Mwaka 2020 umekuwa wa pekee—na haujakamilika bado.
Katikati ya yote, sisi wa Global Voices tumeendelea kuchapisha habari kutoka pembe zote nne za dunia, kuwaletea wasomaji wetu mitazamo ya kipekee yenye sura ya dunia kuhusu masuala kama mlipuko wa UVIKO-19, harakati za usawa wa rangi, maandamano katika nchi kama Belarus na Thailand, na zaidi, na zaidi zaidi.
Jamii ya wanablogu, waandishi, waandishi wa habari na wanaharakati wa haki za kidijitali wa Global Voices imekuwa ikifanya kazi kwa zaidi ya miaka 16 kujenga madaraja baina ya nchi na lugha mbalimbali na kutetea uhuru wa vyombo vya habari, uwazi wa Intaneti, na haki ya kila mmoja, kokote na uhuru wa kujieleza.
Tafadhali Changia Global Voices Jumanne Hii ya Utoaji
Kazi yetu na jumuiya ya waandishi wetu wa kimataifa ni ushahidi kwamba uhusiano wa binadamu bila kujali kiambaza cha tofauti mbalimbali unaweza kubadilisha namna watu wanavyouelewa ulimwengu.
Tafadhali changia leo kutusaidia kuendeleza kazi hii muhimu.
<< Changia Global Voices >>