Mwandishi wa Habari Tanzania Atekwa na Kufunguliwa Mashtaka Yenye Utata

Erick Kabendera akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari mwaka 2012, Dare s salaam. Picha na Pernille Baerendtsen, imetumika kwa ruhusa

Tarehe 29 Julai, askari kanzu 6 walimkamata kwa nguvu
Erick Kabendera nyumbani kwake jijini Dar es Salaam, Tanzania na kumuweka mahabusu. Polisi
wanasema Kabendera amekaidi agizo la kujisalimisha mwenyewe kwa minajili ya kuchunguzwa juu ya uraia wake kama ni m-Tanzania.

Kwa wiki nzima iliyopita polisi walipekua nyumba ya kabendera mara mbili, wakanyang’anya hati yake ya kusafiria, nyaraka zake nyingine binafsi na kuihoji familia yake.

Ilipofika tarehe 5 Agosti, mamlaka zikabadili hoja, Kabandera akashitakiwa kwa makosa ya utakatishaji wa fedha, kukwepa kulipa kodi kiasi cha Dola za Kimarekani 75,000, pamoja na kujihusisha na mtandao wa kiuhalifu. Makosa haya ni kwa mujibu wa hati ya mashitaka waliyonayo Shirika la Kutetea Waandishi wa Habari (CPJ). Polisi wanasema Kabendera ametenda makosa haya kwa muda wa kipindi cha miaka minne sasa tangu mwaka 2015.

Kwa mashitaka yanayomkabili Kabendera anaweza kukumbwa na hukumu ya mpaka miaka 15 jela na haruhusiwi kupata dhamana.

Magufuli wa Tanzania??

Kwanza wamemteka mwandishi, walipoona kelele zimekuwa nyingi wakadai sio m-Tanzania, nalo limekosa mashiko, sasa anashtakiwa kwa makosa ya mtandao wa kiuhalifu na kukwepa kulipa kodi. Kutanana na Erick Kabendera, Kosa lake ni kuwa mwandishi wa habari.

“Uhuru wa vyombo vya habari umezorota kwa kiwango kikubwa ndani ya kipindi hiki cha Tanzaniaya Magufuli” inaripotiwa na CPJ.

Muwakilishi wa Taasisi ya Kuwatetea Waandishi wa Habari (CPJ) katika nchi za kusini mwa Sahara, Muthoka Mumo anasema:

Inaonekana kwamba kwa muda wote wa wiki iliyopita mamlaka zimekuwa zikitafuta namna ya kuthibitisha sababu za kumuweka kizuizini, mwandishi- huru huyu na mkosoaji. Kwanza walidai walidai kwamba uraia wa Erick Kabendera hauleweki, leo hii wameongeza mashtaka mengine tofauti kabisa, ambayo yanafanya tujiuliza sababu ya nia ya wao kumshikilia.

Kama mwandishi wa habari Kabendera amekuwa akiukosoa utawala wa Rais John Magufuli na mara nyingi amekuwa akisimamia upande wa uhuru wa habari. Ameripoti kwenye vyombo vya habari vya ndani na vya kimataifa kama vile The Guardian, African Arguments na The East African

kuhusu siasa za Tanzania na namna zinavyowagawa watu.

JJebra Kambole, ambaye ni wakili wa Kabendera anasema, malamka pia zilimshtumu Kabendera kwa kauli za uchochezi dhidi ya serikali kupitia makala yake iliyochapishwa kwenye gazeti la The Economist, yenye kichwa cha habari kisemacho “ John Magufuli anakandamiza uhuru wa habari Tanzania. Hata hivyo mashtaka haya yaliondolewa baadae.

Uraia umefanywa kama nyenzo ya kuwanyamazisha watu

Familia ya kabendera inasema, hii siyo mara ya kwanza serikali kuuliza kuhusu uraia wa kabendera. Mwaka 2013 pia serikali ilimfungulia mashtaka yanayofanana na haya lakini kesi ilifutwa baadae, hili ni kwa mujibu wa The Citizen. Kabendera kwa wakati ule aliona kwamba mamlaka zilitaka kutumia suala la kuchunguza uraia wake kama namna ya kumnyamazisha.

Mwaka jana pia, gazeti la The Citizen liliripoti kesi kadhaaa ambazo serikali ilitumia suala la kuhoji uraiakama chombo cha kunyamazisha ukosoaji nchini Tanzania. Aidan Eyakuze, mkurugenzi mtendaji wa Twaweza, asasi ya kiraia, waliojikita kwenye sauti za Wananchi , alisema mamlaka zimemnyang’anya hati yake ya kusafiria na kukatazwa kusafiri wakati uchunguzi wa uraia wake ukiendelea.

Wiki mbili kabla ya tukio hilo, Twaweza walitoa taarifa ya matokeo ya utafiti ulioitwa “Kusema ukweli kwa wenye madaraka? Maoni ya wananchi kwenye Siasa za Tanzania” Tume ya sayansi na teknolojia (Costech) ilidai kwamba utafiti huo haukuwa na kibali na ikatishia kuchukua hatua za kisheria lakini baadaye kesi ilifutwa, hii ni kwa mujibu wa makala hiyo hiyo ya gazeti la The Citizen.

Katika miaka ya hivi karibuni Tanzania imeleta marekebisho mengi ya sheria zinazowalenga wablogu na vyombo vya habari , mashirika ya kiraia,, mashirika ya sanaa na utamaduni na pamoja na wanataaluma na watafiti hatua inayochukuliwa na wachunguzi wa mambo wanaoikosoa serikali kama jaribio la kudhibiti taarifa zinazosikika kutoka Tanzania na kuminya uhusu wa kujieleza na haki za kisiasa.

#FreeErickKabendera

Mamia ya waandishi wa habari, wanaharakati za haki za binadamu, viongozi walioguswa na wananchi wamejaa kwenye mitandao ya kijamii wakidiu kuachiwa kwa Kabendera:

AFEX Africa wanaita mashataka hayo kuwa ni “makusudi ya wazi ya matumizi ya nguvu””

Kabendera, ambaye mara nyingi amekuwa akiwafunza na kuwahamasisha waandishi wachanga, amemfanya aliyewahi kuwa mwanafunzi wake kutuma ujumbe huu kutoka mtandao wa twita:

Nilikukutana na Erick Kabendera mara moja tu katika maisha yangu, na kwa muda usiozidi dakika 80. Alikuja kama mkufunzi aliyealikwa kuja kutufundisha (shule ya uandishi wa habari na mawasiliano kwa umma- @UniofDar). Lakini pamoja na kuwa nasi kwa muda mfupi, nilijifunza mengi kutoka kwake. Kwa kweli alinihamasisha sana #100K4Erick

Mtumiaji mwingine wa mtandaoni aanafikiri kukamatwa kwa Kabendera na kubambikiwa makosa ni alama ya tahadhari kwa wananchi wengine:

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.