Waganda Wafanya Maandamano ya Amani Mitaani kwa Kuchoshwa na Mauaji ya Wanawake

Waganda wakiwa kwenye maandano kupinga kutekwa na kuuawa kwa wanawake kulikokithiri. Picha na Katumba Badru,na imetumika kwa ruhusa.

Tangu 2015, karibu wanawake waki-Ganda 42 wametekwa, kulemazwa na wengine kuuawa katika mji mkuu Kampala nusu yao ni ndani ya miezi mitatu katika mwaka 2017. Wengine walikutwa na alama za kuteswa kikatili na kufanyiwa unyanyasaji wa kijinsia.
Mlolongo wa mauaji ya kutisha nchini Uganda yanafanana yanavyotokea. Hakuna juhudi zozote zilizochukuliwa lakini uchawi ndio nadharia maarufu inakubalika Mamlaka hazijamshtaki mshukiwa hata mmoja.
Wanawake wa Uganda waliona wanahaja ya kufanya jambo.
Tarehe 30, mwezi Juni 2018, maandamano ya kikundi cha wanawake wafanyakazi (WPWG) kikuungwa mkono na wanaharakati kutoka nchi nyingine, waliamua kufanya maandano ya amani katika mji mkuu Kampala kupinga utekaji na mauaji yanalenga wanawake Uganda.

Teddy Nakacwa 30
Regina Zawedde 60, Bulaga Mityana
Beatrice Mudondo mwanafunzi wa Chuo kikuu cha Makerere Kitivo cha Biashara
Nansubuga Patricia alias Proscovia
Desire Mirembe mwanafunzi wa mwaka wa kwanza chuo kikuu cha Makerere
Nampijja Juliet alias Nantabazi
Rehema Nassali miaka 14 mwanafunzi shule ya msingi Buganda Road
Allen Ampumuza 17 kutoka Kabale
Birungi Maria
Josephine Nakazibwe
Penina Kobusingye mwanafunzi wa chuo kikuu cha Makerere
Juliet Kyandali kutoka Nansana
Gorret Nansubuga alias Jamila miaka 31 kutoka Halmashauri ya Mji Katabi
Dona Zakanya alias Aisha Kasowole miaka 27 mfanyakazi wa jinsia
Nora Wanyama 18 mwanafunzi shule ya sekondari ya Airforce Entebbe
Rose Nakimuli 27
Sara Nakajjo Nakintu 35 mama wa watoto watano
Aisha Nakasinde 25 muchuuzi wa mihogo halmashauri ya mji Katabi
Jenifer Namwanje 20
Hellen Ayebazibwe kutoka Makindye, Kampala.
Nakajjo Sarah
Emily Akite mwanafunzi wa Chuo kikuu cha Makerere kitivo cha Biashara
Namuwonge Jenifer
Nalule Jalia
Nabilanda Mary alias Maria
Suzana Magara 28
Charity Kyohirwe mmilki wa mgahawa barabara ya Masajja Entebbe
Lowena Murungi
Jackline Masibo mama wa watoto wanne na mfanyabiashara katika mji wa Busia
Brinah Nalule 17 mwanafunzi YMCA Buwambo
Rose Nakisekka 17 mkazi wa Kigo Villa- Maria wilaya kalungu
Dorcus Nakiwunga
Israel Namalego

Kwa hiyo naandamana, niwakumbuke, hawakupewa haki yoyote na hakuna aliyekamatwa kwa ajili ya vifo hivi vya kutisha. Lakini nawathamini. Nawafikilia, familia na marafiki waliowaacha hakuna kizuizi bali hofu na hasira.

Global Voices ilihudhuria maandamano hayo na kiongozi wa kikundi cha wanawake wafanyakazi Dr. Stella Nyanzi aliuambia umati uliohudhuria kwamba wanawake wamejitoa kufanya ufuatiliaji wa haki kwa familia za waliouwa na pia kushinikiza kuchukuliwa hatua dhidi ya unyanyasaji dhidi ya wanawake. Halafu, mwanaharakati mwezao Patricia twasiima alisoma majina ya wanawake 42 waliouwawa.
Mapema askari walizuia waandamanaji kwa kudai kwamba masuala ambayo wanawake hao wanayapinga tayari yalishatatuliwa baada ya Rais Mseven alipohutubia taifa juu ya mikakati yake 10 ya kurejesha amani Uganda.

Barua kutoka kwa kamishina wa polisi ilisema:

Mnaarifiwa kuwa maandamano yaliyolenga kuongeza uelewa na kueleza kuchukizwa kutekwna vifo vingi vya wanawake / wasichana hayawezi kuruhusiwa kufanyika kama yalivyokuwa yamepangwa.

Hata hivyo wanawake walidhamiria kuendelea na maandamano:

Hatutaacha kuzungumza, kufikiria na maombi dhidi ya nguvu za askari polisi na serikali ambavyo vinatumia fedha za walipa kodi. Ni muda wa vitendo kwa hiyo uungana nasi kesho pale Centenary Park tutakapokuwa tunadai majibu ya maswali ambayo hayajajibiwa.

Jaribio la kuzuia lilichochea wananchi wakiwemo waandishi wa habari, wanaume na wanawake kuunga mkono zaidi na kuapa kujiunga katika maandamano.

Mwandishi wa habari Daniel Kalinaki alitoa maoni yake katika gazeti la Daily Monitor kwamba ujumbe mwingi kupitia Twitter ndio uliomfanya ajiunge katika maandamano:

Hivyo nitakuwa kwenye maandamano na binti yangu. Tutashikana mikono na kutembea pamoja na wengine bila silaha na kwa amani. Ninamtaka aipende nchi yake na kujifunza kusimama na kudai kama mwanamke kijana wa kiafrika. Atakapokuwa pamoja na wengine kama yeye watakuwa wakombozi wa waliovunja moyo, waliopigwa na kuupuzwa. Karibu kwenye paredi ya waafrika – na ninamatumaini polisi wapo makini vya kutosha kutotia doa la damu maandamano.

Mujuni Raymond ambaye ni mwandishi wa habari za runinga alisema kuwa naye angejiunga na maandamano hayo pia:

Nimekuwa kwenye matukio ya mauaji ya wanawake karibu 13, nimeona maisha yao yalivyokatishwa vya kutisha. Ubinadamu ni kuwaombea na kuwa na matumaini. Lazima kuchukua hatua.

Mwishowe, askari polisi walikubali. Maandamano hayo ya wanawake yalifuata sana miongozo iliyotolewa na askari polisi.
Hii ni mara ya kwanza maandamano ya amani kufanywa na wanaharakati tangu kupitishwa sheria tatanishi ya usimamizi wa amani ya umma ya mwaka 2013, ambayo inampa mkuu wa polisi uhuru mkubwa wa kuruhusu au kuzuia mkusanyiko wa watu. Maandamano yaliyofuata baada ya sheria hiyo kupitishwa yalibadilika kuwa vurugu.

Wanawake wa Uganda wamethibitisha kuwa maandamano sio vurugu

Maandamano hayo yalileta msukumo mkubwa kwa viongozi sio tu kuhakikisha usalama kwa wanawake bali pia kusimamia katiba ya watu wa Uganda na kuheshimu haki ya wananchi ya uhuru wa kukusanyika.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.