimekufa cha Ethiopian People's Revolutionary Democratic Front) ambapo kilidhibiti huduma za ulinzi na usalama wa Ethiopia kwa miaka 27  kabla kuangushwa kutoka madarakani hapo Aprili 2018. Hachalu alikuwa mpinzani wa wazi wa uongozi wa TPLF na alitumia maisha yake kupigana nao. 

Mwaka 2017, katika  tamasha la kitaifa lilirushwa mubashara lililenga kwa kiasi kikubwa kuisaidia jamii ya Waoromo waliokuwa uhamishoni kutoka katika Mkoa wa Somali, Hachalu aliwakosoa TPLF kwa uwazi na ujasiri mkubwa.

https://www.youtube.com/watch?v=UoQiCFN0Ag4

Tukizungumza kisiasa zaidi, TPLF walimuhusianisha Abiy na Ufalme wa  Ethiopia, wakidai kuwa Abiy alikula njama na kuleta masalia ya ufalme katika serikali. Wanafaidika na uchochezi huo wa kwamba vurugu za hivi karibuni ni kwa sababu ya makosa ya serikali ya Abiy iliyoshindwa kutoa ulinzi kwa Taifa.

Utawala wa Abiy pia umekataa madai hayo na kuwalaumu TPLF, ambapo amesema wanasababisha vurugu na kutaka kubadili utawala nchini Ethiopia.

OLF-Shane ni wanamgambo waliojitenga na OLF ambao hutumia siasa za vurugu wakiwa na lengo la kusimamisha Oromia huru. Kikundi hiki kimeripotiwa kuendesha kikundi cha mauaji kinachoitwa Abbaa Torbee, – neno la ki-Afan-Oromo linalomaanisha “ni zamu ya nani wiki hii?”

Abbaa Torbee wana uwepo hai huko Facebook. Kuna mamia ya wafuasi wa  akaunti hizi na kurasa karibu 28 na makundi kadhaa ya watu waliowekeza nguvu zao katika kundi hili lenye vurugu za kutisha. Karibu makundi yote na akaunti za watumiaji hao zilitengenezwa zaidi ya miaka miwili iliyopita na pia sehemu ya vikundi vya OLF  vilikaribishwa na kurudi kutoka uhamishoni ilivutia makumi elfu ya wafuasi huko Facebook.

Katika miezi iliyofuata kabka ua mauaji ya Hachalu,In  the months leading up to Hachalu’s assassination, wanachama wa Abbaa Torbee waliwakamata wakawapiga na katika baadhi ya matukio waliwaua wageni na wenyeji wanaokiunga mkono chama tawala cha Mafanikio. Wanafikiri kwamba kikundi hicho cha watawala  wananyonya isivyo haki rasilimali za watu wa Oromo. 

Mauaji haya ni nadra sana kuonekana  katika vyombo vya habari vya Ethiopia, hata vile vya kimataifa pia.

Inaonekana kwamba Abbaa Torbee inashikilia baadhi seemedya taarifa 3ndani kuhusu vurugu zilizofuata baada ya mauaji ya Hachalu. Katika moja ya kurasa zao maarufu walionya kuwa wataanza “kuisafisha Addis Ababa”  siku moja kabla Hachalu hajauwawa

Moja ya picha ya skrini za machapisho katika ukurasa wa facebook wa  Abbaa Torbees. Picha  ilipigwa Agosti 2020.

Na  kweli vurugu ziliibuka na kusambaa ndani ya Addis Ababa na makundi madogo ya kidini na kikabila yalikumbwa na vurugu hizo katika maeneo ya Oromia. Ukurasa huo huo ulibandika picha ya maiti ya Hachalu masaa kadhaa baada ya kuuawa kwake, wakiituhumu serikali kwa kumuua. 

Pia baadhi ya kurasa za Abbaa Torbe huko Facebook iliwataka waandamanaji  wa Ki-Oromo kuandamana kuelekea Addis Ababa na kwenda kulibomoa sanamu la Menelik II

Picha ya skrini ya bandiko la  Abbaa Torbee  huko Facebook. Picha ilipigwa Agosti 5,2020

Kwa wafuatiliaji wa karibu wa  kampeni za habari zisizo sahihi nchini Ethiopia wanajua hili sio jambo geni. Ukirudi nyuma majira ya kiangazi mwaka 2019, wakati makundi mawili  observers of Ethiopian disinformation campaigns, this all sounds wildly familiar. Think back to the summer of 2019, when intra-ethnic hasimu valries   ndani ya jumuiya ya wasomi wa  Amhara yalipokuwa na mgogoro ulioisha kwa mauaji ya viongozi wa juu wa serikali katika mkoa wa Amhara. Kurasa za Facebook zilizohusianishwa na wazalendo wa ki-Amhara zilisambaza uvumi kwamba mauaji hayo yalikuwa sehemu ya mpango wa viongozi wa Ki-Oromo wa kufuta kabisa utawala wa watu wa Amhara. 

Vivyo hivyo, kampeni ya kusambaza uongo kuhusu mauaji ya Hachalu yanaonesha mgawanyiko ndani ya viongozi  wa Ki-Oromo. 

Upande mwingine kuna wale waliunganisha mauaji ya Hachalu na WaAmhara na kuitafsiri Ethiopia kama  koloni la WaAmhara na mauaji ya Hachalu ni mwendelezo wa mradi huo.

Pia kuna wale wanaoamini kuwa Waoromo wamecheza nafasi kubwa katika kuijenga Ethiopia ya sasa na wauaji wa Hachalu wanajaribu kuonesha uwezo wao kisiasa kwa kumuua nyota wa Ki-Oromo wakiwa na lengo la kuendeleza mradi wao wa siasa za utengano. 

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.